Yule ng'ombe hakuuzwa tena

Yule ng'ombe hakuuzwa tena

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,683
Reaction score
14,066
Ni ng'ombe jike katika familia fulani...huyu ng'ombe alikuwa anakamuliwa maziwa na kuleta riziki kwenye hiyo familia.

Mtoto wa kwanza mpaka wa mwisho kwenye hiyo familia alikuzwa na maziwa ya huyo ng'ombe pia vitu mbalimbali vilipatikana kwa faida ya maziwa yaliyokuwa yanauzwa.

Miaka ikapita ng'ombe akazeeka akawa hatoi tena maziwa...basi familia ikaona vyema imuuze huyo ng'ombe kwa wachinjaji.

Wanunuzi wakaja kumkagua wakaona kwamba amenenepeshwa vyema na anafaa basi wakatoa fedha kiasi walichokubaliana na kuanza kumtoa bandani.

Ng'ombe akawa analia kwa uchungu kama vile binadamu mbaya zaidi watoto wote toka yule wa kwanza mpaka wa mwisho walikuwa wanashuhudia tukio hili..ng'ombe anapiga hatua mbili anageuka anatoa mlio wa huzuni mpaka wale watoto nao wakaanza kulia yule baba na yule mama wenye ng'ombe wakaghairi.

Ghafla yule baba akapaza sauti..AISEEE simameni huyu ng'ombe hauzwi tena chukueni hela yenu.
NG'OMBE ALIRUDISHWA BANDANI.

Hiki kisa ni kama cha kipuuzi lakini ni cha miaka mingi iliyopita na kila ninapokumbuka huwa natafakari sana kitu ROHO.....Roho is anaza samsing
 
Back
Top Bottom