KATUNZI THE YOUNG
Member
- Jan 2, 2015
- 37
- 3
Ndugu zangu leo hii naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa. Yupo mwalimu aliyejulikana kwa jina la Lweshabula Kyabugera kutoka wilaya ya Muleba.
Akiwa kama mtaalamu wa kwanza katika wilaya hiyo kama mwalimu wa viziwi aliweza kufungua vituo viwili kwa gharama zake mwenyewe.
1. SHULE YA MSINGI RUBYA''B''
Akikusanya watoto kutoka maeneo ya Omukitenge, Kanyambogo, Kitarabwa, Kalanda, kashenshero, Omukigando na maeneo yote yaliyoko pembezoni mwa kata zinazolizunguka eneo la Rubya. Mnamo mwaka 2008 ndo alikamilisha na kuanzisha kituo rasmi.
2.SHULE YA MSINGI KAIGARA 2009
Baada ya utendaji kazi wake uliotukuka kukubaliwa alihamishiwa kufungua kituo cha pili yaani Wilayani. Lakini kumbe alikuwa anafanya kazi kuwanufaisha Maafisa elimu na Waratibu wa elimu maalumu kwani kupitia mihutasari yake waliweza kuaandaa maandalio kadhaa na kujineemesha kupitia mgongo wa huyu mwalimu.
Baada ya kuona anadhulumiwa haki zake ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara aliamua kustaafu kwa hiari mwaka 2013 akiwa bado na umri wa kuchapa kazi kwani muda wake stahiki ulipaswa kuwa tar 7/1/2019.
Tunaziomba mamlaka husika zitambue uwepo wa mtu tunu kubwa aliyechapa kazi kwa uhodari makini hasa katika kuhakikisha walemavu wanapata elimu.