Yuko wapi kamanda wetu MTIKILA? Huu ndio wakati wa kuidai Tanganyika yetu

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Yuko wapi huyu jamaa. Mwanasiasa mwenye msimamo mkali katika kudai uwepo wa nchi ya Tanganganyika. Kiongozi wa kanisa aliyepindukia mipaka katika kudai haki za wanyonge. Mwanasiasa wa mahakamani na mwenyeji wa mahabusu. Mchunga kondoo wa bwana mwenye ujasiri wa kusimama hadharani na kupaza sauti yake akidai uwepo wa Tanganyika ya ukweli....yuko wapi huyu bingwa?
 
Mtikila alisha chakachuliwa siku nyingi, yeye yuko kimaslahi zaidi.Kaburi la kisiasa la Mtikila lilikuwa kwenye ule uchaguzi mdogo wa Tarime,alichukuwa fedha ya CCM kuipiga vita Chadema, na tangu pale ndiyo hajasikika tena akitoa hoja ya maana, ni kama mtu mwenye laana fulani hivi.
 
Hivi huyu Mchungaji Kanisa lake liko wapi??
Alikuaga Mtanganyika enzi hizo, kwa sasa washamchakachua, amebaki kua Mtanzania tu
 
Kweli hata mimi sijamsikia kitambo,au ameamua kuanza kushinda kanisani?
 
Mtikila alisha chakachuliwa siku nyingi, yeye yuko kimaslahi zaidi.Kaburi la kisiasa la Mtikila lilikuwa kwenye ule uchaguzi mdogo wa Tarime,alichukuwa fedha ya CCM kuipiga vita Chadema, na tangu pale ndiyo hajasikika tena akitoa hoja ya maana, ni kama mtu mwenye laana fulani hivi.

Madai yake yako wazi nawe unyajua usingoje awe kamanda yeye sasa ni zamu yako uwe Kamanda wake na wetu pia anzia alipo malizia tafadhali .
 
Hawa viongozi wa dini hawa. Usione ajabu dr Slaa naye siku moja akachakachuliwa km Mtikila.
 
Mtikila,Mrema waliweza kuwashika sikio watanzani waweze kujua wako wapi na wanaibiwa vipi lakini matokeo yake watanzania waliwasaliti kiasi kwamba wameona ni bora wageuke wasije kupotza maisha yao kwa kuwatumikia watu waoga. Huyu Dr. Slaa vile vile amejaribu alivyoweza kwa kufumua maovu ndani ya uongozi wa Magamba lakini wapi, sitashangaa kama Dr. Slaa naye akigeuka.
Tunaojua haya tumeamua kumuachia Mungu ashushe roho ya neema aidha iwabadilishe nafsi za ubinafsi walizonazo hawa Magamba au vinginevyo!!!
 
Nasikia ameenda kule mlima Sinai kuchukua amri kumi za uandaaji wa katiba mpya!!! Tumwombee Mungu arudi salam!!!
 
Hawa viongozi wa dini hawa. Usione ajabu dr Slaa naye siku moja akachakachuliwa km Mtikila.
Kwakweli sio ajabu ni kama Edward Lowasa alivyochakachuliwa na Richmond na ndio likawa kaburi lake la kisiasa na mwisho wa ndoto zake.
 
Address zak e hizi hapa..mtafute!!

Democratic Party (DP)
Party Leaders
Rev. Christopher Mtikila - Chairman
Mrs. Georgia Mtikila - Secretary General
Contact Address
Mchikichini Ilala
P.O.Box 63102 Dar es Salaam
Mob: 0713-430516
0713-625349
Email: dp- watanganyika@yahoo.com
 
Address zak e hizi hapa..mtafute!!

Democratic Party (DP)
Party Leaders
Rev. Christopher Mtikila - Chairman
Mrs. Georgia Mtikila - Secretary General
Contact Address
Mchikichini Ilala
P.O.Box 63102 Dar es Salaam
Mob: 0713-430516
0713-625349
Email: dp- watanganyika@yahoo.com

Mkuu namba ya tigo ya mshikaji napiga haipatikani . Huna nyingine?
 
Mtikila alipotezwa na Rostam, kuna kipindi Rostam alienda kutoa msaada kwenye kanisa moja hivi kama sijakosea ilikua magomeni...Mtikila akamshambulia yeye (Rostam) pamoja na hilo kanisa akidai kanisa hilo linapokea fedha za ufisadi..Kesho yake Rostam akaenda kwenye media na vielelezo tosha kuwa Mtikila nae alisha wahi kupokea msaada wa kifedha kutoka kwa Rostam, toka siku hiyo makeke ya Mtikila yakapotea kama si kufifia
 
Back
Top Bottom