MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,295
- 39,977
Ninakereka sana na huu utamaduni wa nchi yetu kuandika historia huku taarifa nyingi sana zikifichwa. Kwa mfano historia ya muungano wetu huwa inaanza na kumaliza na majina mawili tu, Nyerere na Karume. Hata kwenye uhuru asilimia kubwa anatajwa Nyerere peke yake. Inasikitisha sana.
Leo nilikuwa natazama video za mchezo wa riadha huko You Tube mara ghafla nikaona Marathon ya mwaka 1974 jumuiya ya madola kuna jina Hassan Juma, mtanzania. Ingawa hakupata medali ila alimaliza mbio kwa muda wa masaa 2:38
Kama lisivyotajwa sana jina la Suleiman Nyambui ambaye alishiriki mbio za 1500m mwaka 1974 pamoja na Filbert Bayi ndo ilivyo kwa Hassan Juma. Nitoe wito kwa mamlaka zinazohusika kuandaa hata documentary ya kuonyesha tulipotoka na tunapoenda kwenye riadha. Yaani huu mchezo anayetajwa miaka yote ni Bayi tu kiasi kwamba kuna wanaodhani Bayi bado anakimbia. Angalau sasa hivi Simbu anatajwa.
Je, Mzee Hassan Juma yuko wapi? Kuna mwenye taarifa kumhusu?
View: https://youtu.be/4fwdXKXp2co?si=JLTL_j3GEVdmkmUY