respect wa boda
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 4,556
- 3,838
Wakuu habari za kitambo kirefu....
Naam ni muda sasa umepita tangu Magufuli amteue jamaa huyu kuwa Waziri wa Wizara inayohusiana na mambo ya Mifugo. Uteuzi huo ulikuja baada ya kazi iliyoonekana kama ni ya kutukuka aliyoifanya bwana huyu alipokua N/Waziri wa Fedha.
Alipokabidhiwa Wizara hiyo alianza kwa mbwembwe nyingi kiasi akafungia Mchinjio za Vingunguti nahatimaye kuelekea Chalinze kwa aliyekuwa mwana mfalme kukagua ranchi ya Taifa.
Tangu hapo hajasikika tena, kiasi sasa wadau wananza kuhisi kwamba pengine ilikuwa nguvu ya soda. Jamaa huyu mwenye mbwembwe za hali ya juu ambaye kila mti na Mawe yaliyoonekana ni makubwa yalipitiwa nawinowenye maandishi ya jina lake wakati wa kura za maonindani ya chama chake. Haikutarajiwa kwamba atazima ghafla kiasi hicho.
Ndipo watu tunajiuliza Rais huyo wa Mawe, Miti, Milima na Michongoma kimempata nini? Kwamba ameshindwa kwenda na kasi ya Magufuli au tatizo ni nini?
Tafadhali kama unajua aliko Waziri wetu hebu tujuze.
BACK TANGANYIKA