Yu wapi Prof. Mark Mwandosya?

T1986MCK

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
210
260
Mzee huyu ameutafuta urais lakini bahati haikuwa yake. Kwenye kampeni hata hakushiriki japo alisema Magufuli ni rafiki yake.(kwenye ile script iliyosambaa wakati wa kampeini).

Prof anaonekana kuwa na uwezo na ndiyo sababu JK aliamua kumuacha kwenye baraza japo hakuwa na wizara. Rais Magufuli ukiona huyu mzee anakufaa mtumie.
 
mara ya mwisho nilimuona kwenye mahafali ya NBAA mwezi wa kumi pale bunju,alipiga hotuba iliyoenda shule..moja ya kauli zake ni"nashangaa niliingiaje kwenye siasa".
 
Kwani Mzee Sitta yuko wapi.....na vipi Mzee Wassira.Hebu tusubiri hiyo Jan 26th next year Inshaalah huenda tukapata habari zao.
 
Kwani alikuwa team gani wakati wa kampeni?

Ilikuwa bahati yake mbaya sana Prof Mwandosya hakuwa mtandao wowote ule.
Na hilo pamoja na kuwa ni la kiungwana , mtandao umembagua sana Mwandosya.(wote JK na Lowassa)

Na mkoa wa Mbeya umeathirika sana kisiasa na kimaendeleo.
 
JPM nae hakuwa na kundi....
NB: hakuna bahatimbaya...rais huchaguliwa mbinguni
 
Mzee huyu ameutafuta urais lakini bahati haikuwa yake. Kwenye kampeni hata hakushiriki japo alisema Magufuli ni rafiki yake.(kwenye ile script iliyosambaa wakati wa kampeini).

Prof anaonekana kuwa na uwezo na ndiyo sababu JK aliamua kumuacha kwenye baraza japo hakuwa na wizara. Rais Magufuli ukiona huyu mzee anakufaa mtumie.

Umri nao umeenda.Kuna mahali tukubali mtu akifikia umri unaoendana na umri wa Lowasa inabidi apumzike apishe vijana.Mwambieni na Lowasa na Sumaye Wasilalamike tu kuwa vijana hawana ajira.Ajira kuzitengeneza ni pamoja na wao kuachia ngazi za kisiasa kupisha kizazi kingine kishike kwani nafasi hizo zina posho.Haitakiwi wawe wale wale tu toka enzi za mwalimu ndio wa kutumiwa.Wanakizibia kizazi kipya nafasi ya kutumika.
 
Yule alikawa hana wizara maalum?!! Hatufai haende zake huko
 
Jamani na Mzee wa CCM imeishiwa pumzi,aliyekuwa mlezi wa waganga wa Jadi Tanzania,kwamba chama Tawala wamuombe radhi Lowasa la sivyo PATACHIMBIKA HAPA NCHINI YUKO WAPI?siyo siri kila nikikumbuka yale maneno mmh,nabaki kujisemea mwenyewe hivi wenzetu hapa pakiharibika si wanarukia ndege kwenda nchi za nje?Mtu ametumia robo tatu ya maisha yake yoote serikalini na Chama alifikia hatua ya kusema HAKUNA LOLOTE LA MAANA LILILOTENDWA NA CHAMA TAWALA,mbona jibu la hayo halihitaji uelewa na elimu ya chuo kikuu,safari ya bus toka Mbeya-Sumbawanga ilikuwa siku mbili njiani,ukisema ufike hadi Mpanda siku tano,toka Mwanza kwenda Tabora njia haikuwepo,mmh siasa ni mchezo mchafu mno.
 
kafutika kama lowassa na sumaye. usicheze na JK wewe kijana wa mujini yule.

Mzee huyu ameutafuta urais lakini bahati haikuwa yake. Kwenye kampeni hata hakushiriki japo alisema Magufuli ni rafiki yake.(kwenye ile script iliyosambaa wakati wa kampeini).

Prof anaonekana kuwa na uwezo na ndiyo sababu JK aliamua kumuacha kwenye baraza japo hakuwa na wizara. Rais Magufuli ukiona huyu mzee anakufaa mtumie.
 
Mzee huyu ameutafuta urais lakini bahati haikuwa yake. Kwenye kampeni hata hakushiriki japo alisema Magufuli ni rafiki yake.(kwenye ile script iliyosambaa wakati wa kampeini).

Prof anaonekana kuwa na uwezo na ndiyo sababu JK aliamua kumuacha kwenye baraza japo hakuwa na wizara. Rais Magufuli ukiona huyu mzee anakufaa mtumie.

Wazee wa shoneni suti walisema anajiunga UKAWA sio muda mrefu kipind kile cha kampeni so bado tunasubir ajiunge UKAWA
 
Mwandosya Hakumung'unya Kuhusu Jk Na Magufuli. Alikua Hasira Sana. Duh!
 
Back
Top Bottom