Yu wapi Pof. Mbwiliza? Mjamaa, bosi wa CCM Kivukoni aliyekataa kumdhamini JK 2005 kugombea Urais

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Wadau wa JF naomba msaada wenu, nahitaji kuonana na Profesa Mbwiliza aliyewahi kuwa Mkuu wa chuo cha CCM Kivukoni walipokuwa wananolewa makada wa CCM enzi zile za Mwalimu Nyerere.

Nafanya utafiti juu ya kuporomoka kwa vyama vya siasa vilivyowaunganisha waafrika kudai ukombozi.

Mwenye namba yake anisaidie.

Ninachojua tu ni kuwa licha ya kutumikia Wizara moja na JK akiwa naibu wake alikataa kumudhamini wakati JK akitafuta wadhamini ili apate ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM mwaka 2005. Na aliamua kumdhamini msomi mwenzake Salim A. Salim ambaye kura hazikutosha. Kipindi hicho Prof. Mbwiliza alikuwa mjumbe wa NEC akiwakilisha mkoa wa Kigoma.

Naomba namba yake tafadhali.
 
Visasi vya Kikwete kwa wale waliompinga 2005 akiwemo Mbwiliza haviishi mpaka atakapokwenda mbele ya haki; na hiyo ni moja ya sifa za kiongozi DHAIFU!!

Mimi nilimuona siku moja Dar kwenye kituo cha daladala amechoka sana!! He must be living somewhere in Dar.
 
Prof. Mbwiliza sasa hivi anaishi wilaya ya Kasulu kijiji cha Nyumbigwa , ukitaka kumpata nenda Kasulu siku hiyo hiyo ukimwuliza utapelekwa nyumbani kwake siyo mbali na mji.
 
nenda chuo kikuu huria kinondoni yupo kitengo cha political science hata ijumaa nimemwona,siyo kweli kuwa yupo kasulu
 
Prof. Mbwiliza sasa hivi anaishi wilaya ya Kasulu kijiji cha Nyumbigwa , ukitaka kumpata nenda Kasulu siku hiyo hiyo ukimwuliza utapelekwa nyumbani kwake siyo mbali na mji.

ni kweli prof mbwilliza kwa ni nyumbigwa apa kasulu lakin siyo kweli kuwa yuko kijijin.ni mhadhiri chuo kikuu uria.nitawatafta watu wa nyumbigwa wanipe contakt zake nami nitazimwaga apa
 
back 2008-2010 nilikuwa nakutana naye Tabora, tunapanda naye bodaboda, alikuwa mkufunzi MUCCOBS Tabora Centre, nilikuwa na namba yake simu iliibiwa nimeitafuta nimeikosa,
Ninaamini Prof.anaishi kwa shida kwa gharama ya dhaifu, ila prof. alikuwa anayajua haya ya sasa ya dhaifu na ndio maana hakumdhamini huyu jamaa
 
msaada wakuu jinsi ya kuanzisha uzi mpya na namna ya kuupost,kila nikisaka sehemu itakayo niwezesha kuandika thread nachemka wakuu plz.:mad::sad:
 
Wapi abdallah kigoda..huyu nae hasikiki tena tangia autake urais

Wewe mdogo wangu utakuwa na ubongo wa kuku wewe!

Yaani mpaka sasa hivi hujawahi kumsikia Abdallah Kigoda kuwa yuko wapi? Au unatania? Hebu tutajie basi angalau Mawaziri 10 wa Baraza la JK!!
 
nenda chuo kikuu huria kinondoni yupo kitengo cha political science hata ijumaa nimemwona,siyo kweli kuwa yupo kasulu

Na wala siyo kweli kwamba amejichokea kama wengine wanavyotaka kutuaminisha. Miaka kadhaa nyuma alikuwa Mkurugenzi wa Kituo cha OUT pale Tabora. Kwa maana hiyo pia huwa ni mhadhiri wa OUT, sasa mtu wa hivyo hawezi kuwa amejichokea!! MSOMI BWANA. Kwa hiyo jamaa alikuwa ameshamtathimini Mr. DHAIFU kwamba asingeweza kututoa??!
 
Alikuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro enzi za Mkapa,he was a good leader.
 
Back
Top Bottom