Yu wapi Jaji John Tendwa?

Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
27,110
39,289
Kuna msemo usemao shetani hana rafiki!!

Leo nimekumbuka aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa aliyepata kutikisa anga la siasa Za Tanzania kwa mbwembwe huku akionesha waziwazi kuibeba CCM!!

Tendwa alijawa kiburi, Jeuri na majivuno hasa!! Mara nyingi aliapa kukifutia usajili chama cha CHADEMA kiasi kwamba chama hicho kilitangaza kutoshirikiana nae!!

Nimejiuliza tu Leo yu wapi huyu mtangulizi wa Mutungi? Ya wapi matambo yake? Ki wapi kiburi chake? I wapi jeuri yake?

Anayejua alipo atujuze!!

Hii ni rejea kidogo ya siku Za nyuma

” Tendwa alikuwa mbaguzi, hakuwa mlezi wa vyama kama sheria ilivyomtaka. Alikuwa akikipendelea chama tawala na kuukandamiza upinzani hasa Chadema. Hakusimamia sheria aliyoapa kuilinda, tunashukuru Mungu amejifuta yeye kabla ya kuifuta Chadema,” alisema Dk Slaa.

“Upo usemi wa Kiswahili kuwa hata kama umefanya mema tisa jambo moja baya linaharibu yote, lakini kwa Tendwa hakuna lolote zuri alilofanya,” aliongeza Slaa.

Dk Slaa alisema mambo mawili mabaya ambayo Chadema hawatayasahau katika utumishi wa Tendwa ni pamoja na kujaribu kuitetea CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru, alipodai kuzungumza na wazee wa mila wakimuonya Godbless Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) asifike Arumeru.

“Yote yale alilenga kuitetea CCM ili ishinde, lakini Chadema iliibuka na ushindi.

Jambo lingine alisema ni kujaribu kuizuia Chadema kufanya kazi za kisiasa pale alipowaruhusu kuendelea na mkutano Arusha Mjini na baadaye mkutano huo ukapigwa mabomu na kusababisha mauaji ya wafuasi wao.

“Yale mauaji ya Januari 5, 2011 mkoani Arusha yalichangiwa na undumilakuwili wa Tendwa…mimi niliwasiliana naye mpaka dakika ya mwisho akinisisitiza tuendelee na mkutano, matokeo yake akaja kugeuka. Hakuwa kiongozi huyu bali kibaraka wa CCM.”
 
Kuna msemo usemao shetani hana rafiki!!

Leo nimekumbuka aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa aliyepata kutikisa anga la siasa Za Tanzania kwa mbwembwe huku akionesha waziwazi kuibeba CCM!!

Tendwa alijawa kiburi, Jeuri na majivuno hasa!! Mara nyingi aliapa kukifutia usajili chama cha CHADEMA kiasi kwamba chama hicho kilitangaza kutoshirikiana nae!!

Nimejiuliza tu Leo yu wapi huyu mtangulizi wa Mutungi? Ya wapi matambo yake? Ki wapi kiburi chake? I wapi jeuri yake?

Anayejua alipo atujuze!!

Hii ni rejea kidogo ya siku Za nyuma
Mara ya mwisho nilisikia ametelekezwa na Nyumba yake ndogo .

Malipo ni hapahapa
 
Yaan nilikua naisoma hii thread na picha yake ikaja kichwan na ule mwanya wake..huyu baba kama ccm haijamjengea hata mansion bas hawajamtendea haki...maana aliwabeba na ambapo hawatakiwi kubebwa...!Mungu amlaze mahali panapostahili.. (for future use☺)
 
Yaan nilikua naisoma hii thread na picha yake ikaja kichwan na ule mwanya wake..huyu baba kama ccm haijamjengea hata mansion bas hawajamtendea haki...maana aliwabeba na ambapo hawatakiwi kubebwa...!Mungu amlaze mahali panapostahili.. (for future use)

Haha nikimwangalia Mutungi afanyayo na yaliyomkuta Tendwa nasema waafrika tuna laana!!
 
Kuna msemo usemao shetani hana rafiki!!

Leo nimekumbuka aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa aliyepata kutikisa anga la siasa Za Tanzania kwa mbwembwe huku akionesha waziwazi kuibeba CCM!!

Tendwa alijawa kiburi, Jeuri na majivuno hasa!! Mara nyingi aliapa kukifutia usajili chama cha CHADEMA kiasi kwamba chama hicho kilitangaza kutoshirikiana nae!!

Nimejiuliza tu Leo yu wapi huyu mtangulizi wa Mutungi? Ya wapi matambo yake? Ki wapi kiburi chake? I wapi jeuri yake?

Anayejua alipo atujuze!!

Hii ni rejea kidogo ya siku Za nyuma
Kuko anaburudika na mafao ya uzeeni kwenye kasri lake. We u wapi?
 
Back
Top Bottom