Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,904
- 1,364
Huko mahakamani sawa alijukana lakini mitaani alifahamika zaidi wakati wa harakati za kugombea udiwani wa Manzese. Nakumbuka kijana mmoja wa manzese alikuwa na kesi ya kubambikiwa na polisi, Lamwai alipolijua hilo wakati wa kampeni alilivalia njuga na kuhakikisha kesi ile inafutwa - na hapo ndipo vijana wengi walipomuona kuwamkombozi wao.Mbona Lamwai amekuwa maarufu hata kabla ajachaguliwa Diwani wa Manzese, Kwenye Corridor za Mahakama za Tanzania jina lake si Dogo, Ni Mwalimu mzuri wa Sheria, kwamba UKIMWI unamtaiti, sina uhakika sana na hilo, mara nyingi nimetokea kufanya naye kazi kwa karibu sijaona tofauti ya Afya yake. Naona yuko fit.Kila mtu anahitaji kuombewa aliye na ........., na asiye na .............., unless kama mtu ameamua kuwa Towashi , vinginevyo huwezi kujua kesho yako.
Hapo kwenye nyekundu Mkuu, Kwa maana hiyo nimekuelewa.Lamwai alipolijua hilo wakati wa kampeni alilivalia njuga na kuhakikisha kesi ile inafutwa - na hapo ndipo vijana wengi walipomuona kuwamkombozi wao.
Yuko CCM na ana kacheo fulani as kuna siku Makamba akawa anatoa tamko alikuwa nae benet sijui ndo mwanasheria wa CCM
Siasa sio za Kuingia kichwa kichwa, thus why Dr. Slaa alimwambia yule jamaa wa UWT kama anataka siasa aende halafu wamchakachue ndio ataelewa, kuna watu wamewekeza siasaSasa Dr Lamwai si angekufa na heshima yake angekuwa pale UDSM jamani?
Namwonea huruma sana.
Jina lake limemfanya apate masumbuko. Vinginevyo hata hivyo vyeti vinavyodaiwa kuwa alinyang'anywa asingenyang'anywa.
Ninachokumbuka alirejea CCM kama sikosei, baada ya misukosuko. Hana ubavu wa kufia nchi yule. Mwoga kama bawa la kungulu.
Mdogo wake ni mpiganaji anayeitwa Joseph Selasini ni mbunge wa jimbo la Rombo kupitia CHADEMA ndiye aliyemuangusha Fisadi Mramba!
Wana JF naombeni nifahamu huyu Masumbuko Lamwai yupo wapi? anafanya nini? amezungumza lolote kuhusiana na ushindi uliotolewa na NEC kwa baba Ridhiwani? kwanini huyu mtu yupo kimya sana? nini kimemsibu kisiasa? Anatufundisha nini kuhusiana na somo la ubinafsi na ufia Nchi? Je anaweza akawa anafanana na Zito Kabwe?
Kuuliza ndiyo kujua nisaidieni.
Wana JF naombeni nifahamu huyu Masumbuko Lamwai yupo wapi? anafanya nini? amezungumza lolote kuhusiana na ushindi uliotolewa na NEC kwa baba Ridhiwani? kwanini huyu mtu yupo kimya sana? nini kimemsibu kisiasa? Anatufundisha nini kuhusiana na somo la ubinafsi na ufia Nchi? Je anaweza akawa anafanana na Zito Kabwe?
Kuuliza ndiyo kujua nisaidieni.
Dr. Masumbuko Lamwai kwa sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria (Faculty of Law) cha Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la dar es Salaam. Pia bado anaendelea na kazi yake ya Uwakili na nafikiri bado ndiye wakili mkuu wa CCM. Kwa sasa ameamua kujikita zaidi katika taaluma lakini nafikiri alimsaidia kwa hali na mali mdogo wake Joseph ili aweze kushinda ubunge wa Rombo.