Yu wapi Cheusimangala?

Kumbe humu ndani kuna wataalamu wa vina!!

hahaha kaka katavi, heri umekuwa mkweli,
katu kataa viwavi, vyenye kujaa kejeli,
hapa tu wengi wajuvi, wa vina pia na ngeli,
wakongwe na chipukizi, hao wa nzito kauli.
 
How much time did you take to produce this wonderful thing?
 
hahaha kaka katavi, heri umekuwa mkweli,
katu kataa viwavi, vyenye kujaa kejeli,
hapa tu wengi wajuvi, wa vina pia na ngeli,
wakongwe na chipukizi, hao wa nzito kauli.

Mashairi yako nimeshayatengenezea biti... Hapa nakula mziki mtamu ajabu...
 
Mie ndio Nyamihela, Uporoto cha mtoto,
Cheusi ananihala, kwa mapigo yangu moto,
Nimuitapo Mangala, lazima aitike wito,
Kashaija nina mvuto, kanijazi wetu Mola.
 
Mie ndio Nyamihela, Uporoto cha mtoto,
Cheusi ananihala, kwa mapigo yangu moto,
Nimuitapo Mangala, lazima aitike wito,
Kashaija nina mvuto, kanijazi wetu Mola.
Kelele za mlango hazimzuwi mwenye nyumba kulala na kwa taarifa yako Cheusi ana aleji na wenye hela,mi muosha vyoo mwandamizi pale Movenpick na kanipenda hivyo hivyo.Na kama unafahamu mashairi si utunge kitabu cha mashairi ?
 
Welcome back my Cheusimangala.

She has come back to me. Thank you.
 
Uko wapi Cheusimangala ???
Kwa nini unapotea hivyo?
majibu pls bi dada

Im back my dear,nilikua huko kwetu kula sikukuu na wazee na jamaa zangu,sikuweza kuwa karibu na mtandao ndio maana nikapotea.
lakini mim cjambo kabisa na nimeanza mwaka nikiwa mwenye furaha nyingi.
asanteni kwa kuonyesha kunijali.
 
samahani naomba kupinga hoja,mapenzi nayajua na kuyafahamu,muulize Uporoto01.
vile vile shavu la kaishaijabutege sijalipiga kofi bali nimeli.......
sion kwa nini kaishaijabutege ashindwe kupumua ilhal nimemtunuku nafasi maalum ktk moyo wangu.
 
Kwanini tubishane angalia signature yake kamaliza kila kitu.Weye Kasha sijui Tenga 'kusoma hujui hata picha' ?

chukua vyote NIACHIE Uporoto01.:angel:

Nataka sumu nilambe, Cheusi kanisaliti,
Kamfuata mzembe, nimekiri simpati,
Uporoto kula embe, mie nitala chapati,
Sianzishi valangati, wacha nikameze tembe.
 
chukua vyote NIACHIE Uporoto01.:angel:

Nataka sumu nilambe, Cheusi kanisaliti,
Kamfuata mzembe, nimekiri simpati,
Uporoto kula embe, mie nitala chapati,
Sianzishi valangati, wacha nikameze tembe.

pole zako ewe gwiji, wa mashairi na tenzi,
hapo yakuzidia maji, yaruka hayo mapenzi,
heri upate kilaji, kuliko hayo makonzi,
cheusi kenda na maji, kwako kaacha majonzi,

pole na sumu silambe, mola na akupe ari,
japo si lako embe, jiepushe nazo shari,
valangati usiombe, sijegeuka habari,
cheusi kenda na maji, kwako kaacha majonzi,
 
Bado mnatunga mashairi tu!

Hongereni kwa hivyo vipaji.

Mkumbuke kuwaimbia babu zenu.....sawa Judith?
 
Bado mnatunga mashairi tu!

Hongereni kwa hivyo vipaji.

Mkumbuke kuwaimbia babu zenu.....sawa Judith?

sawa babu usikonde, wajukuu tuko gado,
kukupa vyako vipande, ng'amue miaka bado,
japo huwezi makonde, huwezi kushindwa prado,
daima babu tupende, na deko japo kidogo

vipaji ni vyake mola, mbingu na yote dunia,
shairi lisilo ala, dakika moja tungia,
hata ikiwa makala, bila bei andikia,
daima babu tupende, na deko japo kidogo
 
Achana na Uporoto, atakutia msala,
Rejea kwangu mtoto, kwanini hivyo Mangala?
Nimekusanya kipato, nikakufiche mahala,
Uporoto ni kachala, Cash'ja ni kizito.

Mzee Mwenzangu Kashaija, mie hapa naona unashikilia pembe na huku nyuma akina Uporoto1 wanakamua maziwa kiulaini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…