Yoweri Museveni: Siwezi kuweka ruzuku kwenye mafuta ili yapungue bei mkajaze magari yenu kwenye starehe

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Rais Yoweri Museveni amesema yupo tayari kutoa ruzuku kwenye mbolea lakini sio kutoa ruzuku kwenye mafuta ya petroli ili Watu wakajazane na magari yao kwenye starehe zikiwemo ‘Night Clubs’ wakati tayari petroli ilishapunguzwa bei kutoka pesa za Uganda (UGX) 6,563 hadi 5,138.

Museveni (78) amesema wote wanaotaka kwenda kwenye starehe na magari yao gharama za mafuta zinatakiwa kuwa juu yao japokuwa anaweza kutoa ruzuku endapo tu bei zitayumbishwa na vikwazo vinavyowezwa kuwekwa kwao na Nchi za Magharibi ambazo hazijapendezwa na maamuzi ya Nchi hiyo kupitisha sheria dhidi ya Wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Rais Museveni ameyasema haya wakati akilihutubia Taifa kuongelea changamoto mbalimbali zinazolikabili ikiwemo mfumuko wa bei za vyakula, gharama za maisha na ufisadi na jinsi ya kuzitatua changamoto hizo wakati huu ambao Nchi za Magharibi zinatishia kuiwekea Serikali yake vikwazo vya kiuchumi baada ya kupitisha sheria dhidi ya wanaoshiriki vitendo vya ushoga
 
Back
Top Bottom