Yoweri Kaguta Museveni: We were gaining the grounds of Kampala, lead by Colonel Mahfoudh

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,275
FROM HIS OWN WORDS - YOWERI KAGUTA MUSEVENI, the President of UGANDA. " We were gaining ground of Kampala, lead by Colonel Mahfoudh and we three of us, Me, Major Marwa and Major Isonda IN A TRIANGLE and on our back, the battalion charging ahead gaining ground of Kampala in a MISSION-ACCOMPLISHED "

. Major Isonda was my Uncle as husband to my Aunt Winnie (now Rev. Winnie Mulindwa). Was a perfect Trained-Combatant and the graduate of MONDULI MILITARY ACADEMY with several SANDHURST short courses. Was a Man of MILITARY and MILITARY-INTELLIGENCE UNIT. He knew his job so well and eventually attracts love/hates to some colleagues as usual.

According to himself, his retirement " was controversial and circumstantial " as was still in love with TPDF. On the day of his funeral in 1992, his Nyamwezi-Mother cried " my Soldier, my Soldier " and never mentioned " my Son, my Son " . She knew him well as the born-Soldier. He was darling to many in the name of Military-family, the like of the late Major General JOHN WALDEN, the late Colonel CHIMPENYI, the Mozambican-Military Attaché to Tanzania and many Tanzanians and Ugandans STAR-GENERALS of the Army. He once told me that " One can work for government and goes top the dreams, BUT in no given hour, you just baunce on the ground, you fall, AND IS OVER ".

When 2 Tanzanian PMs resigned the Offices in 1992 and 2008 respectively, his word just ECHOES !

1130783

Yoweri Kaguta Museveni

1130784

Colonel Mahfouth with Mwalimu Nyerere

1130786
 
..Mahfoudh, Marwa, na Isonda, wote si Watanzania hawa?

..Ina maana Watanzania walishiriki kumuondoa Iddi Amin, halafu wakamuondoa na Tito Okello?

..Tito Okello baada ya kupinduliwa alikuja kuishi Tanzania.

NB:

..kuna mambo fulani siyaelewi vizuri kuhusu vita vya msituni vya Museveni.

cc Kichuguu, Ndahani, Nguruvi3, Manyerere Jackton
 
Mkuu JokaKuu
Kuna vitu havieleweki vizuri katika vita ya Uganda. Tatizo kubwa ni kukosekana kwa rekodi ya washiriki ambao wengi sasa wametangulia mbele ya haki.
Mara kadhaa tumsisitiza kuwa waliobaki kama Maj Gen Msuya wahojiwe na kwamba ni wakati sasa JWT wafanye declassification ya habari za vita.

Kama utakumbuka, Idd Amin alipoondoka kulikuwa na serikali na 'coup d'etat''
Kuna Yusuf Lule, kisha Godfrey Lukongwe Binaisa, halafu Paul Mwanga, Tito Okello, Milton kisha Kaguta.

Lule hakuelewana na Mwalimu na hata alipoondolewa kulikuwa na 'ridhaa kutoka Magogoni''
Binaisa hakuelewa na wanajeshi . Paul Mwanga hakuwa popular wala kukubalika Dar.
Tito Okello alionekana kama mtu anayechagiza mapinduzi na mwenye tamaa
Obote aliporudi ilikuwa visasi kwenda mbele. Kaguta akawa mtoto mpendwa kutoka Magogoni.

Katika hali kama hiyo, swali lako la '' kumuondoa Amin na Tito Okello' lina mantiki sana.
 
..Mahfoudh, Marwa, na Isonda, wote si Watanzania hawa?

..Ina maana Watanzania walishiriki kumuondoa Iddi Amin, halafu wakamuondoa na Tito Okello?

..Tito Okello baada ya kupinduliwa alikuja kuishi Tanzania.

NB:

..kuna mambo fulani siyaelewi vizuri kuhusu vita vya msituni vya Museveni.

cc Kichuguu, Ndahani, Nguruvi3, Manyerere Jackton

Thanks mkubwa. Indeed, some of these things can't be mentioned anywhere near us, normal citizens.
With these writings, I believe Col Mahfoudh was always our invisible "star boy". Hakutupwa kama inavyodhaniwa
 
FROM HIS OWN WORDS - YOWERI KAGUTA MUSEVENI, the President of UGANDA. " We were gaining ground of Kampala, lead by Colonel Mahfoudh and we three of us, Me, Major Marwa and Major Isonda IN A TRIANGLE and on our back, the battalion charging ahead gaining ground of Kampala in a MISSION-ACCOMPLISHED "

. Major Isonda was my Uncle as husband to my Aunt Winnie (now Rev. Winnie Mulindwa). Was a perfect Trained-Combatant and the graduate of MONDULI MILITARY ACADEMY with several SANDHURST short courses. Was a Man of MILITARY and MILITARY-INTELLIGENCE UNIT. He knew his job so well and eventually attracts love/hates to some colleagues as usual.

According to himself, his retirement " was controversial and circumstantial " as was still in love with TPDF. On the day of his funeral in 1992, his Nyamwezi-Mother cried " my Soldier, my Soldier " and never mentioned " my Son, my Son " . She knew him well as the born-Soldier. He was darling to many in the name of Military-family, the like of the late Major General JOHN WALDEN, the late Colonel CHIMPENYI, the Mozambican-Military Attaché to Tanzania and many Tanzanians and Ugandans STAR-GENERALS of the Army. He once told me that " One can work for government and goes top the dreams, BUT in no given hour, you just baunce on the ground, you fall, AND IS OVER ".

When 2 Tanzanian PMs resigned the Offices in 1992 and 2008 respectively, his word just ECHOES !

View attachment 1130783
Towering Kaguta Museveni

View attachment 1130784

Colonel Mahfouth with Mwalimu Nyerere

View attachment 1130786

Hii ilikuwa ni vita ya 1978-9 au ya 1985-6?
 
Thanks mkubwa. Indeed, some of these things can't be mentioned anywhere near us, normal citizens.
With these writings, I believe Col Mahfoudh was always our invisible "star boy". Hakutupwa kama inavyodhaniwa
Mkuu JokaKuu anatusaidia sana kuleta watu walioigania hii nchi lakini hawatajwi. Mkuu ahsante sana.

Ukisoma kuhusu alivyomweleza Brig. Gen Hashim Mbitta, ndivyo haswa anavyoheshimika katika frontline states.
Mzee Mbitta akitajwa na RTD kama mwenyekiti wa kamati ya ukombozi.

Kila siku alikuwa njiani aki-organize shughuli za nchi zote ndiyo maana amepewa nishani za juu alizoeleza JoKakuu.

Kifo cha Mzee Mbita kilipokelewa kwa majonzi sana katika nchi za SADCC.
Mbita alikuwa 'alama' ya akina Nyerere, Khama, ''Kaunda'' , Machel, Neto, Mugabe, Nkhomo, Tambo n.k.

Kwa bahati mbaya hapa nyumbani hakuna utaratibu wa kuwaenzi mashujaa

Siku hizi hata sherehe za kuwaadhimisha kwa kuwakumbuka hazipo na kama zipo ni ilimradi tu.
Sherehe za mashujaa haziwezi kuwa 'ufunguaji wa visima au kuzindua miradi''

Ni sherehe za kuwaeleza mashujaa wetu nini kilitokea, wapi lini na akina nani walikuwa mbele.
JWTZ ni hazina kubwa sana ya habari , sijui kwanini hawaandai documentaries !

Ilikuwa kunyunyizia kidogo, turudi kwenye mada ya Kaguta
 
..Mahfoudh, Marwa, na Isonda, wote si Watanzania hawa?

..Ina maana Watanzania walishiriki kumuondoa Iddi Amin, halafu wakamuondoa na Tito Okello?

..Tito Okello baada ya kupinduliwa alikuja kuishi Tanzania.

NB:

..kuna mambo fulani siyaelewi vizuri kuhusu vita vya msituni vya Museveni.

cc Kichuguu, Ndahani, Nguruvi3, Manyerere Jackton
Kilichonivutia katika hii artcle ni kuona ma legendary wetu walivyoingia Kampala.
 
FROM HIS OWN WORDS - YOWERI KAGUTA MUSEVENI, the President of UGANDA. " We were gaining ground of Kampala, lead by Colonel Mahfoudh and we three of us, Me, Major Marwa and Major Isonda IN A TRIANGLE and on our back, the battalion charging ahead gaining ground of Kampala in a MISSION-ACCOMPLISHED "

. Major Isonda was my Uncle as husband to my Aunt Winnie (now Rev. Winnie Mulindwa). Was a perfect Trained-Combatant and the graduate of MONDULI MILITARY ACADEMY with several SANDHURST short courses. Was a Man of MILITARY and MILITARY-INTELLIGENCE UNIT. He knew his job so well and eventually attracts love/hates to some colleagues as usual.

According to himself, his retirement " was controversial and circumstantial " as was still in love with TPDF. On the day of his funeral in 1992, his Nyamwezi-Mother cried " my Soldier, my Soldier " and never mentioned " my Son, my Son " . She knew him well as the born-Soldier. He was darling to many in the name of Military-family, the like of the late Major General JOHN WALDEN, the late Colonel CHIMPENYI, the Mozambican-Military Attaché to Tanzania and many Tanzanians and Ugandans STAR-GENERALS of the Army. He once told me that " One can work for government and goes top the dreams, BUT in no given hour, you just baunce on the ground, you fall, AND IS OVER ".

When 2 Tanzanian PMs resigned the Offices in 1992 and 2008 respectively, his word just ECHOES !

View attachment 1130783
Towering Kaguta Museveni

View attachment 1130784

Colonel Mahfouth with Mwalimu Nyerere

View attachment 1130786
Haya maelezo ya museveni sina uhakika nayo kwa vile timeline yake haieleweki sawasawa. Ninavyojua mimi Col. Mahfoudhi alikuwa na mmoja wa wahanga wa kifo cha Karume mwaka 1972, lakini Nyerere akamhifadhi kivyake vyake tu akihofia kuwa angedhuriwa kame anegerudishwa Zanzibar, alimweka huko Msumbiji ambako ndio aliendelea kuishi hadi mwisho wa maisha yake. Kwa hiyo wakati wa vita ya Uganda yeye hakuhusika kabisa kwani alikuwa akiishi Msumbiji. Utaona hata title anazotumia humo ni pamoja na Major Marwa na hapo sijui ni Major Marwa yupi kwani kama ni kamanda Marwa wakati huo alikuwa ni Brigedia aliyepandishwa kuwa Major General wakati vita inaendelea.
 
Haya maelezo ya museveni sina uhakika nayo kwa vile timeline yake haieleweki. Ninavyojua mimi Col. Mahfoudhi alikuwa na mmoja wa wahanga wa kifo cha Karume mwaka 1972, lakini Nyerere akamhifadhi kivyake vyake tu akihofia kuwa angedhuriwa akirudishwa Zanzibar, alimweka huko Msumbiji ambako ndio aliendelea kuishi hadi mwisho wa maisha yake. Kwa hiyo wakati wa vita ya Uganda yeye hakuhusikia kabisa kwani alikuwa akiishi Msumbiji. Utaona hata title anazotumia humo ni pamoja na Major Marwa na hapo sijii ni Major Marwa yupi kwani kama ni kamanda Marwa wakati huo alikuwa ni brigedia aliyepandishwa kuwa Major General wakati vita inaendelea.
Amemuongelea pia Military Atachee wa Msumbiji, inawezekana Mahfoudh utaalamu wake ulihitajika Uganda. Sina uhakika.
 
..Nadhani habari hii inahusu Museveni na NRA walivyompindua Gen.Tito Okello Lutwa mwaka 1986.

..Inajulikana kwamba Col.Mahfoudhi hakupigana ktk vita ya 1979 iliyomuondoa Iddi Amin madarakani.

..Pia nadhani Mganda aliyekuwa karibu na majeshi ya Tanzania mwaka 1979 wakati yanaingia Kampala ni Lt.Col.David Oyite Ojok, sio Yoweri Museveni.

..David Oyite Ojok ndiye aliyetangaza kwenye Radio ya Uganda kwamba utawala wa Iddi Amin umeanguka. Tanzania hawakutaka kutangaza kwa kuogopa kuonekana kuwa Tanzania inaikalia au inaitawala Uganda.
 
Nadhani upo sahihi, ni vita ya Kaguta kumuondoa Okello 1986
Kuna evidence nyingi, soma paragraph ya kwanza, Kaguta anasema walikuwa wana 'gain ground of Kampala katika Triangle''

Aliyeishika Kampala kwa mara ya kwanza ni Maj Gen Msuya tena kulitokea friendly fire.
Wakati huo Kaguta hakuwepo vitani wala Mahafoudh.
 
..Nadhani habari hii inahusu Museveni na NRA walivyompindua Gen.Tito Okello Lutwa mwaka 1986.

..Inajulikana kwamba Col.Mahfoudhi hakupigana ktk vita ya 1979 iliyomuondoa Iddi Amin madarakani.

..Pia nadhani Mganda aliyekuwa karibu na majeshi ya Tanzania mwaka 1979 wakati yanaingia Kampala ni Lt.Col.David Oyite Ojok, sio Yoweri Museveni.

..David Oyite Ojok ndiye aliyetangaza kwenye Radio ya Uganda kwamba utawala wa Iddi Amin umeanguka. Tanzania hawakutaka kutangaza kwa kuogopa kuonekana kuwa Tanzania inaikalia au inaitawala Uganda.
Ina leta maana, jaribio la kumpindua Amin la mwaka 1972 Museveni alikua mwanafunzi wa UDSM lakini alishiriki. 1979 alikua mwalimu Chuo cha Ushirika Moshi na baadae aliipeleka familia yake ukimbizini Sweden kabla hajaanza Gorilla movements.
 
Hii ni changamoto hasa... kwenye kitabu mlinzi wa Mwalimu, hata habari za jaribio la mapinduzi ya 1964 bado ziko classified
Kuna sheria yoyote ya kuruhusu baadhi ya classified information kutolewa nje baada ya muda fulani?
 
Back
Top Bottom