Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Kwa mawazo yangu,yote wanayoyasema sasa hawa wenzetu kuhususiana na madai ya wananchi ya kutaka kukamilishwa kwa mchakato wa kupata katiba mpya, ni uongo mtupu bali hofu yao kuu ni takwa lillilopo katika katiba inayopendekezwa ambalo ni kuruhusu uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi na si kitu kingine chochote.
Ukiruhusu kura ya maoni iendelee, basi Katiba mpya itakayopatikana pamoja na mapungufu yake yote,itatupelekea tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi na hii ndio hofu yao kubwa na bila shaka hii ndio sababu iliyopekekea hata mchakato wa kura ya maoni kucheleweshwa ili kusubiri uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 upite.
Kwa sasa wanapima upepo na wakiona wana hali mbaya kuelekea 2020, hii Katiba inayopendekezwa wataipotezea kabisa licha ya kuwa wao wenyewe ndio walishiriki kuiandaa kwa kiasi kikubwa baada ya wapinzani kususia mchakato ule wa kuiandaa.
Wanachotaka wapinzani kwa sasa ni pamoja na kuifanyia marekebisho katiba inayopendekezwa ili iendane na matakwa ya Rasimu ya mzee Warioba lakini nina hakika maadam ina kipengele cha kuruhusu Tume Huru(kulingana na kumbukumbu zangu),basi tutarajie figisufigisu na danadana nyingi tu katika hili.
Kwa jinsi bwana fulani anavyopenda kuosha, sidhani kama kweli angekataa sifa ya kukamilisha huu mchako tena mapema kabisa.