Hizi ni danadana tu unapiga hapa.
Mungu hayupo.
Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe na kujitetea mwenyewe kama ana huo uwezo.
Khaa! Yaani Mungu aachie kiti chake cha enzi aje umuone wewe uridhike afu arudi eti kwa sababu unataka kumuona upate uhakika🤣 and who the hell do u think u are?? Huh! Ata Farao na ufalme wote alikuja na kejeli kama hizo vikamshinda!
Kasome Kutoka 5:2
Farao akasema, “Ni nani huyo Bwana niyemsikie sauti yake, niwaache Waisraeli waende? Mimi simjui Bwana, wala sitawaacha Waisraeli waende.”
Sikia ndugu, ni heri uamini Mungu yupo uende usimkute kuliko kuamini hayupo halafu umkute! Kwani ukiamini unanyofoka ngozi au unaota mapele? Unasikia ufahari gani kutukana Mungu wako kwa uhakika hivi na hujui lolote mwenyewe ulizaliwa ukayakuta "when u go to Rome…” utamalizia..
Kama akili yako inakutuma wazungu wameandika hiki kitabu hebu na wewe kakae chini utunge chako uandike kama unaona ni rahisi sana😅 yaani waafrika kwa kuabudu mzungu hamjambo! Kila tukio kubwa mzungu mwee!🤭
Mwingine wa mfano huu ni
Nebukadneza (Danieli 3 & 4) mwanzoni alijiona kama mungu na kuamuru aabudiwe, lakini baadaye alifunuliwa ukuu wa Mungu wa kweli na kutubu. Kama unasubiri ashuke umjue basi sawa, kaa usubiri..
Msipende kujitia ujuaji kwenye mambo yaliyo makuu na njee ya uwezo ambayo hata wewe umekuta maswali yake na majibu bado hujayakubali, ipo siku utayakubali tu.. kila mtu anapokea kwa wakati wake.. ila acha kabisa kutusi kazi za Mungu, usihitaji kufanyika mfano kwa wanaokutazama ukatumika mfano wa kizazi chako…
Zaburi 14:1
Mpumbavu amesema moyoni mwake, Hakuna Mungu. Kwa mtu anayedharau uwepo wa Mungu, andiko hili linaonyesha kuwa hiyo ni kauli ya ujinga wa kiroho.
Kama shetani hujawahi kumuona ila kazi zake unazijua/unasikia kwanini za Mungu unazikataa? Unataka kumuona Mungu live ili uamini we kama nani? Kwaio nyie atheists ndio mna akili sana kuliko sisi tunaokusanyika na kumuabudu Mungu? Yani kanisa zima tumerukwa na akili kuliko wewe? Hebu jitafakari bwana! Muda unatosha kbs huu! Yaani unakaa chini unajiona una uwezo mkubwa wa kufikiri mbele za watu maelfu hmm! Atleast ungekuwa umeanzisha jambo fulani linafahamika dunia nzima kdg tungewaza.. sasa mwenzetu.. dah sitaki kuzidi kumkasirisha Mungu!
Anyways, ukitaka kumuona mungu live labda utengeneze wako, maana wa kwetu ni mtakatifu mno wenye dhambi hatuwezi kumuona kwa macho haya hakika tutakufa!
Kwaio we nenda ata kwa wahindi huko😅 siye wetu tuna njia za kuwasiliana naye aisee! Ungekuwa uko serious unataka kumjua mapema sana ungekuwa ushajipatia majibu! Kila siku watu wanakemea na pepo zinatii afu kuna we binadamu unakuwa mbishi, nimekumbuka ukisoma
Waefeso 6:12
"
Kwa maana vita vyetu si dhidi ya damu na nyama, bali dhidi ya viumbe wa giza, dhidi ya majeshi ya roho waovu katika nafasi za juu za mbinguni."_ imangine wakuu wa giza! “Falme na mamlaka”.. ila si vya damu na nyama! Ina maana tunaelewana na mapambano ya kiroho, si tu ya kimwili.
Sema nini, shetani hajakutandika kisawa sawa utamtafuta tu Huyu Mungu!🤣
Karibu kanisani kwetu uone Mungu wetu anavyopambana na maadui zetu live kama wachaw n.k, fanya masihara kabisa wakati wako waja!
Huna huo uwezo wa kuchunguza ukuu wa Mungu utaishia kukufuru tu! Eti ajitetee yani kwa ujinga wako kushindwa kuelewa neno lake, yeye aje kujinyeanyea kwako😂 ajuaye idadi ya nywele kichwani mwako na mchanga wa baharini! Ukiforce utatokwa jasho la ulimi😁
NB: MUNGU HACHUNGUZIKI!