Yesu akasema; "Simoni, acha kuvua Samaki....!"

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,


Bwana Yesu alipotembelea mto Galilaya, aliwakuta wavuvi wakivua samaki, Simoni alikuwa ni miongoni mwa wavuvi hao. Yesu akasema; " Simoni, acha kuvua samaki. E nenda ukawavue watu.


Naam. Watu wengi wanaangamia kwa kukosa uelewa. Kwa kutojitambua. Wanahitaji ukombozi wa kifikra. Na siku zote, haki uinua taifa, vivyo hivyo, dhulma huangamiza taifa. Na mahala pasipo na haki, basi, hapo hapatukuwa na amani.


Oneni, maovu yametamalaki katika dunia tunaoishi. Siku zote, kujipendelea ndilo shina la maovu. S i tuna mifano hai. Oneni, wale wenzetu waliokaa na wakaamua kuuza nyumba za Serikali. John Magufuli ni mmoja wa watu hao. John alisimamia utekelezaji wa dhulma ile kwa Watanzania.


Lililopelekea uamuzi wa hila na ghilba wa kuuza nyumba za serikali ni ubinafsi na hulka ya baadhi ya viongozi kutaka kujipendelea. Karibu wote waliouziwa au kujiuzia nyumba hizo za Serikali, nyumba za wananchi, tayari walikuwa na nyumba kabla.


Hamu inakuwa ni jambo jema, endapo binadamu ataweza kuitawala hamu yake.Tusipoitawala hamu yetu, tukaanza kujipendelea, kuwasahau wengine, basi, hilo huwa ndio chimbuko la maovu, hupelekea kutoelewana baina ya wanandugu na hata kwa marafiki walioshibana. Hupelekea vurugu na machafuko katika jamii. Tunazungumzia uwepo wa upendo, haki na usawa.


Dini nyingi zinazungumzia umuhimu wa upendo, haki na usawa katika jamii. Iwe ni Uislamu na Ukristo vivyo hivyo. " Naapa kwa zama . Hakika binadamu wote wamo katika hasara isipokuwa wale walioamini na wakafanya matendo mema. Wakahusiana na haki na wakahusiana na subira" (Koran tukufu, Surat ASWR)


Na Biblia inasema; kuwa Kaini alikuwa mtu wa kujipendelea mno, akamwua nduguye. Mfalme Saulo alijipendelea mno, akamdhulumu Daudi. Yuda alijipendelea mno, akaiba fedha za wenzake, hatimaye akamsaliti Yesu.


Na ufufuko wa Bwana Yesu utukumbushe jukumu letu la kupambana na maovu katika jamii. Utukumbushe jukumu la kusaidia kazi ya kuwakomboa kifikra wanadamu wenzetu. Kama Bwana Yesu alivyomkumbusha Simoni kwa kumwambia; " Simoni, acha kuvua samaki. E nenda ukawavue watu. Na hilo ndilo Neno la Leo. Pasaka Njema.


Maggid,
Iringa,
Jumapili, Aprili, 24, 2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
0788 111 765
 
asante mjengwa sasa nadhani unaona ufisadi wa serikari majaji wanaishi hotelini kwa sababu ya unyanganyi wa watu wachache na nguvu ya umma itawashukia kiama chao ki karibu
 
Re: Neno La Leo: Yesu Akasema; " Simoni, Acha Kuvua Samaki....!"

Bwan mjengwa, hili la kuuziana nyumba zetu linasikitisha sana ila nina imani kizazi hiki iko siku kitaweza kurejesha haki hii iliyoporwa na wajanja wachache.
 
Majid, hili suala la kuuziana nyumba za serekali ni la kusikitisha kupita kikomo, sijui serekali ilifikiria nini kwenye hili!

- Yaani utadhani ni kundi la wahuni tu walikaa wakaamua, haiingii akilini kwamba ni serekali ya watu tuliowachagua wenyewe wanaweza kuwa na ubinafsi wa kiwango hiki!!

- Kwa kweli kama wengi wanavyosema ipo siku, hata kama sio zama hizi zetu, haki yetu hiyo iliyoporwa itarudi mikononi mwetu au wanetu au wajukuu zetu!!

-Namuomba mungu iwe ni kipindi cha maisha yangu ili nisiondoke roho yangu ikiwa na sononeko hili kubwa
 
Indeed it was a very serious blunder that will haunt the Government for a long time. They should have thought much wider because what is coming out as a result, is draining the exchequer.
 
Majjid pepo la ujinga limekutoka sasa unaongea kwa uchungu wa kutaka nchi yako itumie rasilimali za taifa kwa wananchi wako heko kuliona hilo
 
Amen,Amen,Amen nawambieni!!!! Hakika kila m2 matendo yake yatafuatana naye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom