johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,957
- 141,948
Chadema ni chama kilichoaminika na kukubalika baada ya kujitanabaisha kama chama cha kutetea wanyonge na kulinda maslahi ya taifa ikiwemo kupiga vita ufisadi.
Katibu mkuu mstaafu wa chadema alisimama kidete kupigana vita hii akishirikiana na mwanaharakati wa rasilimali ya madini na mazingira Tundu Antipas Lisu.
Lakini tokea Dr Slaa aachane na Chadema na kustaafu siasa za majukwaani vita dhidi ya ufisadi pale Ufipa imekufa kabisa.
Kwa sasa si Tundu Antipas Lisu wala JJ Mnyika utakayemsikia akiwakemea mafisadi bali wao ndio wamegeuka kuwa watetezi wa mafisadi.
Najiuliza tu ile vita ya ufisadi ilikuwa ni ajenda binafsi ya Dr Slaa maana siku hizi kuzungumzia ufisadi pale Ufipa ni lazima uwe na moyo kama wa mwendawazimu hivi.
Ni hayo tu akina bwashee
Maendeleo hayana vyama!