CAG amewarahisishia kazi CHADEMA na Kibajaj kapigilia msumari wa mwisho, sema tu CHADEMA ya sasa ni butu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,562
Kesho Chadema wanaanza Mikutano yao Kusini mwa Tanzania kwenye Ngome ya CUF na ACT Wazalendo.

Chadema wanaingia kwenye Mikutano wakiwa na Hati Safi kutoka kwa CAG tofauti na wenye Ngome yao ACT wazalendo waliotuhumiwa kukwepa Withholding tax TRA.

Kwa ile Chadema ya Dr Slaa tungepata mjadala mzuri kuhusu hawa mafisadi wa November lakini Chadema ya Mnyika vitambi vingi maslahi mbele.

Niko hapa Nanjilinji na kesho nitakuwepo Masoko kuwasikiliza ndugu zangu wa Ufipa St.

Siasa ni Sayansi, Siasa siyo Uadui!
 
Huu ndiyo ile rafiki yako Zito aliita uzwazwa. Nchi inaongozwa na CCM na CAG ripoti yake inajadiliwa Bungeni na hatua kuchukuliwa na Serikali inayoongozwa na CCM. Sasa hapo CHADEMA inahusikaje?? Ubutu wake uko kwenye nini??

Ujinga kama huu ni sawa na kumlaumu jirani yako ni kwa nini mkeo hapati mimba wakati wa kwake anazaa kila baada ya miaka miwili. Mpe basi mkeo akae naye kama unataka apate mimba!!

Nimekasirika kidogo!!!
 
Kesho Chadema wanaanza Mikutano yao Kusini mwa Tanzania kwenye Ngome ya CUF na ACT Wazalendo.

Chadema wanaingia kwenye Mikutano wakiwa na Hati Safi kutoka kwa CAG tofauti na wenye Ngome yao ACT wazalendo waliotuhumiwa kukwepa Withholding tax TRA.

Kwa ile Chadema ya Dr Slaa tungepata mjadala mzuri kuhusu hawa mafisadi wa November lakini Chadema ya Mnyika vitambi vingi maslahi mbele.

Niko hapa Nanjilinji na kesho nitakuwepo Masoko kuwasikiliza ndugu zangu wa Ufipa St.

Siasa ni Sayansi, Siasa siyo Uadui!
Kama upo Nanjilinji usitoke bila kuonja samaki Nchanga.Na pia ni vyema ukajiunga na wanachadema ujikomboe na mafisadi yanayokuzonga na kukupa hofu kila mara.Jivue gamba uwe huru,Kuwa mzalendo penda taifa lako,😂
 
Anakwenda Mwanambaya kuangalia mashamba yake, huko Nanjilinji anazuga tu. Leo kaa pale Njia nne utaona anapita.
 
Kesho Chadema wanaanza Mikutano yao Kusini mwa Tanzania kwenye Ngome ya CUF na ACT Wazalendo.

Chadema wanaingia kwenye Mikutano wakiwa na Hati Safi kutoka kwa CAG tofauti na wenye Ngome yao ACT wazalendo waliotuhumiwa kukwepa Withholding tax TRA.

Kwa ile Chadema ya Dr Slaa tungepata mjadala mzuri kuhusu hawa mafisadi wa November lakini Chadema ya Mnyika vitambi vingi maslahi mbele.

Niko hapa Nanjilinji na kesho nitakuwepo Masoko kuwasikiliza ndugu zangu wa Ufipa St.

Siasa ni Sayansi, Siasa siyo Uadui!
Mkuu hebu kaa kwa utulivu uhuishe kichwa cha habari na ulichoandika kwenye post
 
Tunakwenda kuitisha maandamano Nchi mzima kulishinikiza Bunge la CCM ili waliokula tozo wasipate muda wa kukimbilia South Afrika na kwengineko.
 
Bado unayapambania mafisadi wanaotufilisi😂
Magonjwa Mtambuka na wenzake tatizo lao siyo CCM na mfumo wake mbovu, bali wao kutokuwa kwenye mfereji wa kupokea kinachoibwa serikalini. Kundi lao lote siyo Kundi la Mama na ndiyo maana wanapambana naye. Akiingia mtu wao, wazimu wao wa kuitetea CCM hata inapofanya madudu, unawarudia tena kwa kasi ya ajabu hadi utashangaa!!
 
Na huo ndio unaa wao,na hiyo ndio sababu ya umaskini wetu na umaskini wa waafrika 🤔. Uzalendo 0.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom