CURIOSITY_200
JF-Expert Member
- Sep 25, 2016
- 320
- 260
Umeandika nonsenseJibu ni kwamba Mwafrika ni mtoto wa Mzungu, maana yake ni kwamba Mzungu katulea, katufundisha kusema aeiou, katufundisha kusoma, kuandika kwa kifupi Mwafrika hawezi kufikiri nje ya kile Mzungu alichomwambia, na kila kitu ambacho tunakijua ni kile Mzungu alichotuambia, na haya ndiyo madhara ya kutawaliwa na ndiyo maana nchi ambazo hazikutawaliwa na Mzungu ziko mbali kimaendeleo kama Korea (zote mbili), Ujapani, Uchina, Taiwan!
Maadamu hatufanya reforms wakati tunapata Uhuru ktk kwa Mzungu basi hakuna kitu kitabadilika kwa maana hata tunachojifunza ni Mitaala ya Elimu yetu ni ya Mzungu, Mwanafunzi wa Kitanzania/Afrika anajua zaidi kuhusu Ulaya na USA klk anavyojua kuhusu Afrika!
Mwafrika ndiyo Binadamu pekee Dunia hii ambaye anatumia muda wake wote Shuleni kujifunza Lugha tu, hakuna mtu anayejifunza lugha kwa muda mrefu ukiondoa native speakers kama Mwafrika, kwa kifupi tunakwenda Shuleni kujifunza Lugha tu, Kiingereza/Kireno/Kifaransa au hata kihispani kutegemeana na Mkoloni wako, hivyo hakuna muda unaobaki kuwa wabunifu kwani tukishajua hizi lugha ndiyo kila kitu kimeisha!