Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,735
- 40,858
Chakula cha Mawazo: Unafikiri ni kwa kiasi gani ubunifu (creativity) una nafasi katika kubadilisha maisha mtu, kikundi cha watu, jamii au hata taifa kwa ujumla. Unafikiri Watanzania kama mtu mmoja mmoja na kwa ujumla wao ni wabunifu katika kushughulikia matatizo na changamoto mbalimbali zinazokabili maisha yao?
Kwamba, kama kitu hakikufundishwa darasani, au hatujaona watu wengine (hasa wa nchi zilizoendelea) hawajakifanya basi sisi hatuna namna ya kukifanya au hata kukifanya vizuri zaidi? Kwamba, bado tunashughulikia matatizo mengi kwa mbinu zile zile za miaka zaidi ya hamsini nyuma?
Ni kwanini inaonekana hata tunapojaribu kubuni masuluhisho ya mambo fulani bado tunafikiri kwa namna ya wastani mno?