Yawahusu wanawake wa jf tu

Yawahusu wanawake wa jf tu

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,589
Habari marafiki zangu

Natumai mko fiti na mnaendelea na shughuli,kazi na masomo yenu vyema
Leo nimeonelea nizungumze nanyi akina dada/wanawake wa humu mjengoni
kuhusu masuala yetu wanawake.

Moyoni mwangu niliwaza na kufikiri kuwa tuanzishe kitu ambacho kitatupa
umoja/ushirikiano/uhusiano wa karibu yetu na vilevile hata kutembeleana
kama itawezekana kwa wale walioko mkoa kwa mkoa,
na kupeana mambo ya baraka au huzuni pia kwani ziko ndani ya maisha
yetu ya kila siku. Kitu ambacho ningependa kuwashirikisha hususani
wanawake wenzangu, tuwe na jukwaa la akina mama au wanawake wa
jf. Mnaonaje tumshauri huyu Founder wetu atuwekee jukwaa hilo lihusulo
wanawake kama atapenda, jamani marafiki hili ni wazo langu tu ambalo
nimependa kuwashirikisha.

Hilo jukwaa tutakuwa tunazungumzia mambo mbalimbali yanayotuzunguka
yanayotupata, na vilevile tutajadili ni jinsi gani twaweza kuwasaidia wanawake
wa kitanzania katika matatizo/ misukosuko inayowakumba wanawake wenzetu
na vilevile tutajadili namna ya kumkomboa mwanamke aliyekandamizwa na
unyanyasaji toka upande wa pili. (Mfumo dume), kumpatia fursa ya kujikwamua
na kujinasua toka katika makucha hayo hususani wanawake waishio vijijini hasa.

Kitu kingine tutajadili na kupeana taratibu mbalimbali katika mambo yatuzungukayo
kama wanawake, hasa mambo mbalimbali kama ukiwa na shughuli yako unaweza
kutualika nasi tukajumuika nawe kufurahia hiyo shughuli yenyewe. mfano: ngoma,
kitcheni party, sendoff, tafrija fupi, mambo yahusuyo watoto wetu n.k. Hapo ndipo
tunafahamiana na kuleta ushirikiano na mahusiano mazuri katika yetu. Hili ni wazo
tu sijui kama wanawake wa humu mjengoni jf mtalifurahia na kulipenda na kulifanyia
kazi kama mko tayari basi msisite kufanya maamuzi na kutoa michango, ushauri na
jinsi gani twaweza kufanya haya yote kusaidiana na kuendelezana katika kuleta
maendeleo kwa mwanamke. Kama mtakuwa tayari tutawandaa viongozi wa kuongoza
kitu hichi na kuleta motisha katika majukwaa mengine. Ushauri tafadhali.

Kama mwanamke/ mdada wa jf utapenda kushirikiana nami katika hoja/wazo hili
basi usisite kuandika ushauri, kutoa maoni yako tufanyeje ili kuanzisha kitu hiki nami
nitamwomba Founder wetu, afuatilie na kulifanyia kazi kama atapenda naye.
Maoni/Ushauri wako mdada utafanya tuwe na jukwaa hili hapa jf. Naomba tuepuke
mizaha na maneno yasiyopendeza kwani hii wazo tu binafsi ambalo nimependa
kuwashirikisha nanyi kama mnapenda toeni maoni yenu hapa.
TUFANYEJE KWA
JAMBO HILI
(hata wewe mwanaume wa jf unaweza kutushauri ukipenda)

Copy: charminglady, sweetlady, Mamndenyi, snowhite, Paloma, Passion Lady, Zion Daughter
gfsonwin, Sean, Madame B, madame X, Preta, CUTE, na wanawake wengine waliopo
hapa jf mmu wote kwa ujumla wengine sijawashika majina yao mtanisamehe bure wapendwa.
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri ila binafsi sina hulka ya kujimix napenda kukeep my private life private na nina a very small circle of friends, ila ni jambo jema na waencourage kina dada/mama wajf waonyeshe mwitikio chanya
 
mhm...hapa wanaume tuna kazi...wanawake wanataka kujipanga wajikomboe toka huu mfumo dume....ngoja tuwagegede mara ya mwisho maana karibuni tutambia kugegeda hakuna
 
hizi id humu unaweza kuta mzabzab ni boooonge moja ya mrembo (niwie radhi ni metumia jinalo kama mfano tu mwayego)
 
Last edited by a moderator:
nashukuru kwa mchango na maoni yako be blessed
Wazo zuri ila binafsi sina hulka ya kujimix napenda kukeep my private life private na nina a very small circle of friends, ila ni jambo jema na waencourage kina dada/mama wajf waonyeshe mwitikio chanya
 
ni kweli usemayo ndo mana nimewataja wale ninaowafahamu kwani waweza kuweka ID ukajua ni mdada kumbe ni mkaka, id zingine ukaujua ni mkaka kumbe ni mdada hapo sasa yanakkukuta usiyoyatarajia
hizi id humu unaweza kuta mzabzab ni boooonge moja ya mrembo (niwie radhi ni metumia jinalo kama mfano tu mwayego)
 
Hahahahah wanawake mna mambo nyie....zote hizo ni harakati za kumpinga mwanaume na tangu juzi mmeanzisha kampeni ya chini kwa chini hapa nimeishashtuka, asubuhi mwenzenu mwingine kaanzisha thread ya malalamiko kimtindo kuwa JF HAKUNA WAOAJI....sasa kama mna agenda ya siri semeni tu......hahahahaaaaa gud idea keep it up, labda mnaogopa kuoelwa mitaala na JF Men ngoja Little Angel akuje kwa huku
 
Last edited by a moderator:
usijali na potezea toa maoni yako best

haya bwana...mie maoni yangu ni kwamba its a good idea...especially women mlivyokuwa na power sana. ila tatizo yenu ni chuki binafsi na pia this is cyberspace...people may not be who they say they are (me included lol) so chances ya that happening are the same as the chances ya mzabzab kutogegeda.
 
nadhani hujanielewa vizuri best labda ufuatilie hiyo mada vizuri acha nikupaste japo hapa utaelewa "Moyoni mwangu niliwaza na kufikiri kuwa tuanzishe kitu ambacho kitatupa umoja/ushirikiano/uhusiano wa karibu yetu na vilevile hata kutembeleana kama itawezekana kwa wale walioko mkoa kwa mkoa." nadhani hapa utaelewa yaani wale walioko mkoa mmoja wanatembeleana na kupeana yale ambayo tumeyaamua katika jukwaa letu litakaloanzishwa na founder wetu hapa, kisha mambo ambayo tumeambiana na kupeana majukumu tutayafanya huko huko tuliko katika mikoa yetu na wale viongozi tutakaowachagua wao itabidi wafanye ulazima wa kujua kila kikundi cha mkoa kuna nani ambaye ataleta maelezo ya kikundi hicho toka mkoani kwake atokako sasa hapa naona umeshanielewa, lete ushauri na maoni yako best
Sina uhakika kama tunaweza kukutana.Ni ngumu sana from past experience.
 
wazo zuri mm nimelipenda, lakini je tutakuwa na makundi, mf:- wanawake wa JF Dar, wanawake wa JF moshi halafu kunakuwa na mkutano mkuu wa mwaka ndipo tunakutana wote, au Inakuwaje?
 
nadhani hujanielewa vizuri best labda ufuatilie hiyo mada vizuri acha nikupaste japo hapa utaelewa "Moyoni mwangu niliwaza na kufikiri kuwa tuanzishe kitu ambacho kitatupa umoja/ushirikiano/uhusiano wa karibu yetu na vilevile hata kutembeleana kama itawezekana kwa wale walioko mkoa kwa mkoa." nadhani hapa utaelewa yaani wale walioko mkoa mmoja wanatembeleana na kupeana yale ambayo tumeyaamua katika jukwaa letu litakaloanzishwa na founder wetu hapa, kisha mambo ambayo tumeambiana na kupeana majukumu tutayafanya huko huko tuliko katika mikoa yetu na wale viongozi tutakaowachagua wao itabidi wafanye ulazima wa kujua kila kikundi cha mkoa kuna nani ambaye ataleta maelezo ya kikundi hicho toka mkoani kwake atokako sasa hapa naona umeshanielewa, lete ushauri na maoni yako best
Nimekuelewa sana bibie lakini naona hutaki kuukubali ukweli ninaosema. I doubt very much about this..Hapa tunafekisha sana our real identities.Tukikutana nadhani tutachukua muda sana ku cope na tabia za kila mmoja.Nishajaribu hii kitu ya wanawake kwenye jumuia nyingine tena kwa kusukumwa kwa winchi ilimradi tuende lakn wapi? Inahitaji UPAKO hii kitu.Na kwa Dar hii ndo sina uhakika kabisa kwani excuses ni nyingi hasa za kuhusiana na muda.Ni wazo zuri lakn umetoa kwani UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.Lakini tufanyie kazi kwanza mapungufu yetu kama wanawake tusijifanye blind hatuoni tuna matatizo gani.May be ingeanzia kwanza jukwaani kwa mada mbalimbali watu wakishazoea ndio iende kwenye real life.Alichoandika mzabzab ni tatizo lingine tulilonalo sisi wanawake.
hamna unity...division is ur aim kila leo
 
Last edited by a moderator:
MM nadhani hujanielewa best hatujitengi sie wala hatutafuti mambo yetu bali ni kuleta haki kwa mwanamke aliyekandamizwa na kunyanyasika na mfumo dume tokea mababu zetu hata sasa wewe unaona kule mara jinsi wanawake wanavyonyanyaswa na kupigwa hovyo kama kinu, wengine wametoka viungo vyao tokana na unyanyaso wanaoupata huo ni mfano tu mdogo ndugu yangu tukianza kukusimulia madudu yanayofanywa na wanaume kwa wanawake waishio vijijini utakimbia nchi yako wewe, hebu lete maoni na sio kutukashifu na kutusema ndo mana tunataka kuondoa huu mfumo dume tawaliwa hapa Tanzania
Eee jitengeni tu,
Tena msiishie hapo,
Mkipata jukwaa lenu,
Ombeni na Jf yenu,
Mkipata na hiyo,
Ombeni na nchi yenu,
Si haki sawa?
Si wanawake kwanza?
Si ndio maendeleo?
Vigelegele na makofi
LAKINI Wanaume wana nafasi yao.
 
Back
Top Bottom