yanga

yanga


Mkuu,
Official website ya Dar Young africans OUR PLAYERS ina makosa mengi mfano mchezaji Nurdin Bakari kimo 6''7 ni mrefu kama Peter Crouch wa Stoke City Peter Crouch - Wikipedia, the free encyclopedia au Petr Cech wa Chelsea Petr

Pia inakuwa vipi kimo cha wastani cha wachezaji Dar Young Africans wastani wa kimo ni 5''6 inabidi kuwa na mchanganyiko wa wachezaji warefu zaidi ili kufanikiwa kuwa timu bora kikanda na kwa bara la afrika.

Wasifu wa mchezaji wa Yanga:
Nurdin Bakari OUR PLAYERS

[TD="width: 198, bgcolor: #ffefae"][/TD]

[TD="bgcolor: #b0ffb0"] NATIONALITY [/TD]
[TD="bgcolor: #b0ffb0"]TANZANIA
[/TD]

[TD="bgcolor: #ffefae"] DATE OF BIRTH [/TD]
[TD="bgcolor: #ffefae"]06 JULY 1988
[/TD]

[TD="bgcolor: #b0ffb0"] HEIGHT [/TD]
[TD="bgcolor: #b0ffb0"] 6'7 INCHES
[/TD]

[TD="bgcolor: #ffefae"] WEIGHT [/TD]
[TD="bgcolor: #ffefae"]67 KGs
[/TD]

[TD="bgcolor: #b0ffb0"] POSITION [/TD]
[TD="bgcolor: #b0ffb0"]MIDFIELDER[/TD]

[TD="bgcolor: #ffefae"] JERSEY [/TD]
[TD="bgcolor: #ffefae"] 22
[/TD]
 
Hongereni, mnahitaji goli moja tu mechi ya marudiano nyumbani
 
EWED 845 TIMES
dnzlsp.jpg
Kikosi cha Young Africans kilichoanza dhidi ya Denizlispor fc katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo katika viwanja vya Selen Football - Kalemya Complex

Young Africans imepoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Denizlispor FC ya Uturuki kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika viwanja vya Selen football - Kamelya Complex pemebni kidogo ya mji wa Antalya.
Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema zaidi lakini umaliziaji wa washambuliaji Saimon Msuva na Jerson Tegete katika dakika za 7, 15 na 24 uliikosesha mabao ya mapema.
Young Africans ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 35, mfungaji akiwa ni Jerson Tegete akimalizia pasi safi iliyopigwa na Saimon Msuva kufuatia migongeo mizuri ya Haruna Niyonzima na Athuman Idd 'Chuji'
Young Africans ileindelea kutawala mchezo kwa kipindi chote cha kwanza na hadi timu zinakwenda mapumziko Young Africans ilikuwa mbele kwa bao 1-0
Kipindi cha pili Denizlispor FC ilifanya mabadiliko ya kikosi chake kuanzai mlinda mlango mpaka washambuliaji wake, lakini mabadiliko hayo bado hayakuweza kuisadia kwani umakii wa walinzi Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro, Kelvin Yondani na Juma Abdul ulikuwa kikwazo kwao kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'
Dakika ya 78 Denizlispor FC ilijipatia bao lake la kwanza, baada ya mfungaji kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni ili hali walinzi wa Young Africans na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' wakisubiri kusikia filimbi ya mamuzi kwani mfungaji kabla ya kufunga alikuwa ameunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Huku mpira ukiwa katika dakika za mwisho kabla ya kumalizika, mwamuzi wa mchezo ambaye hakuonekana kuwa makini aliwapatia wenyeji Denizlispor FC penati dakika ya 88, penati ambayo ilileta utata kutokana na mwamuzi kupishana na mshika kibendera aliyekuwa ameonyesha kuwa mshabuliaji wa Denizlispor alikuwa amemfanyia madhambi nahodha Nadir Haroub, Denizlispor FC walipiga penati hiyo na kujihesabia bao la pili na la ushindi.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1- 2 Denizlispor FC.
hnds.jpg
Wachezaji wa Young Africans wakisalimiana na wachezaji wa Denizlispor kabla ya kuanza kwa mchezo leo jioni

Kocha mkuu Ernest Brandts hajapendezewa na matokeo hayo na hasa akitupa lawama zake kwa mwamuzi amabaye alishindwa kulimudu pamabano hilo ambapo katika kipindi cha pili alitoa maamuzi ya utatanishi yaliyopelekea timu yake kupoteza mchezo huo.
Timu yangu imecheza vizuri, nadhani wote tulikuwa mashuhuda jinsi vijana walivyocheza soka safi la kuvutia lililowashangaza baadhi ya wapenzi wa soka waliokuwa wamefika kutazama mchezo huo, naamini timu yangu kwa sasa iko vizuri na wachezaji wanaonekena kuelewa vizuri mafundisho yangu alisema 'Brandts'
Young Africans kesho itaendelea na mazoezi asubuhi katika viwanja vya Hoteli ya Fame Residence football .
Young Africans: Ally Mustafa 'Barthez', Juma Abdul, Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani/Mbuyu Twite, Athumani Idd 'Chuji, Saimon Msuva/Oscar Joshua, Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu,Jerson Tegete/Hamis Kiiza, Haruna Niyonzim
 
... Young Africans ileindelea kutawala mchezo kwa kipindi chote cha kwanza na hadi timu zinakwenda mapumziko Young Africans ilikuwa mbele kwa bao 1-0

Kipindi cha pili Denizlispor FC ilifanya mabadiliko ya kikosi chake kuanzai mlinda mlango mpaka washambuliaji wake, lakini mabadiliko hayo bado hayakuweza kuisadia kwani umakii wa walinzi Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro, Kelvin Yondani na Juma Abdul ulikuwa kikwazo kwao kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'

...Denizlispor FC walipiga penati hiyo na kujihesabia bao la pili na la ushindi...
... Waturuki walikuwa nyuma goli 1-0
... Waturuki walifanya mabadiliko ambayo hayakuwasaidia
... Waturuki walisawazisha na kuongeza la pili na hadi mwisho walishinda 2-1

Sasa mwandishi wangu, kama hatimaye walikuja kushinda 2-1, iweje useme mabadiliko hayakuwasaidia? Uandishi wa wana-Yanga bwana!
 
timu yenyewe waliocheza nayo imeshuka daraja alafu imewafunga; sasa kweli hapo wana-Yanga mnaweza mkajisifia kwamba kiwango chenu kimeongezeka jamani!!! mechi ya kwanza zidi ya timu ya daraja la tatu kutoka ujerumani nayo iliwashinda sasa hapo mna nini jipya??????,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom