carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 409
- 1,050
Kocha mpya wa Yanga, Fadlu Davids, ameanza maisha yake ndani ya kikosi hicho kwa ushindi baada ya timu hiyo kuichapa KVZ mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Maisala, Unguja, leo Jumamosi Novemba 14, 2026, Yanga ililazimika kutoka nyuma kabla ya kugeuza matokeo na kupata ushindi huo, ikiongozwa na mshambuliaji Cheikh Toure na kiungo Stephanie Aziz KI.
KVZ ndiyo ilianza kupata bao la kuongoza dakika ya 32 kupitia mshambuliaji Mudrick Abdi ‘Gonda’.
Yanga ilipata nafasi ya kusawazisha dakika ya 43 baada ya mwamuzi kutoa penalti kufuatia mchezaji wa KVZ kushika mpira ndani ya eneo la hatari, lakini Toure alishindwa kuitumia baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa Hamad Ubwa ‘Baro’.
Hadi mapumziko, KVZ ilikuwa mbele kwa bao 1-0.Kipindi cha pili Yanga ilirejea ikiwa na kasi, huku Toure akisawazisha dakika ya 52 kwa shuti la mguu wa kushoto akimalizia pasi ya Aziz KI. Dakika mbili baadaye, Toure alifunga bao lake la pili akitumia pasi nyingine ya Aziz KI.
Yanga iliendelea kulishambulia lango la KVZ na kupata bao la tatu dakika ya 79 kupitia Edmund John, aliyemalizia pasi ya Aziz KI katika shambulizi lililoanzia kwenye mpira wa adhabu ndogo.