Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,563
- 7,321
View: https://www.youtube.com/live/5nhKldXzqtQ?si=VuEACJPdOlKVtZpt
Kwenye kikao chetu tuliuliza pia kuhusu ripoti ya kilichotokea Machi 8, na CEO wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo akakiri kuwa ripoti wanayo na kuna kiongozi mkubwa wa Serikali alipiga simu kuzuia geti la uwanja lisifunguliwe, lakini hawawezi kumtaja hadharani. Nashangaa hili hajalisema kwenye tuliyoyazungumza leo, tumshauri akiamua kusema aseme yote asibakishe” Ali Kamwe - Meneja Habari na Mawasiliano.
Tumetoa matakwa manne. Matatu yanahusu mchezo namba 184, tunaamini yakifanyiwa kazi hayo matatu kwanza, tutakuwa tayari kucheza mechi hiyo kwa tarehe nyingine itakayopangwa. Na takwa la nne ni la muda mrefu, kuanzia msimu ujao. CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo asiudanganye UMMA kwa kuchagua kuzungumzia takwa moja tu na kuacha yanayotakiwa kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo yeye mwenyewe kujiuzulu” Alli Kamwe - Meneja Habari na Mawasiliano.
“Takwa letu la kwanza na la pili linahusu ukiukwaji wa kanuni uliofanyika Machi 8. Tunataka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi pamoja na CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo wawajibike kwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia kanuni na kuutia doa mpira wetu. Ligi yetu ni kubwa sana Afrika na inataka watu makini wenye weledi kuiongoza” Ali Kamwe - Meneja Habari na Mawasiliano Yanga SC.
Takwa letu la tatu ni kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya maamuzi mabovu ya mara kwa mara ya waamuzi. Kamati ya waamuzi ipo chini ya TFF kwa Katibu Mkuu, unashangaa ni vipi mwamuzi mmoja anafanya makosa yakujirudia na bado anaendelea kupangwa kwenye mechi bila kuchukuliwa adhabu yoyote ile. Ali Kamwe - Meneja Habari na Mawasiliano Yanga SC.
Napenda kuwajuza waandishi wa Habari, yasipofanyiwa kazi matakwa yetu matatu kwa uharaka, Young Africans SC hatutakuwa tayari kucheza mchezo namba 184, mechi zote mbili za Ligi zilizobaki na hatutashiri Ligi Kuu Msimu ujao. Huu ndio msimamo wetu na hatutayumba kwa lolote lile”. Ali Kamwe - Meneja Habari na Mawasiliano Yanga SC.
“Taarifa hii iwafikie ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF na Wadhamini wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, kuwa HATUTACHEZA mchezo wa Fainali wa CRDB siku ya tarehe 28, mpaka tutakapolipwa hela yetu ya Ubingwa kwa msimu uliopita. Tumevumilia dharau hizi kutoka kwa Mamlaka za Soka kwa muda mrefu sana, sasa imefika mwisho. Hii ya Zanzibar pia HATUCHEZI. @alikamwe - Meneja Habari na Mawasiliano.
“Kama wanafikiri tunatania waendelee kupuuza, katika hili Klabu ya Yanga tuko serious zaidi ya wanavyodhani na tuko tayari kwa lolote litakalotokea. Na kama yuko mmoja wao anadhani kupunguza pointi ya Yanga ni rahisi, na ajaribu kufanya hivyo na asuburi aone NGUVU YA WANANCHI. Ali Kamwe Meneja Habari na Mawasiliano.