Yanga yapata dili nono Ulaya

cnjona

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
1,027
239
YANGA SC ipo katika mazungumzo na klabu tofauti za Asia na Ulaya ambazo zinataka kununua wachezaji wake watatu, beki Mtogo Vincent Bossou, kiungo Mbrazil Andrey Coutinho na mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma.
BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE inafahamu Yanga SC ipo kwenye mazungumzo na klabu mbili za Malaysia ambazo zinawataka Bossou na Coutinho.
Aidha, klabu moja nchini Denmark imeonyesha nia ya dhati ya kumnunua mshambuliaji Ngoma na mazungumzo yanaendelea na klabu yake.
Baada ya mazungumzo ya awali, Yanga SC wameziagiza klabu zote hizo ziandike barua rasmi za ofa za kuwataka wachezaji hao.
 
Baada ya Okwi kuonesha kiwango cha ajabu sana katika Super Liga.. Sasa timu toka Denmark zinaifatilia kwa makini ligi ya Bongo.
 
Hawauzwi popote hao, hiyo ndio Yanga muulize Tegete. Wataishia kucheza ligi ya vilabu vya Afrika na kutolewa raundi ya pili. Wakiwa wajanja sana wakatae kuongeza mkataba kama alivyofanya Ngassa, ingawa naye alichelewa sana kuchukua uamuzi mgumu
 
Okwi yuko benchi kule anaosha viatu vya timu ya vijana

Baada "Cristiano wa Uganda" kupona hamstring injury.. ambapo alikaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili.. amerejea tena dimbani akiwa timamu zaidi.

Mpaka sasa amacheza mechi 2 katika mechi 3 za mwisho za timu hiyo.. Mechi ya pili alicheza 28/10/2015.. na kuweka rekodi zifuatazo.. zilizowaacha wazungu midomo wazi..

1. Kufunga magoli mawili ya haraka zaidi tangu Superliga ianzishwe [Dk. 61 na Dk. 64]... fastest brace.
2. Mchezaji wa kwanza toka EAC kutupia kambani goli 2 katika mechi 1.

Mpaka sasa Okwi kacheza mechi 2 kafunga goli 2 [wastani mechi 1 goli 1].. kwa wastani huu ana sail on the same boat with aubemeyang, lewandowisk na mtalamu mwenzake CR7.

Mechi ijayo timu yake itakua uwanjani dhidi ya Aab siku ya leo.. Naimani atarudi tena katika 1st eleven.

Kwa fixture zaidi pitia hapa chini..
1446826000317.jpg
 
Hawauzwi popote hao, hiyo ndio Yanga muulize Tegete. Wataishia kucheza ligi ya vilabu vya Afrika na kutolewa raundi ya pili. Wakiwa wajanja sana wakatae kuongeza mkataba kama alivyofanya Ngassa, ingawa naye alichelewa sana kuchukua uamuzi mgumu

Na hivi Manji kaukwaa umbagala wasahau!
 
Coutinho wamemuona wapi kiwango chake wakati muda mrefu tu yuko bench
 
Back
Top Bottom