Yanga yaachwa na ndege Algeria

geometry

JF-Expert Member
Oct 30, 2014
466
356
Yanga imepata pigo lingine nchini Algeria baada ya wachezaji wake kuchelewa ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene, jijini Algers.
Wachezaji hao walikuwa wasafiri na ndege ya Uturuki kupitia Istanbul wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa walichelewa kufika uwanjani hapo.
Wakati benchi la ufundi na wachezaji wachecha wakiondoka leo, wachezaji waliochwa na ndege wanategemea kuondoka Algeria kesho au keshokutwa. Yanga imeondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa mabao 4-0 na MC Algers katika mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Algeria

Hawa waandishi uchwara taabu sana, hiyo nayo umeona Habari ya kutuletea hapa, hiyo ni Timu ya mpira lete Habari za uchambuzi kuhusu mechi yao iliyopita, nini kimechangia mafanikio au mapungufu gani yalisababisha, lakini pia linganisha na wenzao kwa nini wamepata mafanikio dhidi ya yanga, na je nini kifanyike ili Timu zetu zifanikiwe zaidi, upuuzi wa kuachwa na ndege unafaida gani kwa hiyo Timu ya mpira? ? Acheni uandishi wa umbea umbea na MATUKIO, hovyo kabisa !!
 
Wanafikiri waarabu wakishakutia vinne wanakurudisha home utarudi mwenyewe uchelewe uwahi hilo hawajui ila cha msingi awe kakutatua tayari.
 
Hawa waandishi uchwara taabu sana, hiyo nayo umeona Habari ya kutuletea hapa, hiyo ni Timu ya mpira lete Habari za uchambuzi kuhusu mechi yao iliyopita, nini kimechangia mafanikio au mapungufu gani yalisababisha, lakini pia linganisha na wenzao kwa nini wamepata mafanikio dhidi ya yanga, na je nini kifanyike ili Timu zetu zifanikiwe zaidi, upuuzi wa kuachwa na ndege unafaida gani kwa hiyo Timu ya mpira? ? Acheni uandishi wa umbea umbea na MATUKIO, hovyo kabisa !!
Kuchelewa ndege sio habari ?
Jamii inataka kujua mbona leo hawajawasili Nchini wataambiwa wamechelewa ndege, hiyo ni habari na tena ina sifa zote za kuwa habari
 
Hakuna lolote, ingekuwa yanga ni kampuni ya ndege hiyo Ingekuwa Habari muhimu, amkeni basi nyie watu
 
Haina umuhimu wowote kwa wasomaji, nikupoteza rasilimali tu
Kuna rasilimali yako imetumika katika hiyo habari?.

Acha hasira za kijinga Timu ipo Algeria ilienda kwa taarifa na kurudi inarudi kwa taarifa ila kulingana na taarifa iliyotoka kuwa wangekuja leo haikuwa kweli tunataka kujua kisa nini tunajuzwa kuwa wamechelewa ndege.

Unataka taarifa iwe inahusu siasa au kupotea kwa watu?

Hakuna rasilimali iliyotumika hapo katika hiyo habari na hili ni jukwaani la michezo linahusu habari zote za michezo sio lazima kila mmoja aandike kwa jinsi itakavyokupendeza acha watu waandike habari ili mradi ziwe za kweli na wewe ukiona unataka kuweka mjadala hapa weka tutadadavua hiyo ndiyo maana sahihi ya mawazo huru kwa kila mtu.

Kama umeumia kwa hii habari basi utakuwa una matatizo.
 
Umeshasema hili ni jukwaa huru, uhuru huo ndiyo ulioleta hoja yangu kuwa Habari haina mashiko, usinilazimishe kuamini kuwa hii ni Habari muhimu kwangu, kaa na mawazo yako sihitaji ku kubadili na usinibadili msimamo pia.

Pili, mimi si muumini wa Siasa na sihitaji maelezo yoyote pia juu ya eneo hilo.

Tatu, kuanzia leo tambua kuwa hata muda wa kusoma na kujibu upuuzi ni rasilimali inayopotea.

Jipange.
 
Jipange !! Hayo maneno nayasikia kwa wanawake mara nyingi.
 
Hawa waandishi uchwara taabu sana, hiyo nayo umeona Habari ya kutuletea hapa, hiyo ni Timu ya mpira lete Habari za uchambuzi kuhusu mechi yao iliyopita, nini kimechangia mafanikio au mapungufu gani yalisababisha, lakini pia linganisha na wenzao kwa nini wamepata mafanikio dhidi ya yanga, na je nini kifanyike ili Timu zetu zifanikiwe zaidi, upuuzi wa kuachwa na ndege unafaida gani kwa hiyo Timu ya mpira? ? Acheni uandishi wa umbea umbea na MATUKIO, hovyo kabisa !!

Uchambuzi umeshafanyika labda umebaki uchakondoo tu. Uchambuzi ni kuwa Yanga kapigwa 4 mtungi. Uchakondoo ni kuwa mbona povu linakutoka
 
Hakuna povu binti, taifa kubwa hapa
 
Back
Top Bottom