Yanga Wavunja Mkataba Mwingine

Yanga Wavunja Mkataba Mwingine

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
YANGA SC imevunja Mkataba wa kupitishia malipo ya ada za wanachama wake Benki ya Posta na kuingia Mkataba mpya wa aina hiyo na beki ya CRDB.

Viongozi wa Yanga SC na CRDB wanakutana na Waandshi wa Habari muda huu kutangaza ndoa yao hiyo mpya baada ya klabu hiyo kuachana na benki ya Posta waliyoingia nayo Mkataba Juni mwaka huu.

Sababu za Yanga kufikia uamuzi huo, ni baada ya kuona benki ya Posta imeshindwa kuwafanya wafikie malengo yao waliyojiwekea na kwamba katika mkataba wao, kulikuwa kuna kipengele cha kuuvunja iwapo malengo hayatafikiwa. Benki ya Posta iliingia Mkataba wa aina hiyo na Simba SC pia.

TAARIFA ZAIDI ITAFUATIA.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga mkataba wa makabaliano yao kuhusu kuanzishwa kwa akaunti ya mashabiki na wanachama wa klabu hiyo katika hafla iliyofanyika Hyatt Regency jijini Dar es Salaam Juni mwaka huu.
Chanzo: SalehJembe

crdb.jpg
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dr Charles Kimei (kulia), akimkabidhi kadi mpya ya uanachama wa klabu ya Yanga SC mjumbe wa bodi ya Wadhamini Bi Fatma Karume (katikaki), kushoto ni makamu mwenyekiti wa Yanga Bw Clement Sanga

Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umewekeana sahihi ya makubaliano na Benki ya CRDB nchini juu ya uboreshaji na utengenezaji wa kadi za uanachama, hafla hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya Benki hiyo eneo la Posta mpya jijni Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dr Charles Kimei amesema anaushukuru uongozi wa Yanga kwa kuwaamini benki yao kuwa wanaweza kufanya kazi hiyo, na sisi tunaamini tutafanya kazi vizuri na kuweza kufikia malengo yao waliyotuwekea katika kipindi muafaka.

Kwetu sie kupata nafasi ya kufanya kazi na klabu ya Yanga ni jambo jema, tunatambua wana wana wapenzi zaidi ya milioni 20 nchi nzima, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunawifikia kila sehemu walipo na wanajiunga na uanachama wa kalbu yao pendwa alisema "Dr Kimei".

Aidha Kimei amesema kwa utaratibu huo wa mfumo wa kisasa, wataanza kwa kutoa bure kadi za uanchama wa Yanga ambazo zitakua na nembo ya VISA itakayomfanya mtumiaji aweze kuitumia sehem yoyote alipo na kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa ada za uanachama.

Gharama ya kadi itakua ni Tshs 8,000 tu kwa watakaoanza upya (bure kwa waliokua tayari wanachama) na mteja/mwanachama ataendelea kuichangia klabu yake ya Yanga kiasi cha Tsh 250/= tu kwa wiki ambapo kwa mwezi ni sawa Tsh 1,000/= na kufanya kwa mwaka ada kuwa ile ile Tshs 12,000/=.

Kwa upande wa mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu ya Young Africans Bi Fatma Karume amesema anaishukuru benki ya CRDB kwa kubali kufanya kazi hiyo, na kwa uwezo wao wa utendaji kazi anaamini wataifanya kazi hiyo kwa kiwango cha hali ya juu.

"Kikubwa nilichofurahi ni kuwa hawa CRDB Bank wapo mpaka kwetu Unguja, hivyo naona zoezi hilo litafanikiwa vizuri na kurahisisha upatikanaji wa kadi za wanachama kwa uharaka zaidi alisema " Bi Fatma.

Kadi mpya za uanachama wa Yanga zitakazotolewa na CRBD Bank zitakua za aina mbili, Premieum Visa Card kwa ajili ya viongozii mashuhuri wa klabu ya Young Africans tangu kuanzishwa kwake na nyingine ni Normal Visa Card kwa ajili ya wanachama wa kawaida.

Awali klabu ya Young Africans ilikuwa na mkataba wa aina hiyo na Benki ya Posta, Uongozi wa Yanga umeshawasilisha Notice kwa benki ya Posta juu ya kusitisha mkataba nao na sasa huduma hiyo itaanza kutolea kupitia benk ya CRDB.

Chanzo: Tovuti Rasmi ya Yanga
 
Waliokuwa washachukua kadi itakuwaje?? Ubabaishaji at work
 
Yanga wako bize kupamba CV yao
 
Mi ni mpenzi wa yanga ila nataka kadi ya simba.
 
hao CRDB nao wakae chonjo...............
 
timu lenu Simba lamatapeli na maamuma ndomana mikataba yenu fekifeki,wewe haujasoma vizuri term and condition baina ya Young Africans na Postal bank,ndomana unaongea kama unaimba ndolela
 
Sababu za Yanga Kuvunja Mkataba

Juni mwaka huu, Yanga SC iliingia Mkataba wa aina hiyo na benki ya Posta, lakini imeamua kuachana nayo kwa madai malengo hayajatimia.

Haingii akilini kabisa, nadhani kuna mtu hajapewa 10% yake
 
wacha kutokwa na povu wewe ngonjera
 
povu uanatokwa wewe ambae umekalia kigogo kwa kusema ya watu mbona huleti hapa mkataba wako wewe na postal bank kwa nyie hamkuiga haya???
wewe unabishana kishabiki zaidi si kihoja hata vijembe vyako vinaonekana vya kiswazi........nenda mwembe Yanga
 
Kimei nilikuwa namheshimu sana.. lakini hili nimemuona sio kabisa. Eti after 5 yrs yanga itakuwa kama Manchester.
swali; Manchester ina wanachama?
 
Sababu za Yanga Kuvunja Mkataba

Juni mwaka huu, Yanga SC iliingia Mkataba wa aina hiyo na benki ya Posta, lakini imeamua kuachana nayo kwa madai malengo hayajatimia.

Haingii akilini kabisa, nadhani kuna mtu hajapewa 10% yake

Mkuu,sometimes you need to think big,
CRDB ni among the best brand kwenye bank industry kwenye coverage,services,technology,profit huwezi linganisha na Poastal Bank.Wafanyabiashara na wafanyakazi wengi wanatumia CRDB over Poastal. Ukilist benk 5 zinazofanya vizuri huwezi kuta Poastal Bank ,Sio kila mahali mnaleta ushabiki
 
Hongera sana yanga na sasa azam on the way to go lazima vitu kama hivi na sie tukomae mbaya na imani kuwa azam nao watafanya pia..
 
Azam FC inawaalika waandishi wa habari za michezo Chamazi Complex leo.... Usafiri wa basi la Azam FC utakuwa TFF Karume saa tatu asubuhi kuwapeleka chamazi na baadaye kuwarudisha....Kuna habari kubwa ya kimapimduzi itakayotangazwachamazi leo.......... Stay tuned
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom