Yanga wampa uchifu Manji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga wampa uchifu Manji

Discussion in 'Sports' started by nngu007, May 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sunday, 15 May 2011 20:54

  Clara Alponce
  WAZEE wa klabu ya Yanga jana walimkabidhi Mkuki, Ngao na Kigoda kama alama ya cheo cha uchifu kwa aliyekuwa mfadhili wao Yussuf Manji.Manji alikabidhiwa heshima hiyo na kamati ya wazee ya muafaka wa Yanga chini ya kiongozi wake Mzee Yahaya Akilimali.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo mama Shadia Karume alisema Manji amejifunza mengi Yanga na amerejea rasmi kwa ajili ya kufanya kazi ya kuijenga Yanga mpya.Mama Karume alisema," Manji anatakiwa kujua hasira, jazba hazifai namtaka asahau yote yaliyopita."

  Mama Karume aliongeza kuwa kuna watu wengi waliofanya mambo makubwa na mazuri Yanga huko nyuma na Manji ni moja wao."Mume wangu ndiye aliyejenga jengo la Yanga hapa Dar es Salaam, lakini angejisikia vibaya kama lingeachwa na kuharibika bila ya kufanyiwa ukarabati kama aliousimamia Manji,"alisema Mama Karume ambaye pia alimtaka Manji kujenga jengo lingine la Yanga huko Zanzibar kwa sababu uwanja umeshapatikana.

  Tukio hilo lilishuhudiwa na viongozi wa serikali akiwemo Jamal Rwambo, Mbunge Mussa Zungu, Mudhihir Mudhihir pamoja na wachezaji wa Yanga huku burudani ikitolewa na bendi za Msondo, Sikinde na Tanzanite.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  this is when wazee waliozoea pilau na takrima wanapoona wamesahauliwa na siku zinapita meet the best opportunistic mofo who takes advantage of our ignorance and poverty!!!!
   
 3. O

  Ombeni Charles Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ok kila la heri Yanga. Tatizo la hao wazee Ombaomba sana hadi kero.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  dah.... ombeni unawakandya ombaomba :biggrin1:
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sasa huyo kijana atakuwa chifu wa Himaya ( chiefdom) ipi ? Haya mambo yawe yanawekwa kisayansi kidogo jamani. Au yanga nayo imeshakuwa chiefdom?
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  atapewa kabila la wazaramo maana ndio wenyeji hapa mjini
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sio wazaramo wote ni washabiki wa Yanga, wamo wa Azam, Simba Mtibwa etc na Si wanayanga wote wazaramo sasa inakuwaje hii. Kiunganishi cha klabu ya yanga ni wanachama sio klabu ilipo
   
 8. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  tulitegemea dunia inabadilika kwa kwenda mbele (upward trends) lakini cha kusikitisha baadhi yetu bado hatupendi kujitambua! Na kuna watu wanasema kuwa vijana wengi kwenye mpira klabu zetu za mpira wanapenda 'utumwa' hata zaidi ya wazee hawa kwa maana hiyo tutarajie machifu zaidi!
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kupenda kubaya mkuu.
   
 10. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  yanga imara.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa mkuu, ila wanaweza wakaangalia tu geographical location ya klabu basi.... au wa bahri kama alivyofanywa osam; to me, his chiefdom is ujustifiable kabisa

  Ni njaa tu ya hao wazee
   
 12. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Kuganga njaa tu, kama walivyosema wadau hapo juu. Makabila huwapa watu uchifu(hasa wa CCM) kwa kuwa Uchifu ndio mfumo wao, sasa ya Yanga na uchifu mhm.....
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  You have been rather soft, to put it better I would say "it is incosequential and of no effect". Void ab inito !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  umaskini mbaya sana!manji anafunika ufisadi wake kuphtia yanga!mengi anaonekana hana lolote yanga kwa sasa
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa mkuu

  yani wazee wamepangiwa pilau, ndizi, matunda na maji wanagawa heshima na kila kitu.......... klabu inaneemesha maponjoro

  haya mambo ya kusimikana haya matatizo makubwa
   
 16. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nijuavyo uchifu hukoma chifu akifa, na akifa mtoto wa chifu anarithi kiti cha baba. kwa hiyo sasa yanga chini ya chiefdom ya ukoo Manji!
   
Loading...