-Mjumbe wa Baraza la wazee wa klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amemshangaa Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa klabu ya Yanga, George Mkuchika kwa kukiuka katiba ya klabu ya Yanga kuhusu maagizo ya BMT kupitia shirikisho la soka Tanzania (TFF) la kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi 6 za uongozi ndani ya klabu ya Yanga.
-Mzee Akilimali amesema wajumbe wanne waliobaki walikubaliana na TFF kuhusu kufanya uchaguzi na wakasaini makubaliano ya kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi sita ndani ya klabu ya Yanga sasa amelishangaa Baraza la wadhamini kuingilia majukumu ya kamati tendaji ya klabu. Akilimali ameenda mbali zaidi na kusema kwa mujibu wa katiba ya Yanga kazi ya Baraza la wadhamini ni kulinda mali za klabu tu na si kupitisha maamuzi ya kikao au kuitisha mkutano wa klabu.
-Mzee Akilimali ameuliza why Bwana Yusuph Manji amekuwa wa kusemewa kila siku kama Manji anataka kurudi Yanga kwa nini asijitokeze hadharani atangaze yeye mwenyewe kuliko kuja kusemewa na watu na ameomba TAKUKURU kuichunguza barua iliyosomwa jana na Mkuchika inayodaiwa kuandikwa na Yusuph Manji. Akilimali amesema kuna watu wanatumiwa ndani ya klabu ya Yanga na hawafuati katiba ya Yanga. amesema yeye kamwe hatakubali katiba ya Yanga ivunjwe na watu wachache kwa maslahi yao wenyewe.