Mzee Akili Mali atangaza kugombea uenyekiti wa Yanga

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,476
4,447
Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali, ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji.


Mzee Akilimali aonesha nia nafasi ya Mwenyekiti Yanga

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu ya hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.

Hivi karibuni Manji alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo ili aweze kupumzika kutokana na matatizo mbalimbali aliyokumbana nayo siku chache zilizopotia.

Lakini pia maamuzi hayo ya Manji yalikuja ikiwa ni muda mfupi tu umepita tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka 10, lakini akakukumbana na changamoto kibao kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo na kuamua kusitisha mpango wake huo.

Akilimali alisema anaamini amefikia uamuzi huo ili aweze kuleta mabadiliko makubwa ya ndani ya klabu hiyo kuanzia pale Manji alipoishia.

Alisema licha ya kutokuwa bilionea kama ilivyokuwa kwa Manji lakini anaamini kwa kutumia utajiri wake wa hekima na busara alizonazo ataiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kwa hiyo amewataka wanachama kutulia.

“Manji keshaondoka Yanga akapumzike kutokana na matatizo yaliyompata hivi karibuni kwa hiyo siyo vizuri kuanza kuumiza vichwa kuwa mambo yatakuaje bila ya yeye.

“Yanga ni timu kubwa, jina lake na nembo yake tu chanzo kikubwa cha kuingizia mapato endapo atapatikana kiongozi mwenye uchungu na maendeleo ya Yanga na asiwe mpigaji.

“Kwa hiyo, katika uchaguzi ujao ambao utafanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manji, nitagombea nafasi hiyo kwani uwezo wa kuipa Yanga mafanikio ninao,” alisema Akilimali.

Saleh Jembe

2a07f6d307d537461853d9b0e540ad13.jpg
 
Hiyo sio Breaking news kwasababu tuko wengi tunaowania hiyo nafasi na mimi nina wanachama wengi wanaonikubali kuliko huyo mzee.
 
Mzee wa mjini huyo. Anataka wagombea wa maana waje wampe hela ili eti ajitoe
 
Huyo mzee
Elimu yake ya hapa na pale
Na pia niya kuunga unga kma mchuzi
Na pia amepitwa na wakati huyo
Alfu ameshapitiliza life expectancy ya bongo
Muda wowote anaweza akafa na kutuhangaisha wana yanga
 
PALE AKILI NDOGO INAPOONGOZA AKILI KUBWA,AKILI YA VIBUYU NA MADAWA INAPOTAKA KUONGOZA AKILI YA DARASANI
 
Huyo mzee
Elimu yake ya hapa na pale
Na pia niya kuunga unga kma mchuzi
Na pia amepitwa na wakati huyo
Alfu ameshapitiliza life expectancy ya bongo
Muda wowote anaweza akafa na kutuhangaisha wana yanga
Mkuu mbona mnageukana wenyewe kwa wenyewe
 
Uzee dawa. Ngoja apewe tuone Matopeni FC watafurahia namna gani ujio wa wenye Yanga yao!
 
Hana sifa. Cheti cha kidato cha nne hana.
Ingekua Ukuu wa Mkoa sawa JPM anaweza kumpa kama alivyompa Bashite.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali, ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji.

SalehJembe.

2a07f6d307d537461853d9b0e540ad13.jpg

Samahani naomba kuuliza anagombea Uenyekiti wa Uchawi ndani ya Klabu ya Yanga au Uenyekiti / Urais Yanga?
 
Back
Top Bottom