Yanga tusimuache yule beki ya El Merreikh

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Benchi la ufundi uongozi na scouts wetu wa Yanga hebu tujaribu fanya mawasiliano na yule mchezaji beki rasta wa timu hii ya Sudan el Mereikh, hakika atatufaa sana kuimarisha ukuta kule nyuma.

Ni matumaini yangu yule mtu kama akisimama na Lamine hakuna paka yeyote atakayekatisha, hebu tumwangalie tena leo vizuri hapo saa kumi kwenye dimba la mkapa wengi mtakubaliana nami kuwa yule mtu atatufaa sana wananchi.
 
Benchi la ufundi,uongozi na scouts wetu wa Yanga hebu tujaribu fanya mawasiliano na yule mchezaji beki rasta wa timu hii ya Sudan el Mereikh,hakika atatufaa sana kuimarisha ukuta kule nyuma
Unafikiri kila mchezaji anayetakiwa na Yanga na yeye pia anaitaka Yanga? Kuna klabu zinataka wachezaji, na kuna klabu zinatakiwa na wachezaji. El Mereikh ni matajiri kuliko Yanga, atoke Marekani aende Afghanistan?
 
Benchi la ufundi,uongozi na scouts wetu wa Yanga hebu tujaribu fanya mawasiliano na yule mchezaji beki rasta wa timu hii ya Sudan el Mereikh, hakika atatufaa sana kuimarisha ukuta kule nyuma.

Ni matumaini yangu yule mtu kama akisimama na Lamine hakuna paka yeyote atakayekatisha,hebu tumwangalie tena leo vizuri hapo saa kumi kwenye dimba la mkapa wengi mtakubaliana nami kua yule mtu atatufaa sana wananchi.
Mlipeni kwanza Tambwe na Sibomana
 
Unauliza jibu! sio pesa tu hua wachezaji wazuri wanaangalia malengo ya team husika mpaka sasa ukiulizwa malengo ya utopolo ni yapi ? Utakosa jibu team ipo ipo tu ,nyie suburin wachezaji kama kina sarpong na wengine wa level hiyo
Malengo ya Utopolo FC ni kuchukua bingwa, Ila wanaweza kujikuta nafasi ya tatu
 
Yani mnafeli kuanzia viongozi,wachezaji,mashabiki mpaka threads zenu mnafeli.
Tunafeli vipi?si ni nyie mnaokosa usingizi sababu ya yanga siku zote?nyie mnatengaga fungu maalum kwa ajili ya kumvurugia Yanga tu mambo yake
Mfano tu mchezaji Morrison
 
Kocha mliyenaye katoka El Merreik kaja kuifundisha Simba, ndio kusema Simba ina pesa zaidi ya El Merreik?
Ulichosahau ni kua kocha anaweza kufukuzwa lakini mchezaji muhimu hawezi kufukuzwa na pia mshahara wa kocha unaweza ukawa wa kawaida ila wachezaji ukawa mkubwa ....
Sasa unaposema kocha basi ujaribu kutumia akili ndogo tu...
Unawaza kama kenge
 
Tunafeli vipi?si ni nyie mnaokosa usingizi sababu ya yanga siku zote?nyie mnatengaga fungu maalum kwa ajili ya kumvurugia Yanga tu mambo yake
Mfano tu mchezaji Morrison
Mnaweza mkatenga nanyi pia, si mnajiona tuko level moja?
 
Hela mnayo ya kumtoa mchezaje club kubwa kama Merikh, tena akiwa kwenye ubora wake? Subirini akiishiwa kiwango kiasi cha kutostahili namba pale Merikh, kama ilivyokuwa kwa Mkoko na Vita Club ndo muende.
Hela ipo
 
Benchi la ufundi uongozi na scouts wetu wa Yanga hebu tujaribu fanya mawasiliano na yule mchezaji beki rasta wa timu hii ya Sudan el Mereikh, hakika atatufaa sana kuimarisha ukuta kule nyuma.

Ni matumaini yangu yule mtu kama akisimama na Lamine hakuna paka yeyote atakayekatisha, hebu tumwangalie tena leo vizuri hapo saa kumi kwenye dimba la mkapa wengi mtakubaliana nami kuwa yule mtu atatufaa sana wananchi.

Luís ama konde boy anahitaji mabeki wasiopungua 7 kumkaba sasa sijui una maanisha nini !
 
Tunafeli vipi?si ni nyie mnaokosa usingizi sababu ya yanga siku zote?nyie mnatengaga fungu maalum kwa ajili ya kumvurugia Yanga tu mambo yake
Mfano tu mchezaji Morrison
Simba ana time na Yanga ambao ndo kwanza wanaandaa pahala pa kulala wachezaji.
Simba ni Next Level.

Morison amkua na hela ya kumsajili wenye hela Simba chap wamemchukua,ndo maana kesi yenu ya CAS kuhusu BM imezimika kimyakimya.
 
Back
Top Bottom