Yanga SC msingewafunga Singida United Leo.. Dunia Ingesimama.

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Yanga SC na Singida United ni ngumu kuwatenganisha ...
Kwanini?

Shabiki lia lia wa Yanga SC, Mwigulu Nchemba.. Ndiyo mlezi wa Singida United ... Leo timu yake inafungwa, eti anashanglia ... Unategemea nini sasa hapo??

Huu udugu wao ulisababisha haya msimu huu ...
Singida United walimsajili Feisal Salum kutoka JKU ya Zanzibar. Baada ya Yanga SC kusua sua katika dirisha la usajili, Mwigulu Chemba aliamua kuwapatia Feisal Salumu bureee kabisa.

Hivi inawezekanaje Baba alie ukata alafu mtoto ule na kusaza ...
Ungana nami ...

1. Tangu msimu huu uanze, beki Mganda wa Singida United, Shafiq Batambuze, hajaripoti katika timu kwa kile kinachodaiwa kuwa ni suala la kutolipwa mshahara na kumaliziwa fedha za usajili.
2. Kuelekea mechi ya leo, makocha wasaidizi wa klabu ya Singida United Athuman Mfaume na Jumanne Chale wameachia ngazi kwa sababu ya kutokulipwa mshahara miaka kadhaa.
3. Golikipa wao tegemeo, Manyika Peter naye kajiengua katika timu kwa kutolipwa stahiki zake.

Kwa kifupi mechi ya leo kati ya Ndala na Singida ilikua ni ...
"Mbuzi wa bwana heri.. Kala shamba la bwana heri.. Kesi imeenda kwa bwana heri.."

Jambo la kufurahisha 30/09/2018 hizi mbereko hazitakuwepo kabisa ... Tukutane Taifa.
 
Pale Singida United inapomfurahisha bosi aliyefanya wema wa kutoa wachezaji.

Nilisema mapema leo, United itagawa alama kiurahisi tu. Amechukua nafasi ya Toto Afrika.
 
Lakini toka ligi ianze hajafungwa, sijui unasemaje kuhusu timu zilizomtangulia singida united kufungwa na yanga?
Ni kweli Mkuu.. Kushinda mlishinda tena kihalali.. Lakini cha moto mlikiona.

Ila leo.. HAPANA.
 
Pale Singida United inapomfurahisha bosi aliyefanya wema wa kutoa wachezaji.

Nilisema mapema leo, United itagawa alama kiurahisi tu. Amechukua nafasi ya Toto Afrika.
Hawa jamaa hiii dhambi itawatafuna daima... Na nawaona msimu ujao wakiwa ligi daraja la kwanza.
 
Yanga sio wa kuhangàika na mechi moja tu ya Simba...Sisi Yanga tunaxhotaka ni ubingwa
Hahaha.. Naona mshaanza kutafuta sababu mapema.

Baada ya msimu uliopita kutokuhangaika na mechi dhidi ya mfalme wa nyika.. Mlifikia wapi harakati zenu za ubingwa?
 
Ubingwa hakuna hapo. Labda Malinzi arudi TFF.. ili mechi ya away ya Ndanda FC zipigwe Taifa kama zama Zenu aisee!
kwa mfano ligi ikiisha leo..nani ni bingwa?.... hujui Yanga wanaongoza ligi?... Hujui Yanga hata wakifungwa na Simba bado wataongoza ligi
 
Hivi Kama si uhodari wa Kakolanya unafikiri Singida wasingesawazisha hayo Magoli?
Mkuu.. Kila kitu kilichokua kinafanyika uwanjani kilikua kimepangwa.

Natamani Mkurugenzi mpya wa TAKUKURU akianza na hawa.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom