Yanga SC msingewafunga Singida United Leo.. Dunia Ingesimama.

1) je kutokuripoti kwa Shafiq Batambuze tokea msimu uanze imei favour Yanga peke yake au timu zote zilizokutana na Singida kabla ya mechi na Yanga? au mechi ya Yanga vs Singida ndio ilikuwa mechi ya kwanza kwa singida?

2) kwahiyo mkuu tutegemee kuwaona makocha pamoja na kipa wakirejea kuitumikia Singida united baada mechi ya Yanga kumalizika? Au ndio timu zingine nazo zitacheza na Singida iliyokuwa na upungufu wa hao watu?

3)kutokana na kauli yako ya undugu wa Singida na Yanga je msimu uliyopita Yanga aliamua kutomfunga kwa makusudi Singida kwenye mechi zao zote walizokutana? Hivyo hata kwenye mechi ya shirikikisho Yanga aliamua kutolewa na Singida kutokana na undugu?
Kuhusu 1 na 2 nilikua naeleza ni jinsi gani timu ilivyo na ukata mkubwa kwa sasa.. Hivyo ikawa rahisi kwa Ndala siku ya jana kutembeza miamala.
Kuhusu 3, msimu uliopita timu ilikua chini ya kocha makini Hans, ambae pamoja na kugoma kuintataini 'upuuzi' aliokua akiletewa, pia alitaka kuiprove timu yake ya zamani kua bado yeye ni kocha bora.. Ndo mana alikua akikutana na Ndala anajipigia tu. Tofauti na hali ilivyo sasa.
 
Ila tusemage tu Na ukweli, kwa uchezaji wa yanga na simba...yanga ipo vizuri technical, na skills kuliko simba pakubwa,, ,,af yanga inacheza Kitimu zaidi kuliko simba... Ubora wa simba upo kwa mchezaji mmoja mmoja lkn suala la technical na skills simba hawako vizuri sana!!!!! Cha kufurahisha yang leo walikuwa na consistency mwanzo mwisho tofauti na game tatu zilizopita, wakicheza na simba bila kuchoka hasa kipindi cha pili ....simba lazima walie, uwezo wa Ibrahim ajib sijaona wa kumzuia pale simba kutawanya mipira kifundi vile...!!
Ajibu akija leo Simba anasugua benchi kama kawaida, ndio maana aliona bora akimbilie Yanga hakuna viwango kama chake.
 
Yaonyesha wewe kida katika soka. Simba amefika Nusu Fainali Klabu Bingwa Barani Afrika.

Amefika Fainali Kombe la Shirikisho, zamani (Caf)

Nitajie Yanga imefika wapi kwenye michuano hii mikubwa Afrika kama IQ yako inafanya kazi.

Karibu...!
Hiyo nusu fainali ya club bingwa simba ilicheza mwaka gani...??? Ilicheza na timu gani..??? Hizi ndoto za alasir mbaya sana.
 
Ni kweli Mkuu.. Sisi wengine tunapambana dk 90, kwa nguvu na akili nyingi na tunatoka na ushindi wa kihalali lakini kwenu ni mambo ya Rose Muhando. Ila si mbaya 30/09 tutakata ngebe zenu.
Baada ya Mbao FC kugomea msiingie kwenye change room zao naona mmekuwa wenye kuweweseka sana.

Tuliza mwanya ifike hiyo trh 30
 
Back
Top Bottom