Yanga: Rangi zetu zinatuponza jamani

Yanga: Rangi zetu zinatuponza jamani

Hata mimi siipendi Yanga kutokana na rangi za nguo zao!

Kuna mwenyekiti wa cdm kijiji cha utyego ni mpenzi wa yanga na alienda uwanjani kavaa jezi ya yanga alikimbizwa balaa na alibondwa na mawe akadandia gari bila kujijua.
 
Dada ham d hilo ndo umeona tu yako mbo mengi tuu unaleta yasiyo na maana!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu chama,

Hawa pro CHADEMA wamepapasa huko na huku na kutafuta wapi pa kutokea ili waichafue CCM ila imeshindikana; eti sasa wameamua kutokea kwenye rangi.

Hawa jamaa kweli viroba vitawaua.

mkuu HAMY-D
jamaa zetu wanapokea viposho pale Togo sasa wasipoandika riziki haingii; siku hizi hawana chakusema wanajionea wenyewe jinsi wananchi wanavyoipokea CCM; jukwaa wanalikimbia siku hizi kasi ya maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za CCM ni tishio; leo wamekuja na rangi kesho watatafuta ujinga mwingine wa kusema!
 
Sio Kweli Mimi Ni Shabiki Wa Simba Ila Siwachukii Yanga Kisa Jezi Zao Bali Naichukia Yanga Kwa Kubebwa Kwao Na Kutokujua Kucheza Habri Za Chadema Kuipiga Yanga Mawe Ni Ya Uzushi Kamwe Haiwezi Kupenya Kwenye Sikio La Watu Makini!!
 
Wakuu JF Wana Young Africans Amani iwe Nanyi.
Nipende kuonesha masikitiko Makubwa sana kwa kilichowapata Wachezaji wetu jana Mbeya Baada ya Gari lao kushambuliwa na Mawe na anaodhaniwa kuwa ni Mashabiki wa Mbeya City FC.
Gari limevunjwa vioo na Dereva kujerehiwa Vibaya sana.


Ombi.
Niwaombe wa Tanzania na Makamanda wote kujua kuwa ijapokuwa Rangi zetu binafsi zinanikera sana na kupelekea Matukio kama ya jana.
Nipende kuwajulisha kuwa zaid ya 80% ya Mashabiki wa Vijana wa Jangwani sio wafuasi wa Magamba.
Ni Hayo tu
Kweli aiseee........
 
Hivi wewe mleta mada kama huna la maana la ku-post si ufiche upumb.avu wako?

ama kweli,nyoka ni nyoka tu hata avue gamba,yanga huwezi kutoa hoja yako mpaka utukane?huku hakukufai rudi kulekule ulikotoka....
 
Ficha ujinga wako... Kwa mtazamo wako waliovamia basi ni cdm na sio mby city.. Kama ishu ni rangi why mashabiki wa mby cty?
Ficha Upungani wako
 
Funikeni upum*avu wenu. Mbona Brazil ilikuja hapa na haikupigwa mawe na rangi zao ni sawa na za Yanga. Michezo sio siasa!

Yule Jamaa aliyeenda uwanjani kumhug Kaka lazima atakuwa ni Gamba tu na alivutiwa na Rangi
 
We unaonekana Umetumwa Na magamba kuwaaminisha Watu kuwa yanga walipigwa na wanachama Wa CDM, Acha uchwara

Mkuu, Nasikia zile zilikuwa ni Fitna za Magamba ili ionekane kuwa Mashabiki wa Sugu na CHADEMA ndo walifanya Fujo
 
Mkuu chama,

Hawa pro CHADEMA wamepapasa huko na huku na kutafuta wapi pa kutokea ili waichafue CCM ila imeshindikana; eti sasa wameamua kutokea kwenye rangi.

Hawa jamaa kweli viroba vitawaua.

Mkuu afadhali sie Viroba, Nyie Sembe ndo ishawapoteza tayari
cc chama
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi siipendi Yanga kutokana na rangi za nguo zao!

Nachukia sana kuchanganya siasa na michezo. Siasa 'is struggle for power' wakati michezo ni burudani na raha. Wakoloni walitutawala tangu mwaka 1885 baada ya Berlin Conference tukianza na Mjerumani na ilipofika 1919 akaingia Mwingereza na kututawala hadi 1961. Kokotoa ni miaka mingapi ya mateso ya Mjerumani mwenye viboko na Mwingereza mwenye kupora rasilimali zetu. Mwingereza akatuachia na timu yake Sunderland a.k.a Simba SC ikiwa na jezi hizo hizo nyekundu na nyeupe, na hata ukiangalia huko Uingereza ni klabu ngapi hazitumii jezi nyeupe na nyekundu. Hao unaowaita Magamba wametutawala kwa miaka takribani 52 tu unawachukia kiasi hiki kwa nini usiwachukie hao wenye rangi nyekundu na nyeupe waliotutawala kwa zaidi ya miaka 76? Mimi siamini kama walioleta vurugu pale uwanjani ni Mbeya Site (Sijakosea, Mbeya siyo City bhana) bali ni maadui wa Yanga ambao tunawafahamu. Siku zinakuja tena zimekwisha kuwadia tutakapoanza kutoa vipigo vitakatifu kwa timu yao. TFF kaeni chonjo, mpira umegeuka kuwa vita sasa, chukueni hatua mapema.
 
Walichofanyiwa Yanga ni muendelezo tu wa ujinga ambao wao waliuanzisha wa kuikataa logo ya Vodacom (wadhamin wa Ligi kuu) eti kwasababu ina rangi nyekundu ambayo pia hutumiwa na Simba. So yaliwakuta Yanga ni muendelezo wa upuuzi ambao wao waliuanzisha, na kwasababu wao ndio waasisi wa dhambi hiyo ya ubaguzi ni halali dhambi hiyo iwatafune.
 
Walichofanyiwa Yanga ni muendelezo tu wa ujinga ambao wao waliuanzisha wa kuikataa logo ya Vodacom (wadhamin wa Ligi kuu) eti kwasababu ina rangi nyekundu ambayo pia hutumiwa na Simba. So yaliwakuta Yanga ni muendelezo wa upuuzi ambao wao waliuanzisha, na kwasababu wao ndio waasisi wa dhambi hiyo ya ubaguzi ni halali dhambi hiyo iwatafune.

Mbeya city wana alejI na kijani na njano
 
Back
Top Bottom