Yanga Queens mpaka sasa wamefungwa mbili bila

Simba 3-0 hadi Sasa, yaani hawa Yanga princess wanacheza Kama kikundi cha wahuni tu uwanjani Kama walivyo Kaka zao kina Sarpong.

Hawa wadada wa Simba wanacheza mpira mzuri saana, kiukweli soka la wanawake limebadilika sana kwa wanao tazama huu mchezo basi wanapata burudani ya kutosha kabisa.

Ball control ipo juu, wadada wapo imara hawaanguki ovyo Kama vile vituko tulivyo vizoea hapa ni tofauti kabisa, wanapiga pasi zinafika, wanakimbia na mipira vizuri sana.

Kubwa zaidi nimependa sana jinsi walivyo na nguvu za miguu wanapiga mashuti hawa wadada balaa, makombora wanayo piga huwezi amini Kama limetoka kwenye mguu wa mwanamke.

Hongera kwa kocha Mussa H Mgosi kazi yako nimeiona.
 
Kweli soka la wanawake limeimprove nilikuwa nashuhudia mechi ya fountain geti vs Simba huku dodoma mzungoko wa kwanza nilikuwa nainjoy sana....yaani wanacheza kama wanaume tu kwa kweli wadada mkiamua hakuna kinachoshindikana
 
na wasipojipanga vyema hawa Yanga kipindi cha pili wanaenda kupokea magoli ya kutosha.. huenda yakafika magoli 5+
Hawa ndio super women wetu sasa wanawake wenye kujiamini baba anapo toka kwenda kwenye majukumu makubwa ya nchi super women wapo hapa nyumbani wanahakikisha familia inakuwa na furaha kama hivi wanatuletea maziwa ya kutosha haya yaani raha tu.
 
Back
Top Bottom