Yanga noma,yaondoka na point moja ugenini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga noma,yaondoka na point moja ugenini

Discussion in 'Sports' started by Bwana Mapesa, Sep 15, 2012.

 1. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,901
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Katika hali ya kuonyesha wamejizatiti kuchukua ubingwa wa Ligi kuu bara bingwa wa A.MASHARIKI YANGA leo wameanza vizuri kwa kuchukua point moja dhidi ya timu ngumu(iliyopanda daraja msimu huu) ya Prison na kufanikiwa kuchukua point hiyo baada ya kufanikiwa kuwadhibiti visiki hao wa mbeya na kufanikiwa kutoka suluhu ya bila kufungana.YANGA ambayo imefanya usajili wa kufuru na kimafia..leo wamedhihirisha Ukuta wao(UKUTA WA BERLIN) Mgumu kwa kufanikiwa kuwazuia Prison kufunga.Watani wao wa jadi simba wao kwa sababu wamependelewa kuanzia nyumban takriban mechi sita wamefanikiwa kushinda goli 3 kwa 0 dhidi ya A.LYON simba.HONGERENI YANGA kupata point moja ugenini sio sawa na kupata point 3 nyumbani.
   
 2. M

  MPUNGA JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 802
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 80
  Mbuyu tuite kacheza? kweli pesa si msingi wa maendeleo!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mbuyu Twite na Kelvin hawakucheza ndiyo maana wametoa droo...hahahaha
   
 4. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mabingwa wa kagame hata kagame walianza kwa kichapo
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hshaaaaaa sasa hii inahusikaje na uislamu khaaa
   
 6. C

  Cape city Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna bijitu ina stress za droo, uislamu unahusikaje hapa?
   
 7. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,345
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  Ukuta wa berlin wapi? Goli lilifungwa sema refa kabeba

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 8. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kichapo kwenda mbele na hasa atakapokutana na mtani wake
   
 9. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwakweli unachekesha...
  mbona mlikuwa mnajigamba kwamba mnaenda Mbeya kufanya mauaji, au mauaji ndo haya kuambulia pointi moja?????
   
 10. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mbuyu tuite hakucheza, nasikia alikuwa saluni anajipodoa!
   
 11. Root

  Root JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,146
  Likes Received: 12,853
  Trophy Points: 280
  kwani hawakufanya usajili msimu huu?
   
 12. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,345
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  Timu imesajili mabeki tu unategemea nn? Tuliosajili wapasia nyavu matunda tunayaona

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 13. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wewe jamaa tafadhali usirudie kosa kwani wewe unautaja uislamu tumekukosa nini?Acha amani idumu .
   
 14. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Huyu kocha wa Yanga naona anafundisha mbinu za kujihami zaidi kuliko kushambulia. Ligi kuu inahitaji kushambulia na kujua kujihami zaidi kuliko kujihami tuu. Prison siyo timu ya kutoka draw na Yanga kirahisi namna hiyo. Bahamuzi, Tegete na Kazimbangu ni washambuliaji wazuri sana kama fomesheni ikiwa 4.4.2 na siyo 4.5.1. anyway, Hongera sana yanga kutoa draw lakini kitu muhimu ni kushambulia zaidi nako kuna manufaa sana . Maana huyo prison yeye angerudi nyuma kujihami na hivyo kuwapa mwanya wa kutawala .

  Brazil walipiga sana marufuku timu kujihami sana kuliko kujua kushambulia. Ndio maana unakuta Timu haichukui ubingwa mara mbili mfululizo. Bondia wako ukiona anashinda ulingoni lakini muda mwingi hurudi nyuma usifurahie ushindi wake ila mpe mbinu za kusonga mbele huku anrusha makonde.
   
 15. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Yanga , ukuta wa Berlin mpaka lini? tunataka ukuta wa berlin , ushambuliaji makomandoo wa Ki israeli.Ukinichezea, ukuta wa berlin, makomandoo wa ki Israel ,utachukua point popote pale penye luongewa Ligha ya kiswahili.
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Mnapoteza lengo la nyuzi!acheni udini bana msiwe kama JK!
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  SIMBA SC itaiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani na kwa sasa inakabiliwa na jukumu kubwa la kutengeneza timu yake hadi kufika Januari wawe wamekamilika.
  Pilika za kutosha na vurugu ndani yake zinafanyika kwa sasa Simba katika kile unachoweza kukiita kujenga timu- wachezaji wanasajiliwa kwa mamilioni baada ya wiki mbili wanafukuzwa, baada ya kucheza mechi moja au mbili.
  Lino Masombo, Patrick Kanu Mbivayanga, Mussa Mudde na Danny Mrwanda ni baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi, lakini wakatemwa hata kabla ya msimu kuanza.
  Usajili wa wachezaji wote hawa wanne unakadiriwa si chini ya Sh. Milioni 100, lakini fedha hizo ‘zimetupwa jalalani’ na sasa unaweza kuhisi hali fulani kutokea tena ndani ya Simba SC.
  Kelele zimekwishaanza juu ya wachezaji waliosajiliwa baada ya kutupiwa virago akina Mudde, Mbivayanga na Masombo, ambao ni Komabil Keita, Paschal Ochieng na Daniel Akuffo kwamba nao ni magalasa.
  Angalau Akuffo hazungumziwi sana kwa sababu katika mechi nne za kirafiki alizoichezea Simba amefunga mabao matatu, lakini mabeki Keita na Ochieng kwa sababu timu hiyo inaruhusu sana mabao kipindi hiki, wao wameingia kwenye ‘zengwe’.
  Nimesoma gazeti la Mwanaspoti jana, Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula anahoji Keita na Ochieng wamefuata nini Simba na kwa kuwa huyu kwa sasa ni Mwandishi wa habari za michezo na mchambuzi na kwa jinsi ambayo viongozi wa sasa wa Simba wanapenda kufanya kazi kupitia vyombo vya habari, nina shaka na mustakabali wa wachezaji hao katika klabu hiyo.
  Magazeti yanaandika Simba ilifungwa na Sofapaka ya Kenya mabao 3-0 Alhamisi katika mchezo wa kirafiki kwa sababu ya kupwaya kwa Keita na Ochieng wanaocheza pamoja katika beki ya kati.
  Tayari huo unachukuliwa kama mwendelezo wa makosa ya Simba katika usajili wa wachezaji wa kigeni, baada ya akina Lino Masombo, Mbiyavanga na Mudde.
  Mara nyingi nawaambia watu, kusajili wachezaji wazuri ni jambo moja na kuwa na timu nzuri ni jambo lingine- timu nzuri ni ile inayotayarishwa taratibu baada ya usajili.
  Mfano mmoja ni jinsi ile timu B ya Simba iliyochukua Kombe la BankABC mbele ya vikosi vya Ligi Kuu vya timu za Azam FC na Mtibwa Sugar- kwa sababu imekaa pamoja muda mrefu na wachezaji wamezoeana.
  Sasa leo Simba inasajili wachezaji wawili kutoka timu na nchi tofauti, inataka ndani ya wiki moja tu wacheze pamoja kwa maelewano, jamani hicho kitu hakiwezekani.
  Miezi miwili iliyopita wakati wa michuano ya Klabu Bingwa Afrka Mashariki na Kati, Kombe la Kagame watu walianza kumkosoa Felix Sunzu- bahati kwake hayupo kwa sasa, lakini kama angekuwepo na matokeo haya, zengwe lingeendelea na upande wake pia.
  Sijui hata hao wanaojiita wachambuzi huwa wanachambua nini- maana tatizo la Simba hivi sasa linaonekana wazi na litahitaji muda kidogo.
  Kifo cha Patrick Mutesa Mafisango ndio kinaitesa Simba kwa sasa- hajapatikana kiungo mbadala wake wa kuiongoza timu. Jamaa alikuwa ana mchango mkubwa sana kwenye timu enzi za uhai wake na kwa kiasi kikubwa ubingwa wa Ligi Kuu ulitokana na yeye.
  Tulikuwa tunaishuhudia Simba inacheza ovyo, inapoteana kabisa msimu uliopita ilipocheza bila Mafisango. Wakati Simba ikiwa inajiandaa na mchezo wa marudiano na ES Setif ya Algeria ilimsimaisha Mafisango kwa utovu wa nidhamu na ilipocheza mechi ya Ligi Kuu na African Lyon bila kiungo huyo, iligundua haiwezi kwenda bila mtaalamu huyo (R.I.P.).
  Ilicheza ovyo na kushinda ‘kizali zali’ 2-0 na baada ya hapo ikamrejesha kundini Mafisango akasafiri na timu Algeria. Huyu ndiye alikuwa mfungaji bora wa timu msimu uliopita kwa mabao yake 10.
  Alikuwa anajua kuichezesha timu- sasa hayupo na bahati mbaya zaidi klabu haijampata kiungo mpya mkabaji, hivyo safu ya ulinzi inakuwa na mzigo mkubwa.
  Katika soka, kitaalamu mabeki wakiwa wanamrudishia mipira mingi kipa basi kuna tatizo kwenye kiungo pale chini katika kuiunganisha timu na hilo ndilo linalojitokeza kwa sasa katika Simba.
  Simba inacheza vizuri ikiwa na mpira, kwa sababu ina viungo wengi wachezeshaji, lakini tatizo linakuja mpira unapohamia kwa wapinzani- wanapita kiulaini na safu ya ulinzi ya klabu hiyo inafikiwa mno, tena kwa urahisi.
  Mipira inapenyezwa mno kwenye eneo la hatari la Simba- sasa wazi hapa kabla ya kuanza kuwatazama mabeki, Simba waimulike safu yao ya kiungo.
  Pamoja na hilo, kubwa ni kwamba bado timu haijazoeana na hilo limetokana na ile wachezaji wanasajiliwa, wanafukuzwa- maana yake kila siku timu inaanza upya na sasa tushukuru pazia la usajili limefungwa hadi Januari, timu haitabomolewa tena.
  Amri Kiemba na Jonas Mkude ndio viungo pekee wakabaji katika Simba kwa sasa ambao siku za karibuni hawapangwi- mi nitabaki kuwa mwandishi na mchambuzi, lakini Profesa Milovan Cirkovick ni kocha na mtaalamu, hivyo anajua anachokifanya.
  IIa nachoweza kumshauri tu, babu huyo wa Kiserbia apunguze kujiamini kwa sababu, maamuzi mengi ya viongozi wa Simba hutokana na presha ya mashabiki au vyombo vya habari.
  Mwandishi mnazi kwa hasira zake, timu yake imefungwa anaweza kuandika kwa jazba bila kuzingatia vigezo wala utaalamu akaponda timu na wachezaji na kiongozi asiye mweledi kesho akafukuza mchezaji. Hiyo ndio soka ya bongo.
  Sasa kama hawa wanaowaponda Ochieng na Keita mapema yote hii, ni kwa sababu ya zile bao tatu za Sofapaka- ila kama Wakenya hao wangepoteza nafasi zote hizo na Simba wakatumia japo nafasi moja kati ya tatu walizopata, mabeki hao leo wasingekandiwa.
  Ufike wakati sasa Simba wakajifunza kuwa na subira. Wakajifunza kutokana na makosa, kwani msimu uliopita walimfukuza Derrick Walullya wakiamini ni galasa, ila alikuja na URA kwenye Kombe la Kagame Julai mwaka huu akacheza soka baab kubwa, udenda ukawatoka.
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kim pamoja sana..
   
 19. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  jamani yaaani twite hajasaidia?
   
 20. Kimbojo

  Kimbojo JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Michael Mwakyusa na Mkwakara, sitaki kuamini kwamba +255713...... zilikuwa zinawasha wakati manajiandaa kuchangia hii thread hii. swala la dini linakujaje kwenye suluhu ya yanga, Be greater thinker. ndio lengo la JF
   
Loading...