Yanga noma,yaondoka na point moja ugenini

SIMBA SC itaiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani na kwa sasa inakabiliwa na jukumu kubwa la kutengeneza timu yake hadi kufika Januari wawe wamekamilika.
Pilika za kutosha na vurugu ndani yake zinafanyika kwa sasa Simba katika kile unachoweza kukiita kujenga timu- wachezaji wanasajiliwa kwa mamilioni baada ya wiki mbili wanafukuzwa, baada ya kucheza mechi moja au mbili.
Lino Masombo, Patrick Kanu Mbivayanga, Mussa Mudde na Danny Mrwanda ni baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi, lakini wakatemwa hata kabla ya msimu kuanza.
Usajili wa wachezaji wote hawa wanne unakadiriwa si chini ya Sh. Milioni 100, lakini fedha hizo ‘zimetupwa jalalani' na sasa unaweza kuhisi hali fulani kutokea tena ndani ya Simba SC.
Kelele zimekwishaanza juu ya wachezaji waliosajiliwa baada ya kutupiwa virago akina Mudde, Mbivayanga na Masombo, ambao ni Komabil Keita, Paschal Ochieng na Daniel Akuffo kwamba nao ni magalasa.
Angalau Akuffo hazungumziwi sana kwa sababu katika mechi nne za kirafiki alizoichezea Simba amefunga mabao matatu, lakini mabeki Keita na Ochieng kwa sababu timu hiyo inaruhusu sana mabao kipindi hiki, wao wameingia kwenye ‘zengwe'.
Nimesoma gazeti la Mwanaspoti jana, Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula anahoji Keita na Ochieng wamefuata nini Simba na kwa kuwa huyu kwa sasa ni Mwandishi wa habari za michezo na mchambuzi na kwa jinsi ambayo viongozi wa sasa wa Simba wanapenda kufanya kazi kupitia vyombo vya habari, nina shaka na mustakabali wa wachezaji hao katika klabu hiyo.
Magazeti yanaandika Simba ilifungwa na Sofapaka ya Kenya mabao 3-0 Alhamisi katika mchezo wa kirafiki kwa sababu ya kupwaya kwa Keita na Ochieng wanaocheza pamoja katika beki ya kati.
Tayari huo unachukuliwa kama mwendelezo wa makosa ya Simba katika usajili wa wachezaji wa kigeni, baada ya akina Lino Masombo, Mbiyavanga na Mudde.
Mara nyingi nawaambia watu, kusajili wachezaji wazuri ni jambo moja na kuwa na timu nzuri ni jambo lingine- timu nzuri ni ile inayotayarishwa taratibu baada ya usajili.
Mfano mmoja ni jinsi ile timu B ya Simba iliyochukua Kombe la BankABC mbele ya vikosi vya Ligi Kuu vya timu za Azam FC na Mtibwa Sugar- kwa sababu imekaa pamoja muda mrefu na wachezaji wamezoeana.
Sasa leo Simba inasajili wachezaji wawili kutoka timu na nchi tofauti, inataka ndani ya wiki moja tu wacheze pamoja kwa maelewano, jamani hicho kitu hakiwezekani.
Miezi miwili iliyopita wakati wa michuano ya Klabu Bingwa Afrka Mashariki na Kati, Kombe la Kagame watu walianza kumkosoa Felix Sunzu- bahati kwake hayupo kwa sasa, lakini kama angekuwepo na matokeo haya, zengwe lingeendelea na upande wake pia.
Sijui hata hao wanaojiita wachambuzi huwa wanachambua nini- maana tatizo la Simba hivi sasa linaonekana wazi na litahitaji muda kidogo.
Kifo cha Patrick Mutesa Mafisango ndio kinaitesa Simba kwa sasa- hajapatikana kiungo mbadala wake wa kuiongoza timu. Jamaa alikuwa ana mchango mkubwa sana kwenye timu enzi za uhai wake na kwa kiasi kikubwa ubingwa wa Ligi Kuu ulitokana na yeye.
Tulikuwa tunaishuhudia Simba inacheza ovyo, inapoteana kabisa msimu uliopita ilipocheza bila Mafisango. Wakati Simba ikiwa inajiandaa na mchezo wa marudiano na ES Setif ya Algeria ilimsimaisha Mafisango kwa utovu wa nidhamu na ilipocheza mechi ya Ligi Kuu na African Lyon bila kiungo huyo, iligundua haiwezi kwenda bila mtaalamu huyo (R.I.P.).
Ilicheza ovyo na kushinda ‘kizali zali' 2-0 na baada ya hapo ikamrejesha kundini Mafisango akasafiri na timu Algeria. Huyu ndiye alikuwa mfungaji bora wa timu msimu uliopita kwa mabao yake 10.
Alikuwa anajua kuichezesha timu- sasa hayupo na bahati mbaya zaidi klabu haijampata kiungo mpya mkabaji, hivyo safu ya ulinzi inakuwa na mzigo mkubwa.
Katika soka, kitaalamu mabeki wakiwa wanamrudishia mipira mingi kipa basi kuna tatizo kwenye kiungo pale chini katika kuiunganisha timu na hilo ndilo linalojitokeza kwa sasa katika Simba.
Simba inacheza vizuri ikiwa na mpira, kwa sababu ina viungo wengi wachezeshaji, lakini tatizo linakuja mpira unapohamia kwa wapinzani- wanapita kiulaini na safu ya ulinzi ya klabu hiyo inafikiwa mno, tena kwa urahisi.
Mipira inapenyezwa mno kwenye eneo la hatari la Simba- sasa wazi hapa kabla ya kuanza kuwatazama mabeki, Simba waimulike safu yao ya kiungo.
Pamoja na hilo, kubwa ni kwamba bado timu haijazoeana na hilo limetokana na ile wachezaji wanasajiliwa, wanafukuzwa- maana yake kila siku timu inaanza upya na sasa tushukuru pazia la usajili limefungwa hadi Januari, timu haitabomolewa tena.
Amri Kiemba na Jonas Mkude ndio viungo pekee wakabaji katika Simba kwa sasa ambao siku za karibuni hawapangwi- mi nitabaki kuwa mwandishi na mchambuzi, lakini Profesa Milovan Cirkovick ni kocha na mtaalamu, hivyo anajua anachokifanya.
IIa nachoweza kumshauri tu, babu huyo wa Kiserbia apunguze kujiamini kwa sababu, maamuzi mengi ya viongozi wa Simba hutokana na presha ya mashabiki au vyombo vya habari.
Mwandishi mnazi kwa hasira zake, timu yake imefungwa anaweza kuandika kwa jazba bila kuzingatia vigezo wala utaalamu akaponda timu na wachezaji na kiongozi asiye mweledi kesho akafukuza mchezaji. Hiyo ndio soka ya bongo.
Sasa kama hawa wanaowaponda Ochieng na Keita mapema yote hii, ni kwa sababu ya zile bao tatu za Sofapaka- ila kama Wakenya hao wangepoteza nafasi zote hizo na Simba wakatumia japo nafasi moja kati ya tatu walizopata, mabeki hao leo wasingekandiwa.
Ufike wakati sasa Simba wakajifunza kuwa na subira. Wakajifunza kutokana na makosa, kwani msimu uliopita walimfukuza Derrick Walullya wakiamini ni galasa, ila alikuja na URA kwenye Kombe la Kagame Julai mwaka huu akacheza soka baab kubwa, udenda ukawatoka.

haya yanauhusiano gani na thread hii inayohusu yanga kupata point 1?
 
wewe jamaa tafadhali usirudie kosa kwani wewe unautaja uislamu tumekukosa nini?Acha amani idumu .
kweli wewe una matatizo ya macho!!!!!!!!hebu fuatilia hiyo thread nzima uone kama nimeongelea uislamu hata sehemu moja!!!!!angalia hata hiyo quote uliyo ichukua vizuri kama ina hata neno uislam?anyway nimekusamehe kwa sababu ilikuwa post yako ya 17 huenda hujajua unacho kifanya!!!
 
jamani yaaani twite hajasaidia?

Tuliokuwepo sokoine ndo tunaweza kuelezea vizuri, prison ni wazuri na wana mijibeki miamba yamepanda ulinganishi na mabeki wowote wa ligi kuu, habari ya twite nayo ni nyingine kabisa, pamoja na yanga kuto kushinda twite ni yuleyule tuliyemuona kagame na alionekana kucheza zaidi ya alivyocvheza kagame. tuache kuwabeza wachezaji twite bado ni mchezaji moto wa kuotea mbali
 
Ha ha ha ha ha Waombe radhi tafadhali. Na hiyo Avatar yako imekaa kishabiki mno.!
 
Kocha wao anasema walifikia hotel mbovu, chakula kibovu na yeye mwenyewe alimaliza siku mbili bila kuoga, wachezaji wa Prisons walicheza kwa kupoteza muda tangu sekunde ya kwanza ndo maana hawakupata goli; hapa inaonekana Yanga hawakumiliki mpira kabisa kama walimiliki kwa kwa nini wapinzani wapoteze muda, hao ndo mabingwa wa Kagame, Mbeya tu hapa wanashindwa kuoga siku mbili je wangeenda Sudan si wangekufa kabisa.
 
Hakuna cha ajabu kutoa droo kwenye mechi za ligi. Ni kitu cha kawaida na ligi bado mbichi.

Tena hata kufungwa Yanga ingewezekana maana sijaona mpira wa ajabu sana kwa hizi timu zinazodaiwa kufanya usajili wa kufuru. Mpira ni ule ule.
 
Kocha wao anasema walifikia hotel mbovu, chakula kibovu na yeye mwenyewe alimaliza siku mbili bila kuoga, wachezaji wa Prisons walicheza kwa kupoteza muda tangu sekunde ya kwanza ndo maana hawakupata goli; hapa inaonekana Yanga hawakumiliki mpira kabisa kama walimiliki kwa kwa nini wapinzani wapoteze muda, hao ndo mabingwa wa Kagame, Mbeya tu hapa wanashindwa kuoga siku mbili je wangeenda Sudan si wangekufa kabisa.

Umeshuka pointi nzito saaanaa aisee!haha
 
Back
Top Bottom