Yanga na Manqoba imeisha hiyooo

Yanga na Manqoba imeisha hiyooo

Hawatapata Kocha kama Yule walitakiwa mashabiki wamlinde kwa wivu mkubwa, viongozi hawaitakii mema yanga! Adios Kocha la Makombe!
 
Sidhani kama shida ni kocha.

Kuna mdau mmoja aliwahi kusema, nanukuu, Hii Yanga ishajifia, inafichwa na matokeo. Mwisho wa kunukuu.
 
Wachezaji hawana shida, kocha ndiye alikuwa tatizo. Hivi ukiulizwa mfumo wake ulikuwa upi? Hivi ulikuwa unaona sub alizokuwa anafanya? Pale hakuna kocha!
Anayeona tatizo ni wachezaji pale Yanga basi hajui mpira.

Manqoba alikuwa tatizo kwa 100%

Yanga kumtimua wala hawajakosea.
 
Anayeona tatizo ni wachezaji pale Yanga basi hajui mpira.

Manqoba alikuwa tatizo kwa 100%

Yanga kumtimua wala hawajakosea.
Uko sahihi mkuu! Kikosi kile kiko vizuri sana, akipewa kocha wa boli kinaweza hata kutinga fainali ya CAF. Ulishaona wapi kocha hana first 11?
 
Ata hivi tumemchelewesha.
Angekuwa anaona timu inapotea angekuwa anakili.
Sasa yeye mashabiki tunaona timu hii inapotea, yeye anasifia anasema hapa timu imejiimarisha sana.
Mmmmmmh
Mpaka tufungwe ndyo muelewe kocha hafaiii?
 
TAARIFA KWA UMMA

OKTOBA 24, 2026

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu umma kuwa umefikia uamuzi wa kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu ya kwanza,

Mangoba Mngqithi.
Vile vile, Uongozi wa Young Africans Sports Club umesitisha mkataba na Kocha wa Viungo wa timu ya kwanza, Chyna Mokaila.

Uongozi unawashukuru Watendaji hawa kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri kwenye majukumu yao mapya.

Tayari mchakato wa haraka wa kumpata Kocha Mkuu mpya umeanza na unatarajia kukamilika hivi karibuni.

Imetolewa na: Afisa Mtendaji Mkuu

Young Africans Sports Club

View attachment 3697780

View attachment 3697757
Dah! Kuna baadhi ya watu humu JF naanza kuwaogopa!
Kuna waliowahi kusema huyu kocha Maboga Mabichi hafiki Krismasi na imekuwa hivyo!!!!
Mi naomba tu wasiniambie, "Mtoto wa Shule, haufiki umri wa kustaafu"! Nitalia saaaaanaaa!!
 
Sidhani kama shida ni kocha.

Kuna mdau mmoja aliwahi kusema, nanukuu, Hii Yanga ishajifia, inafichwa na matokeo. Mwisho wa kunukuu.
Huwezi kuwa na timu iliyojifia afu inabeba vikombe karibia vyote, ni hoja inayokosa mantiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom