Yanga na katibu mpya Mkenya

Yanga na katibu mpya Mkenya

Ushabiki, unazi na siasa tuweke kando, kisha tujiulize: (1) Ukatibu Mkuu Yanga unahitaji kwanza uanachama? Kama jawabu ni ndio, na mwajiriwa si mwanachama, hapo kuna kasoro. (2) kwa mujibu wa katiba ya Yanga, nani ana jukumu la kuajiri? Kama walioajiri hawana mamlaka hayo kikatiba, hapo kuna kasoro (3) kwa mujibu wa taratibu za uajiri wa klabu ya Yanga, kuna ulazima wa nafasi kutangazwa? Kama ulazima huo upo na haikutangazwa, hapo kuna kasoro (4) uzoefu wa ujazaji nafasi kama hizo ndani ya Yanga unaelekeaje, kwa kuangalia na akina Sendeu na Mwalusako. Taratibu hizo zilifuatwa? Kama hazikufuatwa, wazee na wanachama walilalamika? (5) wakati wote wa kujadili mada hii muhimu ni kuzingatia kwamba kinachopingwa si kuajiriwa Mkenya, bali iwapo taratibu zilifuatwa.
 
Sio mbaya, mbona mwenyekiti wameoutsource kutoka nje ya bara kabisa, kwa hiyo katibu mkuu akitoka nchi jirani poa tu, na TFF wasingeweka sheria ya wachezaji watano nadhani timu nzima ingekuwa na wageni, kuna kipindi walikuwa na wachezaji kumi wa kigeni.

Hamia simba
 
Kwa akili matope kama hizi basi soka la Tz lina safari ndefu bado. Wengi wa waswahili wanajidai kufuatilia soka la ulaya bila kuelewa mfumo unaotumiwa na vilabu vya huko. Hakuna kitu nakichukia kwenye mfumo wa vilabu vyetu kama kamati ya wazee wa klabu. Hawa hujiona daima kuwa wanalifahamu soka vizuri kuliko viongozi wa vilabu. Hutaka wawe na maamuzi ya mwisho vilabuni. Hata kama angeletwa David Levy kusimamia vilabu, angejikuta akilazimika kupokea orders kutoa kwa waharibifu hawa. Katika ulimwengu ambao soka ni sayansi, ni aibu kubwa kuwa na mtazamo kama huu wa wazee hawa. Management ya timu ni zaidi ya upenzi. Wangefanya hivi Azam FC wasingekuwa na tatizo kwa vile wana mfumo wa soka la kisasa. Ingeonekana ni hatua kuelekea soka la kisasa.

Tubadilike ndugu zangu. Nina uhakika hakuna mwanachama hata mmoja wa Yanga aliye na uzoefu wa mfumo wa soka unaotumika na vilabu vilivyopiga hatua barani Afrika na ulaya. Wooote wanaelewa soka la fitna za kibingo bongo ambalo limeprove failure. Tunataka management ya kisayansi na si kikundi cha opportunists wanaoamini katika ndoto za alinacha.


Thanks.
Mkuu hiyo management ya kisayansi unaitoa wapi wakati timu inaongozwa na kamati ya utendaji ambayo ni ya wanachama watupu na ndo yenye nguvu kuliko kamati yoyote, bado kamati yenye nguvu inaundwa na mkutano mkuu wa wanachama ambao ndo hawaelewi hizo habari zako za kisayansi, mimi nazungumzia hali halisi iliyopo, mpaka hapo wanachama watakapokuwa hawana nguvu ya kuamua chochote kwenye klabu na hapo itawezekana tu endapo klabu itakuwa ni ya kampuni na si ya wanachama lakini kama itaendelea kuwa ya wanachama ni bora hata hao viongozi wa secretarieti wawe wanachama.
 
Back
Top Bottom