Yanga na Azam kucheza michuano ya kimataifa?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Upo uwezekano mkubwa kwa Tanzania kupata nafasi nne za uwakilishi kwenye michuano ya vilabu barani Afrika (CAF CL na CC) kutokana na uwezekano wa Libya kuondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kukosa sifa kwa kuwa hawakuendesha ligi yao kutokana na changamoto za kiusalama

Kupitia michuano inayoendelea msimu huu, Libya iliweza kuipiku Tanzania miongoni mwa nchi zenye sifa ya kutoa timu nne kwenye michuano hiyo baada ya kufikisha alama 16.5 wakati Tanzania ikishuka nafasi ya 13 ikiwa na alama 14

Hata hivyo kulingana na kanuni za CAF nchi ambayo haitaendesha ligi yake kwa angalau msimu mmoja inapoteza nafasi zake

Aidha nchi za Ethiopia, Sudan Kusini na Jamhuri za Afrika ya Kati nazo zimetangaza kujiondoa kushirikia michuano hiyo msimu ujao na hivyo kuongeza matumaini ya Tanzania kurudishiwa nafasi zake nne

Kama hili litatokea, klabu za Yanga na Azam Fc zitaungana na Simba na Namungo Fc ambazo tayari zimekata tiketi. Timu itakayomaliza nafasi ya pili itacheza ligi ya mabingwa wakati ile itakayomaliza nafasi ya tatu itacheza kombe la Shirikisho

Rais wa TFF Wallace Karia amesema bado hawajapokea taarifa rasmi kutoka CAF ingawa amekiri kuwa taarifa ya Libya kuondolewa kwenye michuano hiyo wameiona mtandaoni

Katika orodha ya nchi iliyotolewa na CAF zenye sifa ya kutoa timu nne, Libya haimo licha ya kushika nafasi ya 12 juu ya Tanzania inayoshika nafasi ya 13
 
hahaaa, hii ni habari mbaya sana kwa wazee wa fitna mikia fc, kwao ni maumivu makubwa sana kwa nguvu na 'kitu kidogo' walichotumia kuizuia tim ya wananchi, kumbe mjinga mmoja akikufungia mlango wa barazani Mwenyezi Mungu anakufungulia geti ili upite kwa kujidai………. kuna mijitu itajinyonga humuu
 
Ha ha wazee wa kulia kulia na visingizio visivyo isha hii tabia wanakua nazo wanawake na mashabiki ya yanga tu.
 
hahaaa, hii ni habari mbaya sana kwa wazee wa fitna mikia fc, kwao ni maumivu makubwa sana kwa nguvu na 'kitu kidogo' walichotumia kuizuia tim ya wananchi, kumbe mjinga mmoja akikufungia mlango wa barazani Mwenyezi Mungu anakufungulia geti ili upite kwa kujidai………. kuna mijitu itajinyonga humuu
mpaka mnaingia ni sisi tumewabeba ila uwanjani hamna uwezo na hata mkiingia huko bado mtatuaibisha lazima mkubali Simba baba lao
 
Back
Top Bottom