Yanga mmeturahisishia mbio za ubingwa

Numero Uno

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
353
1,000
Timu ya Yanga baada yakugomea muda wa mechi na hatimaye kuagirishwa Simba imenufaika kuahirishwa kwa mechi hiyo.

Kwani mpaka kuja kukutana na Yanga tena Simba itakuwa imeshapunguza idadi ya match na hivyo kupelekea kucheza bila presha yeyote.

Endapo Yanga ingekubali kucheza leo na kufanikiwa kuifunga Simba ingeweza kupunguza gap la point na kuwapa Simba wakati mgumu kwani watakuwa wapo kwenye mashindano ya caf na hapo hapo inatakiwa washinde mechi zao za ligi.
 

kijana13

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
1,348
2,000
Uko sahihi kabisa ..Mechi ya leo ilikuwa ya muhimu Sana kwa yanga kuliko Simba..walidhani wanawakomoa tff kumbe wanajikomoa wenyewe..
 

Nigga What

Member
May 1, 2021
34
125
Uko sahihi kabisa ..Mechi ya leo ilikuwa ya muhimu Sana kwa yanga kuliko Simba..walidhani wanawakomoa tff kumbe wanajikomoa wenyewe..

yote kwa yote Yanga wamefanya maamuzi ambayo timu yoyote kubwa yenye kujitambua ingeyafanya, tuache uswahili na ushabiki maandazi
 

Mario Kejob

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
382
500
Sababu za Yanga kususia mchezo ni:
1. Bifu lao na TFF la muda- Morrison ,Mwakalebela na suala la marefa kuwabeba Simba.
2. Kuogopa kipigo.
3. Kuizuia Simba kutangaza ubingwa baada ya mechi.
4. Kumpa muda kocha wao mpya aendelee kukinoa kikosi kama mechi itarudiwa.
5. Simba kukosa kipato kwani wenyewe waliisha chukua chao mechi iliyopita.
6. Ahadi ya Hersi ingevunjika baada ya mchezo huo.
7. Kutompa aibu kocha wao mpya baada kipigo kitakatifu.
8. Walidhani kuwa maamuzi hayo yalishinikizwa na Simba.


Makosa Yaliyofanyoka:
- TFF ingevishirikisha vilabu vyote katika kufikia maamuzi na sio kuamua tu kubadilisha muda.
-Yanga wangetumia tu busara kucheza mchezo huo kwa muda huo.
Mwisho:
Madhara yaliyosababishwa na maamuzi hayo ni makubwa na mengi majawapo likiwa ni kuipa nchi yetu sifa mbaya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom