Yanga kufanya kufuru Afrika Mashariki...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

Thursday, 04 April 2013 17:33Written by Mwandishi wetu

kaunda%20stadiu.jpg

Mchoro wa Uwanja wa kisasa wa Klabu ya
Yanga
kaunda%20stadiu1.jpg

Mchoro wa Uwanja wa Kaunda utakavyo kuwa ndani

Dar es Salaam

WAKATI viongozi wa Simba wakiendelea kurumbana wanachama wa klabu hiyo juu ya nani anastahili kuwa kiongozi halali bila kujali kuwa hali hiyo inasababisha maendelea mabovu ya timu hiyo,Watani wao wajadi Yanga wameanza kuonyesha mikakati dhabidi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa.​

Yanga ambayo ni Mabingwa Kombe la Kagame na vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara imefikia hatua hiyo baada ya Kampuni ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi yakinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani (Kaunda Stadium).

Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema upembuzi yakinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.

Zhang alisema kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 2010.

Aidha Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000 na utaanza Julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.

Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maarufu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.

Bravo!!! Yanga Yetu... Na nategemea UWANJA HUO SIO MKOPO!!! Tutalipa kwa Michango ya Wanachama...
 
Hapa Tz ukishaona statement "upembuzi yakinifu" Ujue hamna kitu hapo...Tunacheza dana dana..
 
Aah! Tutamwita baba Riz aje kufuungua, kwa kuwa na yeye ni mwanachama mwenzetu. Sijui atasemaje? tena mida hiyo atakuwa anahesabu siku za kuwaachia nyumba wana wa M4C.
 
Hahahahhaahaha I see watu wanataka kutakatisha fedha haramu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Aah! Tutamwita baba Riz aje kufuungua, kwa kuwa na yeye ni mwanachama mwenzetu. Sijui atasemaje? tena mida hiyo atakuwa anahesabu siku za kuwaachia nyumba wana wa M4C.

Labda aweke jiwe la msingi. Wakati wa kuufungua atakuwa alishastaafu.
 
Acheni kupiga mayowe kazi ndo imeanza.
 
YANGA werraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! Waache wenzetu waendelee kuvutana na kupigana majungu sisi tunapiga kazi tu!!
 
Waturuki wa mrs Libolo washafika tayari kuachia kitu huko Bunju!!!
 
Thursday, 04 April 2013 17:33Written by Mwandishi wetu

kaunda%20stadiu.jpg

Mchoro wa Uwanja wa kisasa wa Klabu ya
Yanga
kaunda%20stadiu1.jpg

Mchoro wa Uwanja wa Kaunda utakavyo kuwa ndani

Dar es Salaam

WAKATI viongozi wa Simba wakiendelea kurumbana wanachama wa klabu hiyo juu ya nani anastahili kuwa kiongozi halali bila kujali kuwa hali hiyo inasababisha maendelea mabovu ya timu hiyo,Watani wao wajadi Yanga wameanza kuonyesha mikakati dhabidi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa.​

Yanga ambayo ni Mabingwa Kombe la Kagame na vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara imefikia hatua hiyo baada ya Kampuni ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi yakinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani (Kaunda Stadium).

Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema upembuzi yakinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.

Zhang alisema kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 2010.

Aidha Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000 na utaanza Julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.

Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maarufu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.

HII ndiyo yanga bwanaaaaa!!!!!!!!!!!!
 
Hayo mandhari ya nje ya uwanja ndio pale kwenye bonde la mto Msimbazi?
 
Hapa Tz ukishaona statement "upembuzi yakinifu" Ujue hamna kitu hapo...Tunacheza dana dana..
hayo kwa ccm sio kwaa yanga, pole sana mtani ndo nakuacha hivo baki navyoo vyako pale kwenye msongamano
 
Hapa Tz ukishaona statement "upembuzi yakinifu" Ujue hamna kitu hapo...Tunacheza dana dana..
umenena MKUU,kwenye pesa ndio issue.hii imekua ni hadithi ya miaka tele
 
Mie ni Yanga damu lakini mpango huo naona kama ni kiini macho cha kutulaghai maana mosi eneo la kujenga uwanja huo hatuna kwani pale jangwani ni eneo dogo na finyu sana; na kwa sababu hiyo ulazima wa kuhamisha wakazi wa eneo la jangwani na bonde la jangwani ni lazima km mradi utatekelezwa. Na uhamishaji na ubomoaji makazi ni gharama za ziada ambazo sioni dalili kwa Yanga kuzimudu. Simba walianza ngonjera kama hizo za 'kujenga uwanja kule Bunju na Yanga tunaleta za Jangwani....Kuifikia Azam Kimaono ya mbali si jambo jepesi hasa kukiwa na viongozi na wanachama wababbaishaji, wachumia tumbo! I stand to be corrected!
 
Back
Top Bottom