Yanayojiri miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar 26/4/2015

Rais anayepewa heshima zote ulizotaja ni wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hoja hapa si suala la ukoloni bali muundo wa muungno wenyewe. Kwa mf. Wakati wa rais Mwinyi, serikali ya Tanzania bara iliongozwa na Mzanzibari. Ndo maana rasimu Warioba ikapendekeza muungano wa serikali tatu. Kama hoja ni ukoloni wa Tanzania bara, hata Mzanzibari aliwahi kuitawala Tanganyika.
 
Mambo ya muungano ni kuahirisha tatizo yatatokea ya south Africa
 
Naomba kuuliza mbona sijamwona mh. Lowassa au ndio ile taarifa ya kwenda matibabu Germany?
 
Napata kuamini hili kwamba Muungano ulipo sasa ni wa kinafiki na anganya toto kwa Watanzania kwamba kuna Muungano wakati in real sense ni usanii tu. Turudi kwenye mada ni kwamba Zanzibar ni Koloni la Tanzania bara, YES, Napata kuamini hivi kwa mambo yafuatayo:

1. Rais wa Tanzania Bara ndo mgeni rasmi kwenye sehrehe za Muungano
2. Rais wa Tanzania Bara ndo anapigiwa mizinga 21 kwenye sherehe hizi
3. Rais wa Tanzania Bara ndo anaimbiwa wimbo wa Taifa.
4. Rais wa Tanzania Bara ndo anakagua parade ya jeshi letu.
5. Rais wa Tanzania Bara anapewa heshima zote kwenye sherehe hizi.
6. Gwaride la heshima linapita mbele kwaajili ya Rais wa Tanzania Bara na sio wa Zanzibar
7. Huku Rais wa Zanzibar akitoa udenda pale jukwaani kwa yale anayofanyiwa Rais wa Bara.
8. Akili za viongozi wa Zanzibar zikiwa zimeshikiwa Bara.
9. Kwa haya yote Napata kuamini hakuna Muungano bali, Zanzibar ni Koloni la Tanzania Bara huku kiongozi wa Zanzibar akiwa kama Mayor wa kufanikisha unyonyaji huu.

WATANGANYIKA TUFURAHIE MIAKA 51 MUUNGANO TANGANYIKA NA KOLONI LETU (ZANZIBAR)

Kikatiba, muungano wetu ni union, yaani taifa moja la Tanzania ambalo ni a United Repulic of Tanzania, lenye rais mmoja tuu, kwa sasa ni Jakaya Kikwete. Japo nchi zetu ni nchi mbili zilizoungana, bado zina serikali mbili lakini sio marais wawili, ndani ya set up ya muungano, Amiri Jeshi ni mmoja tuu, rais wa JMT!. Kwenye setup ya muungano, rais wa Zanzibar ni nobody, ila ili asijisikie he is nothing, amepewa uwaziri usio na wizara maalum ndani ya JMT hivyo anaingia ndani ya cabinet.
Pasco
 

Kwenye setup ya muungano, rais wa Zanzibar ni nobody, ila ili asijisikie he is nothing, amepewa uwaziri usio na wizara maalum ndani ya JMT hivyo anaingia ndani ya cabinet.
Pasco
Mkuu Pasco napata shida sana kulifikiria hili, hivyo baadhi ya viongozi wanavyoimba kuwa wanataka Zanzibar huru wapo sahihi???
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndo tunaishangaa hii serikali na vibaraka wake kama ile issue ya pengo alivyojitokeza kuwapinga maaskofu waliotoa matamko kwa waumini wao kuipigia kura ya hapana katiba pendekezwa,eti hawana haki!hivi leo serikali inapata wapi haki ya kuwasjawishi watanzania waipigie hiyo hiyo katiba kura ya ndiyo?

impunity!! serikali haifuati sheria zake yenyewe! kunahaja wanaharakati kuanza kuwashtaki mahakamani hawa watawala.

Kwani kampein zimeruhusiwa kisheria au kwakuwa wanaamini watanzania woote ni wehuu!
 
Haya maadhimisho ni ya ccm na serkali yake. Katiba inayopendekezwa ni ya ccm na serkali yake. Kama siyo mwana ccm hayakuhusu waache waendelee na kampeni zao

Kama hivyo ndivyo Watanzania hatuna chetu. Kwani hata Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umeanza kusalitiwa na wanaojiita wazalendo? Tunaelekea wapi?
 
Tz tuna matatizo.
Nilikuwa sijauona uwanja wa uhuru mida, kumbe umesogea hivyo kiujenzi???
Kwa nini tumejenga viwanja 2 world class karibu karibu hivyo?????
Nina mashaka na watu wanaofanya planning hapa Tz.
hata mimi nimeshanga sana ,hivyo viwanja ni kama kiwanja kimoja tu, chenye ukumbi A na B
 
Naomba kuuliza mbona sijamwona mh. Lowassa au ndio ile taarifa ya kwenda matibabu Germany?

Haha..au yupo busy kutengeneza hospitali ya marais yenye ikulu ili aongeoze nchi kwa remote...tofauti na swahiba aliyemtosa ambaye aliacha NCHI KTK AUTO PILOT?

Akiingia hapo uwanjani anaona kama amejinyea kila mtu hamtaki.nasikia amelazwa ujerumani huko anaumwa.

Kwa mshangao mkubwa niko hapa uwanjani lakini hadi sasa sijamuona Edward Lowasa wa Richmond . Mzee yule ni mpenzi wa halaiki lakini leo nashangaa sijamuona . Mwenye taaraifa tafadhali au atakuja baadaye ?
Msaada jamani toka kwa team Lowasa

Kwani amesharudi...???lowassa
 

Attachments

  • 1430047488833.jpg
    1430047488833.jpg
    80.3 KB · Views: 242
  • 1430047633791.jpg
    1430047633791.jpg
    69 KB · Views: 232
Raisi wa Zanzibar hazidiani sana na mkuu wa mkoa, Tofauti yake ni kupigiwa mizinga wakati wa sherehe za mapinduzi na kupigiwa kura na wazanzibar. Lakini yeye ni RC wa zanzibar
 
Jk si aatngaze tena hapa kuwa EL hawakukutana barabarani km alivyosema kule mvunguni pa nchi Monduli?Lowasa ni mjinga km mkwere ndio maana mara zote anaamini JK atasimamia kauli this time.
 
nimefuraishwa na kikundi cha vijana ulinzi wamefanya vizuri tuwapigie makofi wamewafunika wanajeshi wa ukweli
 
Back
Top Bottom