Yanayojiri bungeni Dodoma: Leo tarehe 6 June, 2014

Yanayojiri bungeni Dodoma: Leo tarehe 6 June, 2014

Mmojawapo huyu hapa

Mkuu Ziongate
Huyu jamaa inaonekana anatafuta MUME sasa anajibanza banza kwangu hapa akitafuta huruma naomba umsaidie tafadhari maana mimi huwa sidill na watu wa namna hiyo mkuu.

BACK TANGANYIKA
 
Teh teh teh fisadi hadi kwenye mitandao..

Ohhhhhh kumbe hawa ni mafisadi wa kuzaliwa,.....sasa itakuwaje pindi liccm likipumzishwa mkuu watafisadi nini kama sio matandiko yao yenye kunguni mkuu.

BACK TANGANYIKA
 
Wana JF,

Nimekuwa nikisikiliza bunge letu tukufu na pengine kivutio kikuu au kichekesho kikuu ni huyu Mh. spikaaa bi Anna Makinda anapomwaga kiswahili chake cha "kibena" kufafanua jambo fulani. Kwa mfano leo kivutio kikuu kilichofanya hadi baadhi ya wabunge wacheke ni pale alipowaambia wabunge wawe wanaangalia saa kabla ya kuchangia lakini kwa msemo wake "nimewaambia tosomage saa pamoja hee!" iliwaacha hoi wabubge wengi. Nashauri baraza la kiswahili na la kiingereza kama lipo wampe "tuition" huyu mama. Nasikia akiongea kimombo hali inakuwa ni mbaya zaidi.

Ni hayo tu kwa leo.

ha ha ha beya beya
 
Komba leo hana mgeni mpiga kura aliyeenda kumchum na kumnyonya chuchu aje atutambie tena.? maana simuoni mjengoni..!!
 
yaani ni mwendo wa "senk yuu vere machee, sasa namwita kingunge ngombare mwiru, akifuatiwa na injinia stela manyanya wakati joni pombe akijiandaa" teh teh teh mkuu ni full burudani.
Haki ya Mungu sitazeeka mie jamani mbavu zangu
 
''I AM A WOMAN IN LOVE by Barbara Streisand''.Madam Speaker Sir,listen the song pliz.. naunga mkono hoja.
 
Hivi zile tuzo za MTV MAMA anazoshiriki DIAMONDI PULATINAMUZ zimeshafanyika tayari?
 
Aliwaambia vile kwakuwa wengi waliouliza maswali ya nyongeza ukiacha wale waliouliza maswali ya msingi waliuliza maswali toka majimbo yao kitu ambacho waziri hawezi jibu kwakuwa hakujiandaa nayo. Alishawaelekeza ndio maana akawaambia msishangae mtapata majibu ya hovyo hovyo. Mfano swali la msingi mbunge anauliza matatizo ya maji kyela, mwingine anauliza la nyongeza kilolo hapo itakuwa ngumu kwa wakati huo kwakuwa waziri hakujiandaa kwa kilolo. Ndivyo utaratibu wa kuuliza maswali ya nyongeza. Alikuwa anatoa tahadhari tu.
kwani kama hakujiandaa kwa nini asijibu kwamba sijajiandaa au ajibu hilo silijui kuliko kujibu jibu la hovyo, hii inaonyesha waziri kuji tuhata kama haelewi lolote ndio maana jibu linakuwa la hovyo
 
Ndugu wanajamvi,

Nimemsikia spika Makinda leo akiwaambia wabunge kwamba wakijibiwa majibu ya ovyo ni sawa. Ina maana yeye kama spika kwake yeye ni bora tu waziri ajibu hata likiwa jibu la ovyo?

- Wazee wazee wazeee, ni wakati Leticia Nyerere anauliza swali la nyongeza bungeni leo, ameishauri serikali ianzishe wizara ya kushughulika na wazee katika mambo muhimu kama; matibabu, chakula, malazi hasa wale ambao hawana pension.

Aidha katika michango yake ya leo ameongea vizuri sana pale anapowashauri watu wawe na uzalendo na taifa lao na waache kupost vitu vya ajabu kwenye mitandao.

Hongera sana mama! Watakuwa wamekuelewa wale wenye tabia hizo.

vipi UKAWA leo hatutoki nje ya bunge? mda sasa hatujaenda kunywa juice Ikulu.
 
Utazeekaje wakati kuna kipindi cha the komedi show ukumbi wa bunge dodoma?

Mkuu nashangaa masuala ya bunge siku hizi hayapati michango ya kutosha humu JF....kule kwenye picha nyuzi zinakimbia mbio nyingi.
 
Huwezi kuamini kwa sababu na wewe ndo walewale mliokulia katika familia zilezile, chama kilekile na mifumo, ileile ya .........sadi:israel:
 
Mkuu nashangaa masuala ya bunge siku hizi hayapati michango ya kutosha humu JF....kule kwenye picha nyuzi zinakimbia mbio nyingi.

Nadhani wadau wameshachoka na maigizo ambayo mwisho wake ni kibwagizo cha "wanaokubali bajeti hii ipite waseme ndiyo.....ndiyooooooo, wanao kataa waseme siyo......siyoooo, nafikiri waliosema ndiyo wameshinda na kwa hiyo bajeti imepita"
 
Back
Top Bottom