Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Ali Omari Makame anasema;
Hii katiba tuliyo nayo imerekebishwa mara 11 lakini mambo ya ulemavu hayamo. walemavu tunataka elimu afya mikopo na ajira na mazingira rafiki.

Mimi ni muumin wa serikali mbili. Mimi sikusoma, wasomi wtatuelekeza. je serikali tatu gharama zinakuaje? sisi walemavu tunataka huduma, kwanini hizi gharama za serikali ya tatu zisisaidie wenye ulemavu? Tusaidieni tutoke hapa tulipo sisi walemavu halafu ndo mfukirie kuongeza serikali ya tatu na ya nne. Watu wenye mahitaji maalum itamke ni watu wenye ulemavu. vipofu vigulu viwete ni maneno ya kutudhalilisha.

Kubomoa kunasababisha wajane na yatima. mkibomoa watakao pata tabu sana ni sisi walemavu. mimi naunga mkono serikali mbili
Huyu naye ni kichaa sasa bila kujuwa kwamba kuna vipofu yangeandaliwa maandishi maalum na fimbo nyeupe?

Mimi naona anajidharirisha mwenyewe tu akili ndogo kutumiwa na maccm zile rushwa za ubwabwa sasa tunaona zikifanya kazi.
 
Huyo mbona mpuuzi anaongea umaluun gani hapo...!?

Kama fani ni yako, bora aketi kimya.
 
Hamis mnondwa anasema;
Mimi nipo serikali mbili. mimi nina sababu ya kushabikia hayo nliyo yasema. hizi serikali mbili kama zina matatizo yanaweza kuboreshwa.
kwanini tusizungumzie ajira za vijana na tunazungumzia mfumo wa serikali?. Tukiongeza serikali ya tatu ina maana tanzania bara na zanzibar bye bye.
sasa hivi zanzibar wanajiuliza jeshi kubwa liko bara, hatuna hela za kugharamia uhamiaji wlala hatuna mipaka. Tukiongeza serikali ya tau habari la muungano limekwisha.

Kwanini tusikae tukazungumzia msitakabari wa nchi? muundo wa serikali tatu ni muundo ambao hauna shida. upo kwa ajiri ya kusimamia majeshi na madaraka. haina ardhi. je serikali tau itajenga wapi ofisi? je ni nini kitafuata kama sio mapinduzi? tutaliwa kodi mpaka ya kichwa. kodi ya kichwa itarudi.
 
Sasa kodi ya kichwa kwa akili yake aona haipo mbona mpuuzi kiasi hiko..!?
 
Mlemavu anasema kuwa kutumia majina kama vipofu, viwete, viziwi ni kwadhalilisha walemavu,
Mimi sijamuelewa huyu mtu, anataka kipofu au kiziwi aitwe nini?, wawe wanaitwa tu walemavu bila kuainisha aina ya ulemavu?
 
Dear JF Members,

Let us ask ourselves a simple but tough questions,

Is the union between Tanganyika and Zanzibar popular today as it had been before?

Provide your positions with some concrete example supported by authorities,

Hope to bring light to young generations,

Does the young generation knows how the union was formed,how the founders met,with what objectives,

With regards,

Elisante Yona
 
Zainabu kawawa,
Anaanza kwa kupinga muundo wa serikali tatu.
serikali ya shirikisho haina maana kwa kuwa haitoi huduma yoyote ya kijamii.
Anawaponda viongozi wa upinzani kuwa wanamponda baba wa taifa lakini wao wanasifa gani ya kuvaa koti la baba wa taifa.
 
Huku ni kupoteza bure hela za walipa kodi bunge la katiba halina tena jipya .Wakati umefika waamue kama mbili au tatu bila tusonge mbele kuliko kuendelea kutafuna hela za walalahoi...KIWI CHA MACHO
 
Anayefuata sasa ni Hamisi Mnondwa. Anasema kuwa yeye ni muumini wa serikali mbili. Anasema kuwa matatizo yaliyopo kwenye mfumo wa serikali mbili yanaweza kutatuliwa. Anawataka wabunge kuangalia mustakabali wa vijana waliokosa ajira badala ya kuongeza ukubwa wa serikali. Pia anasema kuwa kuna watu wanadhani kuwa ikiwepo serikali ya tatu watapata madaraka wanayoyahitaji kitu ambacho anasema kuwa si sahihi.


kuhusu takwimu, anasema kuwa takwimu zilizotolewa na tume si za kweli kwani ushahidi wa mabaraza ya kata unaonesha kuwa wananchi wengi walipendekeza mfumo wa serikali mbili.


kuhusu gharama za serikali ya shirikisho, anasema kuwa kutakuwa na tatizo kubwa la kuigharamia. Kwamba hakuna serikali itakayokubali kubeba mzigo wa serikali ya shirikisho wakati ndani ya nchi yake kuna matatizo mengi kama barabara, maji, afya, umeme nk. Kwa hali hiyo anasema kuwa tukiongeza serikali ya tatu ni wazi kuwa muungano huu utakuwa umekufa. Anasema kuwa muungano huu umeanzishwa si kwa ajili ya kufurahisha watu bali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.


kwa hali hiyo anawashauri wabunge kukaa na kutafakari jinsi ya kutatua kero za muungano na kushughulikia matatizo ya wananchi. Kwani muundo wa serikali tatu hauna tija kwa vile serikali ya tatu licha ya kumiliki majeshi, haina ardhi wala rasilimali nyingine. Kutokana na hali hiyo anasema kuwa upo uwezekano wa mapinduzi ya kijeshi kutokea. Anasema kuwa serikali ya tatu haibebeki. Pia anaongeza kuwa mfumo wa shirikishoukiwepo, kutakuwa na kodi nyingi mpaka ya kichwa ili kugharamia serikali ya tatu
 
Wasitudanganye eti serikali tatu zitaongeza gharama, mbona leo hii tuna serikali mbili na bado deni la taifa linazidi kukua na hali ya mtz inazidi kuwa mbaya!
Hapa ni serikali tatu mpaka mwisho na hayo ndio maoni ya wananchi!
 
Matatizo ya kuwapa fadhila kila ati mtoto wa kiongozi hata kama ni bubusa kama huyu binti wa Kawawa.

Yaani yule Nyerere kawa nani hata asijadiliwe mpuuzi mkubwa huyu.

Maloun aende akasome kisha akasimame tena na marupurupu ya MISUKULE wanzie.
 
Zainab Kawawa anasema;
Nataka nizungumze na watanzania leo kwanini sikubaliani na serikali inayo itwa ya shirikisho. nchi ndio inayozaa urai na kutengeneza utaifa.
Jamhuri hiyo ya tanzania haitoi huduma za afya, elimu na huduma zozote. haiwezekani.
viongozi wa upinzani igeni mfano wa viongozi wa ccm, kwanini chama kimeendelea kua imara. nyie hamna utashi wa kuvumilia na kukosoana. Muna hadhi gani ya kuvaa koti linalofanana na wasisi wa nchi hii. Wajumbe wameonesha dhamira ya kuvunja muungano wetu.

Hivi nyiynyi mnaotaka serikali tatu kwania mbaya mnaonesha dhamira ya kuuvunja muungano huu. nani asiyejua chadema haina wanachama zanzibar? watanzania ndio wanao gawa uongozi. waroho wa madaraka ninyi. acheni njia za dezo. nawashukuru sana kwa kunipa nafasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom