Yanayojiri Bungeni Dodoma - baadhi wako nje au wanalala?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Ni kitu cha kushangaza Mheshimiwa Mbunge aliyeaminishwa na wananchi awawakilishe, lakini anachofanya ni kuhudhuria bunge.
Cha kushangaza zaidi anapouliza swali au hoja iliyokwisha pita, sasa wakati wenzake wanajadili hoja hiyo yeye alilala usingizi au fikra zake zilijikita kwingineko kiasi cha kutojua nini kinaendelea ndani ya ukumbi wa bunge?

Nkamia ‘awavunja mbavu’ wabunge
MBUNGE wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM), amegeuka kichekesho na kituko baada ya kuibuka bungeni jana kutoa taarifa ya swali kwa Spika wakati muda wa swali hilo lilishajibiwa na kuulizwa jingine.

Nkamia aliibuka kutaka kutoa taarifa ya swali namba 26, lililohusu ujenzi wa barabara ya Dodoma – Iringa na Dodoma- Babati lililoulizwa na Mbunge wa Dodoma Mjini, David Malole (CCM) wakati muda wake ulishapita na tayari swali namba 27 lilishaulizwa na lilikuwa likijibiwa. Nkamia alisema, “Taarifa Mheshimiwa Spika, napenda Naibu Waziri afahamu kuwa ujenzi wa barabara ya Babati-Bonga haujaanza kama alivyosema kwa kuwa mimi nimepita hapo jana (juzi)”.

Hatua hiyo ya Nkamia ilisababisha wabunge kuanza kunong’ona na wengine kucheka ndipo Spika Anne Makinda alipowashauri wabunge kuwa makini na maswali wanayouliza na kuzingatia wakati. Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Serikali imetenga Sh bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Manispaa ya Dodoma.

Akijibu swali la nyongeza la Mallole, Lukuvi alisema Serikali inatambua umuhimu wa barabara hizo za Manispaa hivyo fedha hizo zimetengwa tayari kuhakikisha kuwa zinakamilika. Mbunge huyo alitaka kujua fedha za awali ni kiasi gani zilitengwa, barabara zitakamilika lini na ujenzi wa barabara ndani ya Dodoma na Uwanja wa Ndege wa Msalato utakamilika lini.

Akijibu swali la msingi la Malole kuhusu ujenzi wa barabara ya Dodoma- Iringa na Dodoma-Babati (Arusha) utaanza lini, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe alisema ujenzi wa barabara ya Dodoma hadi Babati utafanyika kwa awamu na kwa kuanzia tayari ujenzi sehemu ya Dodoma hadi Mayamaya wa kilometa 43.6 unaogharimu Sh bilioni 40.6 umeanza na utafanyika kwa miezi 17......

Source: Habari Leo
 
ukiambiwa CCM imejaa vilaza ndo ivyo...

hawa kina vicky kamata sijui ni wabunge wanaowakilisha kina nini
 
Topic imeshafungwa jamaa anainuka na kutoa hoja, je alilala usingizi? Hawa wenzake wanamcheka ni kuashiria kushangazwa na yanayojilia bungeni. Wabunge wengine wapo tu kuhitimisha siku kisha wajaze posho zao.
 
Back
Top Bottom