Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,850
Kwa wale wanaopenda kufuatilia bunge. AzamExtra wapo live sasa
Huu ni muda mwafaka wa kujua mbivu na mbichi kuhusu tamko la Nape baada ya kamati ya uongozi kukaa.
=========
Anaeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa bunge na anatoa maazimio ya kamati, amesema mjadala uendelee kama ulivyopangwa na ambae hajaridhika afikishe malalamiko yako kwa mamlaka husika.
Lissu(Muongozo): Muongozo wangu unahusu uamuzi ulioutoa, Ni sahihi kwa mambo ambayo yanayotakiwa yatolewe uamuzi na spika/mwenyekiti na kutotekeleza madaraka yake na mambo hayo yapelekwe kwenye kamati ya uongozi. Tangu lini maswala ya kanuni yakapelekwe kwenye kamati ya uongozi badaa ya kamati ya kanuni?
Muongozo wa mwenyekiti(Chenge): Tafsiri ya mwenyekiti ni kama inavyosomeka kwenye kanuni(Anaisoma), kwa mila na desturi za bunge, pale ambapo kuna hoja inayohitaji maamuzi ya pamoja, kamati ya uongozi ikiongozwa na spika inafanya hio kazi. Mjadala wa hotuba ya Rais unaendelea
Chenge: Hatuwezi kutumia muongozo ku-delay shughuli za bunge
Heche: Ukisoma katiba yetu, kila mtu ana haki ya kupewa taarifa, mwenyekiti nafikiri tuko kujadili masuala muhimu ya waananchi wetu, itakua ajabu sisi kukaa humu ndani na kuvunja katiba na hoja hapa ni bunge kuruka live na hatua gharama anazosema Nape zinatoka wapi?.
Chenge: Mwingine anaetaka muongoza!
Wabunge wengi wa upinzani wamesimama kuomba muongozo
Chenge: Ndugu Heche, Hoja yako ya katiba, nalichukua hilo na tutalitolea uamuzi baadae, waheshimiwa wabunge haiwezekani wote hawa wakasimama kuomba muongozo.
=========
Hali ya sintofahamu Bungeni, Polisi waingilia kati, Wabunge wa Upinzani watolewa nje