Yanayojiri Bungeni 19 Novemba, 2015: Rais Magufuli amteua Majaliwa K. Majaliwa kuwa Waziri Mkuu

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Leo ndio siku ambayo Spika wa Bunge atafungua Bahasha yenye jina la Waziri Mkuu na kisha Bunge kuketi kama kikao kumpitisha ama kumkataa Waziri Mkuu Mteule.

Tujiunge mahala hapa kwa ajili ya Updates kutoa bungeni Dodoma

- Bunge linaanza na kazi ya kwanza kuthibitisha jina la waziri mkuu. Spika anasubiriwa aseme. Bunge kimyaaaa

- Spika anatoa utaratibu wa namna ya kuthibitisha jina na kuwa itabidi mwanasheria mkuu aandae profile ya mteule ambae sasa hamjui. Hivyo itabidi bunge liahirishwe kwa muda ili akaandae profile hiyo baada ya jina kusomwa. Katibu mkuu katumwa kufuata bahasha yenye jina now

- Msigwa aomba mwongozo kutaka bunge liahirishwe maana serikali inalidhalilisha bunge kwa kusubiri bila sababu.
Mwanasheria anajibu kuwa mtoa hoja ndie anadhalilisha bunge na hivyo anaitetea serikali kuwa usiri huu wa jina ni muhimu

-Spika anasema bahasha yenye jina italetwa kwa staili mpya katika Briefcase. Kisha briefcase itafunguliwa na bahasha kutolewa na jina kusomwa. Tunaendelea kusubiri

- Spika anakumbusha leo pia kuna uchaguzi wa naibu spika. Wagombea ni wawili. Dr Tulia Mwansasu na Magdalena Sakaya

- Katibu karejea na mpambe wa Rais (ADC) anaingia na bahasha aliyotumwa na Rais kumletea Spika. Spika anafungua Bahasha tatu na anatangaza kuwa Rais amemteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu

Spika anasema barua imeandikwa na Rais kwa mkono wake mwenyewe haikuchapishwa.

Spika anasoma; '' Job Ndugai, Mh Spika, mimi mwenyewe kwa nafasi yangu kama Rais wa JMT nimemteua Mbunge wa Ruangwa mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa JMT.''
attachment.php

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (Mb)

*Spika amesitisha Bunge kwa muda wa dakika 45.

-Bunge limerejea. Mwanasheria mkuu ametoa wasifu wa Kassim Majaliwa, kisha wabunge wanaendelea kumuelezea Majaliwa na kuunga mkono Uteuzi wake.

-Mbunge Saed Kubenea amtaka Kangi Lugora kufuta kauli yake kuwa Kubenea alipiga makofi kumuunga mkono Majaliwa. Spika amwambia ulikuwa mzaha hivyo aendelee kuchangia. Kubenea asisitiza kuombwa msamaha. Hatimaye Kangi Lugora aamua kuyaondoa maneno aliyoyasema kuhusu Kubenea. Katibu wa Bunge anatoa mwongozo wa upigaji Kura sasa

-Masanduku ya kura yamewasili. Kura ni ndio au hapana. Wabunge wanaanza kupiga kura now

-Baada ya kupiga kura za kumthibitisha Waziri Mkuu, itafuata zoezi la uchaguzi wa Naibu spika asubuhi hii. Wagombea ni Magdalena Sakaya wa UKAWA na Dr Tulia Mwansasu wa CCM
=======

Kinachoendelea kwa sasa na wagombea wanaogombea nafasi ya unaibu spika wanaomba kura na kwa sasa ni Magdalena Sakaya kupitia CUF, amesema ana uzoefu wa uongozi kwa miaka 20, kati ya hio miaka 10 ndani ya bunge. Sakaya akijibu swali la Kairuki kuhusu kufanya kazi na spika asie wa chama chake. Amesema kila mbunge anafanya kazi kwa ajili ya watanzania kuhakikisha matarajio ya watanzania yanafikiwa bila kuangalia chama.

Gekul: Umekuwa mbunge kwa awamu tatu, mawazo katika bunge hili hayatekelezwi na serikali, utatumiaje uzoefu wako kuunganisha bunge na serikali.

Sakaya: Tunatambua na awamu mpya ya awamu ya tano, tuna sura mpya za wabunge wengu, spika na tutakuwa na sura mpya ya naibu spika. Naamini sote tukiwa imara tunaenda kuyafikia matarajio ya wananchi.

Anaefata sasa ni Tulia Ackson kupitia chama cha mapinduzi (CCM)

Tulia: Kwa taaluma mimi ni mwanasheria na nimefanya hiyo kazi kwa miaka 14, nilishiriki kutengeneza kanuni zilizoendesha bunge la katiba. Nagombea nafasi kwa sababu najiamini na nina uwezo.

Matiko: Tunatambua alikuwa naibu mwanasheria mkuu na hakupaswa kuwa mwananchama wa chama chochote, leo unaomba nafasi ya unaibu spika, ukiwa mtendaji lakini tayari unachukua upande wa CCM. Unatuaminisha vipi hautaegemea upande!

Tulia: Nilichukua fomu za kugombania uspika nikiwa naibu mwanasheria, kwa ibara ya 67(ii) na 72, anashikilia nafasi mpaka awe candidate na kuwa candidate ni mpaka upite mchakato.

Matokeo ua Uwaziri Mkuu yametoka na Bunge limempitisha rasmi Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri mkuu kwa zaidi ya asilimia 70. Sasa Waziri Mkuu Mteule anatoa neno la shukrani. Anamshukuru Rais kwa kumteua na kusema atawatumikia watanzania wote bila kujali chama cha siasa anachotoka. Pia awashukuru wapigakura wake na wabunge pia kwa kumuamini.

Matookeo ya kura za Unaibu Spika yanasubiriwa.

Matokeo ya unaibu spika

Kura 351
Magdalena sakaya 101
Dr Tulia Mwansasu 250


 

Attachments

  • Waziri mkuu.jpg
    Waziri mkuu.jpg
    15.4 KB · Views: 34,800
Last edited by a moderator:
Naamini mleta Uzi utakuwa bungeni kutujuza kinachoendelea ,kwani huku tanesco wameshafanya yao.
 
Tetesi zinasema Makamba ndio waziri mkuu. Pathetic sana, kama atamteua Makamba nitajua kuwa kuna remote control.
 
Wote mnaowataja Hawafai kabisa anaye faa kwa kasi ya Magufuli ni Mwakyembe tu. ila kwa vile rais yuko chini ya kikwete ateteuwa Mnaowataja
 
Back
Top Bottom