Yametimia: Ngedere kwanza elimu baadae

MTENGETI

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,420
2,000
Kwa wanabodi wote! mwaka jana na pia mwaka huu nchi ilitingishwa na migomo ya walimu na madaktari. Mgomo wa madaktari athari zake ni on the spot kwani watu watakufa kwa kukosa matibabu. Mgomo wa walimu ni kama vile kula ile sumu aliolishwa Mwakyembe kwenye komoni au ulanzi manake kama ni kwenye bia ingefoka mapovu sana na angesanua.

Ni kipindi hicho cha mwezi wa julai mwaka huu Mheshimiwa sana, Profesa aliwasafirishwa walimu wote wa Wilaya ya Mwanga Mkoani kilimanjaro kwenda matembezi kwenye hifadhi ya wananyama pori huko Tarangire. Wakati huo huo walimu wakitumia mishahara yao kununua chaki na zana nyingine za kufundishia kwa mishahara yao. Huku ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ikiteketeza Tsh 40,000,000 kwa safari hiyo matokeo sasa yameanza kuonekanaHabari zilizovuja kutoka kwa maafisa elimu wanaoshughulikia kupangia wanafunzi shule za sekondari wanakuja na matokeo haya


  • NUSU ya wanafunzi walifanya mtihani wa darasa la saba wilayani MWANGA hawana sifa ya kujiunga na kidato cha kwanza mwakani kwani WAMEFELI MNO.
  • matokeo yakiwa serikali kupuuza na kuwatisha walimu kuhusu madai hayo (Hii ni countrywide) na kwa Mwanga ni ahadi za uongo, kukomesha maafisa elimu na wanasiasa (akiwemo Mbunge)

Naomba kuwasilisha

Source: Mkuu wa Mkoa kilimanjaro Bwana Gama kwenye kikao na baada ya Kikao na Walimu wa wilaya ya Mwanga tarehe 05/12/2012
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom