Yamenikuta....

Yamenikuta....

pole kapimetndo utapata jb sahihi km ushaungua unagonga vidonge life goes on mwaya
 
Story maana yake si hadithi!! Au simulizi!! Ninauhakika hili tukio sio la kweli!!
 
bongo movie, wapangaji wenzake walijuaje kuna vidonge na cheti kabatini?


Ndo matatizo mengi tunayoyaona kwenye movies zetu za kibongo. Watunzi na waandaaji viwango vyao vya kuelewa viko chini kuliko watazamaji.
 
inaweza kuwa stori au ya kutunga lakini ni nzuri, inaonya na kufundisha!
 
Kama ni kweli pole sana kaka, lakini usikate tamaa jipe moyo maisha yaendelee nenda kapime ujue ujue upo katika hali ipi, all in all Mungu anaweza kukuhepusha pia na hili likawa somo tu kwako, kila la kheri
 
vya bure vinaua, kwenye Facebook hadi kuvuliana nguo kavu kavu, dezo dezo hiyo.
 
kama ni true story, i real fil sor for u my brother...
 
pole sana sio vyote ving'aavyo ni dhahabu,nenda kapime upate uhakika wa maisha ya sasa na baadae ila mmmmh ngoja ninyamaze nilitaka kukushushia maneno hayo..................

na kweli,, bora kunyamaza na kumuombea......hahahaaaaa..... kavu tamuu eehh...
 
huu ni mkasa unaofanana na ukweli! inawezekanaje mtu akuache kwake akalale huko hadi asubuhi we umekoroma tu ndani tena ugenini na arudi sa 2 asubuhi na usitilie shaka tena kwa siku zote ulizo kaa? hata maswali humuulizi alikuwa wapi au huwa anaenda wapi na anafanya kazi au shughuli gani na yeye akuamini kukuachia nyumba kipindi chote hicho? umekaa kwake hata hiyo droo kuifungua hadi uambiwe na majirani? wewe ni mzembe. na huyo mdada amekubuhu hata kuzuga kwa mgeni kwa siku hata moja hawezi aiseee!!!!!! halafu mkuu sio wote wanapanda magari wakapata ajari huathirika wengine hutoka bila ya hata michubuko na gari likawa nyang'anyang'a. kapime kwanza.
 
Nilimpenda dada wa facebook nikamtongoza tukaelewana akawa mpenzi wangu kweli tulikuwa tuna muda mwingi tunachati facebook. Tuna enjoy na utani wa hapa na pale kwakuwa tulipeana namba za simu tukawa tunapigiana sana simu hasa mida ya usiku tunapiga story za kikubwa ile mbaya mimi nilikuwa nasoma chuo yeye aliniambia anafanya kazi huko Arusha japo akuniambia anafanya kazi gani?

Na aliniambia amejipanga kimaisha kwaiyo shida ndogo ndogo yeye hana Maisha yetu yamapenzi yaliendelea vzuri sana japo hatukuwahi kumit live live nilitamani sana nimuone naye alitamani pia anione coz siku zote tulikuwa tunapeana mapenz ya kwenye simu na kupeana hamu tu .

Nilimuhaidi chuo kikifugwa lazma niende likizo huko kwake Arusha kwakweli yule mpenz nilimpenda shida ndogondogo alikuwa ananisaidia sana kama vocher pesa alikuwa ananitumia za matumizi. Siku ya siku ikafika chuo kikafugwa yule mpenzi wangu alifulahi sana kusikia hizo habari akanitumia nauli nikaenda kukata tiketi nikajipanga kesho yake safari ikaanza.

Nikawa kwenye basi nilitamani basi lipae nifike faster nikakutane na mpenzi wangu, nilifika salama nikampigia simu akaja kunipokea pale stend kwakeli tulifulahiana sana tulikumbatiana kwa furaha.

Kwakeli yule mdada alikuwa mzuri sana jamani japo alionekana ana mwili kunizidi mimi lakini alikuwa ana shepu ya kuvutia sana, tukachukua tax tukaanza safari ya kuelekea nyumbani kwake tukafika nyumbani kwake akanikaribisha pale nje tuliwakuta wapangaji wenzake kama wa tatu hivi tukawasalimia akanitambulisha pale tukaingia ndani lakini kipindi tunaingia ndani kuna kauli kuna dada aliongea sema sikuyatilia maanani aliyema ''AMA MWAKA HUUATAWAMALIZA WENGI'' afu wakacheka wote.

tuliingia ndani akaniandalia maji nikaoga aliniandalia msosi wa nguvu jamani tukala tukanywa kwa kweli maandalizi yalikuwa mazuri sana tukapeana story za hapa na pale na utani mwingi mwingi tukacheza michezo ya kila aina mwisho tukajikuta kila mtu yupo hoi yaani anamuitaji mwenzake kimwili tulibebana hadi chumbani shughuli ikaendelea kwakuwa nilikuwa na hamu na yule mpenzi wangu alafu na kule ni ugenini sikukumbuka condom nikachovya kavu kavu tukapeana mambo kila mtu akalizika tukalala hadi asubuhi.

Aliamka asubuhi akaniandalia chai nkaywa akaendelea na shughuli ndogondogo za pale nyumbani me nkakaa sebuleni nikawa na angalia TV juu ya kabati ya tv nikaona album ya picha nkaichukua nikaanza kuangalia, ndan yaalbum kulikuwa kuna picha nyingi za mwanaume mmoja na picha nyingi alikuwa amepga na yule mwanaume wakionekana kabisa walikuwa wapenzi na picha nyingi zilikuwa zimewekwa X kumanisha yule jamaa ni marehemu.

Niliwaza mengi sana kuhusu hzo picha mara ghafla yule mwanamke akaingia akanikuta na angalia zile pcha alishtuka sana akaniuliza vp? Baby kuna tatizo??? Nikamjibu hakuna ila naomba uniambie huyu jamaa wa kwenye picha ni nani yako? Akacheka kisha akaniambia jamani baby huyu alikuwaga mpenzi wa zamani sana nikamuuliza yupo wapi? Akanijibu alikuwaga dereva alafu akapata ajali alifariki! DUU nilimsikiliza kwa makini nkampa pole kidogo roho ikatulia.

JAPO SIKUMUAMINI SANA SABABU ZILE PICHA ZILIKUWEPO HADI UKUTANI LAKIN KAPOTEZEA ILIPOFIKA UCKU KAMA MIDA YA SA 4 ALINIAGA ANAENDA KAZINI NILISHANGAA SANA KUONA M2 ANAENDA KAZINI SA 4 UCKU LAKN KWA KUWA SIKUWA KWANGU NILIMRUHUSU AENDE 2 KWA SIKU ILE NILILALA FRESH HADI ASUBUHI.

ILIPOFKA MIDA YA SA 2 AKARUDI MPENZI WANGU TUKAPIGA STORY MBILI TATU AKANAMBIA KACHOKA ANAHTAJI KUPUMZIKA NKAMWAMBIA POUWA.

MAISHA YALIENDA POUWA ZILE SIKU MBILI ZA KWANZA LAKN SIKU YA NNE NKAANZA KUBOREKA NA TABIA YA YULE MWANAMKE KWENDA KAZINI USIKU KURUDI ASUBUH LAKINI NILIVUMILIA TU.

SIKU MOJA NKIWA NAFUA NGUO ZANGU ASUBUH WALE WAPANGAJI WALINIFWATA WAKANSALIMIA WAKAKAA PEMBENIWAKANIAMBIA WANA MAONGEZI KIDOGO NA MIMI NKAACHA KUFUA IKABIDI NIWASIKILIZE, MMOJA AKANIAMBIA 'SAMAHAN KAKAWE NI KIJANA MDOGO MZURI HIVI UMEJIAMINI NINI KUTEMBEA NA HUYU MWANAMKE NA KWANZA UMEKUTANA NAYE WAPI NA UMEANZAJE SABABU WANAUME WOTE WANAMUOGOPA WEWE IMEKUAJE?" NILISHTUKA SANA KUSKIA ZILE HABARI NIKAWAELEZANILIPOTOKEA NA NILIPOKUTANA NA YULE MWANAMKE HADI NIPO PALE' WALISIKITIKA SANA KUSIKIA VILE WAKANIAMBIA YULEMWANAMKE ALIOLEWAGA NA MUME WAKE KAFARIKI KWA UGONJWA WA UKIMWI NA TOKA MUME WAKE AFARIKI ANAFANYA BIASHARA YA KUUZA MWILI NDO MANA HUWA ANAONDOKA USIKU ANARUDI ASUBUH NA WAKANIAMBIA KAMA NABISHA NIENDEKWENYE DRO YAKE NIKAANGALIE NTAKUTA VIDONGE NA CHETI CHAKE'

AKILI YOTE ILINIHAMA JAMAN NKAIONA DUNIA CHUNGU SIKUAMINI MACHO YANGU NKAENDA NDANI KUANGALIA HVO VIDONGE NA HICHO CHETI ZILE HABARI ZILIKUWA KWELI JAMAN NLIJITUPA KITANDAN NA KUPOTEZA FAHAMU.

ALIYENSTUA NI YULE MWANAMKE ALIVORUDI ALISHANGAA KUNIKUTA KTK HALI ILE, ALIPONIULIZA NIKAMPA ZILE HABARI, ALICHONIJIBU NI HKI! 'SASA KUSKIA HABARI HZO NDO UPOOZE HIVYO MBONA KAWAIDA TU, MBONA ME MGONJWA NA BADO NAISHI VIDONGE SI VIPO WE ULITAKA MI NIFE MWENYEWE HAPA TOWN WEWE'

DUUH!! YALE MAJIBU YALINCHOSHA NKAJIONA SINA THAMANI HAPA DUNIANI NTAWAAMBIA NIN WAZAZI WANGU ELIMU YANGU NI SAWA NA KAZI BURE DAAA'

MUWE MAKINI JAMAN,USIMUAMINI MTU KWA MACHO

Yamekukuta eeeeeeeeeeeeehhhhhhhh!!!!! Ndio dunia hiyo.
 
umemaliza kuandika ukasepa,coz watu wanauliza ila sijaona majibu,
pole sana,sa hapo unarudi nyumbani then waanza kumwambia baba na mama kuwa umekuaje vile? acha kabisa
 
Yani usije ukarudia tena, nasisitiza tenaa... Arusha unalala kwa mwanamke? tena mgeni alafu unalala 4 days, unapata na nguvu ya kufua? Hivi unapafahamu A-town vizuri? Aisee wangekukuta Ushawasikiaga akina Niaje Niaje, wazee wa kukata mabreki! Huyo mpenzi wako kwanza anaishi mtaa gani? Ngarenaro, Ungaleloo, Ngulelo, Kwa Mromboo, Kijenge, Sanawari juu, Kwa mrefu, Kimandolu (uwanjani) etc

Ila pole sana.
 
Back
Top Bottom