Yamenikuta... Sielewi nifanyeje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yamenikuta... Sielewi nifanyeje

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NgomaNzito, Dec 15, 2009.

 1. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nina boyfriend ambae sasa tumeanza mwaka wa pili kwenye mahusiano yetu na katika haya mahusiano kutokana na huyo jamaa kuwa ni mkorofi, mtemi na anayeamua mambo yake mimi kumsikiliza tu sitakiwi kupinga na hata nikipinga halitafanyiwa kazi, katika kuanza mahusiano yetu nikatambulishwa kwa mama mkwe na jamaa always huwa anadai kwangu ndo amefika kwani amefikia umri wa kuoa ana miaka 34 sasa lakini mahusiano yangu yamekuwa ni ya mateso sana.

  Jamaa yuko busy sana na friends zake na pia yuko bussy na ndugu zake tu yan mpaka nachokaga mwenyewe na always hayuko mwepesi kutamka mpenzi nimekumiss natamani kukuona labda mimi ndo niseme hivyo then acheck if possible ndo tumeet au niende kwao na yeye akiwepo, lakini mwendo ni kuangalia taarifa ya habari kwa kwenda mbele hana muda wa kuongea na mimi na kufanya mapenzi ni mpaka mwezi uandame kweli hii ni haki? Lakini mbali ya hayo yote nikawa navumilia kwa kuwa mipango yetu ni kuoana loh!

  Sasa juzi kati hapa nipo nae usiku wa manane simu yake ikaita nikapokea nikakutana na binti namuuliza anasemaje anasema anamhitaji jamaa nikamuuliza ni nani yako? akasema just a friend na hapo jamaa alikuwa hapo pembeni kawa mdogo ka sisimizi.
  Nikamwambia yule binti apige badae kidogo akasema poa.

  Baadae nikapiga simu nilichukua namba ya yule dada na namba ya demu mwingine nikaikuta nikachukua wote alikuwa anawasiliana nao bila mimi kujijua wakati tumekaa wote.

  Huyu demu wa kwanza akaniambia shosti ngoja nikwambie kitu huyo bwanako ni malaya mbwa sema tu mna mpango wa kuoana otherwise ningekwambia muachane na nakuomba tuonane nikupe list ya wanawake anaodeal nao kimapenzi ujionee miujiza tena shost ujiandae kukutana na ndoa ya matatizo mwanaume wako ni malaya aloshindikana yani dina nilisikia kufa we acha tu. Lakini yeye kama yeye akasema hana mahusiano naye.

  Demu wa pili akasema yeye kama yeye ni mpenzi wake tena wana miaka mitatu na aliwah kunisikia siku nyingi akamkanya, na jamaa amekiri huyu demu wa pili kweli alikuwa nae lakini sio sasa, huyo demu kwa sasa anajing'ang'aniza kwa maelezo ya jamaa, na cha ajabu dada dina huyo dada hatambuliki popote hata familia ya jamaa na ndugu wengi wananitambua lakini ndo hivyo kumbe nina mwenzangu lakini ndg wote wamekana hawamjui huyo binti. Na huyo binti aliniomba tuonane na akaniambia yuko tayari hata kuniita akiwa na jamaa nione mwenyewe kwa macho yangu lakini ukweli nimekataa kwenda kwenye appointment walizoniomba nisije kuchomwa kisu mie.

  Jamaa kwa kifupi kawakana wote kushiriki mahusiano nao.

  Sasa hebu nishauri ndugu yako huyu kweli anastahili kuwa wa maisha? Mbona ananipa jakamoyo la maisha?
  Kwa maana nimeshatendwa mpaka nahisi kuchanganyikiwa huyo ni mwanaume wa 4 kila nikikaribia kutambulishana nae nyumbani ukweli unajiweka hadharani mwisho wa siku namwaga manyaga naumia sana mpaka nakuja kusahau.

  Hapa nilipo sili karibu mwezi sasa na pia sina furaha muda wote kwa ajili ya mawazo na nimeshindwa kujisahaulisha na japo jamaa anajidai kunipenda lakini nimeshindwa kusahau hao wanawake kichwani kwangu na maneno waliyoniambia, so please naomba mnishauri m stressed najua mmekutana na mengi so naomba tushee haya mapito may be ushauri wenu unaweza kunipa matumaini mapya kuwa nifikie maamuzi yapi.

  Doreen.
   
 2. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  pole mwenzangu,huyu jamaa anatafanya kazi ?xul vip imepanda?wazazi wake wanasemaje kuhusu wewe?
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo ngomanzito=doreen?
   
 4. bht

  bht JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mpwa huyu si ndo alisema mkewe anahifadhi pedi wiki mbili??(corrrect me if am wrong) haya leo ana b.f!!
   
 5. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  miujiza yako kuliko ya moses. huli mwezi na bado uko hai? huh!
   
 6. GP

  GP JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  jamani kweli JF samutaimu kuna mauzauza!.
  nimekugongea senksi binamu kwa kufuatilia in lines.
   
 7. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  jamani ww dawa chungu,ushapenda ww?hali ndio si hivyo unavyofikiria,anakula lkn mawazo tele,si imeeandikwa mtu hawezi kuishi kwa mkate tuuuuuuuu?au hujui?
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ngoma nzito...hiyo story yako inaendelea kunihakikishia kuwa nyie wanawake wa siku izi suala la kuolewa mnalipa priority sana? Hivi huwezi kuwa na jamaa kwa ajili ya kula maisha tu mpaka uolewe? Unajua stress nyingine mi naona mnajitafutia wenyewe. Hivi unategemea kuna siku utapata mwanaume wa peke yako kwamba asiwe anamega nje? au asiwe na msururu wa mademu? Wewe kama unamuona jamaa kicheche kula kona, mbona njemba za kukupa starehe ziko kibao? tena unakuwa huru ukiona anakuletea uzushi simple unachimba kuliko kupenda kuolewa olewa kiasi kwamba mkiparangana mnaanza vikao na mambo mengine ya kupotezeana muda...Why?? Kwa niniiiiiii?? Utatafuta wa peke yako hutapata hata siku moja utaishia kufanyia maonyesho tu hiyo naniii kwa kila mtu mwisho unaonekana punch bag!!!
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tatizo kweli kweli!enewei TWENDE KAZI
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jamani ngomanzito amemkoti huyo Doreen siyo yeye (nadhani amepita kule kwa Leo tena).

  We Doreen unataka ushauriwe nini sasa? kwa nini usimwache tu tena kukingali mapema? Mimi sidhani kama hata wewe unampenda kihiiivyo (labda ni hiyo ndoa uliyoahidiwa na utambulisho uliofanyiwa) kwa sababu kama unempenda kiukweli basi hayo yote unayosema ni mkorofi n.k usingeyaona yaani ungekuwa blind kwa kila kitu maana si umeamua kupenda?! Unaniudhi sasa

  Make up your mind. RUN, RUN and RUN before its late
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  tatizo lako unakurupukaga kudanganya watu ukifikiri tumesahau pitia bandiko zako za nyuma then uone aibu.
   
 12. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Pole sana dadaaa, ila usife moyo ni wakati wa kufanya maamzui ambayo hayatakuumiza.

  Kutokana na experience uliyonayo nafikiri hata huyu siyo choice zaidi ya headache, sitaki ubase kwenye statement za hao wanawake waliojidai kukupa hizo information nataka ubase kwa kile ulichoandika mwenyewe kwamba hana muda na wewe zaidi ya yale mambo ambayo anayataka yeye. Hapo tayari ni tatizo.

  Mapenzi ni chachandu ya urafiki, kama yanafanyika kwa nadra hilo ni tatizo with reference kutoka kwa hao wadada wanaosema kwamba nao ni wadau katika mapenzi nae.

  Sasa basi dada wewe nikuulize swali how do you think about him? do you think anakufaa kwenye maisha yako kwa kuangalia ukubwa au udogo wa kile tunachoongelea hapa (tatizo).

  Endelea kuangalia kama hili tatizo linaendelea tangu umefumania hizo sms, je kuna badiliko? kama hakuna my dear piga moyo konde mwache aendelee na mambo yake, being 34 siyo kumfanya mtumwa wa mapenzi mwenzio.

  Ni hayo tu dada.
   
 13. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,503
  Trophy Points: 280

  Noted with thanks
   
 14. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  no comments!!! Enzi za ukimwi baba!!
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Akili mukichwa kila shetani na mbuyu wake naona wewe ndo umemganda kwa kunong'onezwa kaneno utaolewa! Kimbia wewe usigeuke nyuma alah..........
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  MI NADHANI UNAPOTOA STORY SEHEMU NI BORA KUKOTI UMEITOA WAPI,
  maana unatuchanganya last time ulionekana kama dume, story ya leo ni bint kwisha kazi, sasa hapa tunakushauri wewe Ngoma nzito au nanni,
  na huyo DINA ndani ya hiyo story ni nani?
   
 17. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kuna baadhi ya wanawake wazito kufikiri. sasa hapa ushauri wa nini?
   
 18. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mimi nadhani katoa kwenye ile blog ya dinalicious au ngonolicious. Tatizo hajaweka wazi kwamba nimeicopy kule kwa dina matokeo yake kila akiweka hapa story watu wanadhani ni zake. ametoa kwa din jamani. msameheni mwenzenu.
   
 19. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Nyie toeni ushauri na maoni kwa mdada kama hamna kaeni kimya
   
 20. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Jamani humu JF kuna maneno....kwa hiyo mapenzi nyie huwa mnafanya wakati wa sikuu za Eid tu?

  Halafu wanaume hapa mjini wako wengi tu mbona, unakuwa king'ang'anizi kwa mwanaume mpaka unamkera....! Maelezo yako niliyoyanukuu hapo juu yanaonyesha kabisa kwamba hakupendi ila unamng'ang'ania!
   
Loading...